Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Unadhani kulalamika 'live'' kwenye vyombo vya habari kutaondoa matatizo? Ile case ya yule mfanyabiashara wa Kariakoo ambaye inasemekena alijiua kwa kujipiga risasi huko Tabora ni funzo kwa mnaodhani kuwa kulalamika tu kunatosha.
Kulalamika hadharani ni njia bora zaidi kama mifumo imesinzia!! Inamuumbua mhusika lakini pia inaziamsha mamlaka!! Unawezaje kuiona kwamba hii siyo njia sahihi bila kuwa hata na suluhisha kama wewe pia SIYO TAPELI?? Sisi mnaotutapeli kila siku anatufariji sana Makonda
 
Kweli kabisa mkuu. Hii njia anayotumia Makonda itasaidia mambo mengi kubadilika.
 
Watu wameanza kulalamika leo? Mbona wakati wa Magufuli ndiyo ilikuwa ni kilele cha malalamiko? Makonda kaanza kusikiliza malalamiko leo? Huoni kuwa sisi matapeli tunaendelea kudunda huku ninyi wajinga mkipigwa ''mental masterbation''?
 
Kwa hiyo makonda kagundua Hilo??

Hii inatofauti Gani na yule mzungi aliyedai kugundua mlima Kilimanjaro wakati kina meku wako nao tangu kuubwa kwake

Punguzeni sofa za kijinga
 
Makonda anajua. Sio msomi ila amewakalisha/atawakalisha wengi TUNATAKA UTHUBUTU basiii
Ccm waliopotea akitokea kichaa moja akajaribu kufanya mambo ya kawaida sana wanamwona kama mungu

Hakuna jipya analofanya ambalo wengine hawajawahi fanya

Sema Huyu muhuni analipa waandishi njaa watangaze Kila upuuzi anaofanya
 
Ni kweli. Sifa zote za udikteta, uuaji, uporaji na upigaji watu risasi alizokuwa nazo jiwe na Makonda anazo
Na unadhan kwamba hayo uliyosema hayapo kwa viongozi? Kenedy ilikuwaje?John Fitzgerald Kennedy.
 
Mkuu ndiyo maana nikauliza ''kulalamika kunasaidiaje? Yaani umekiri kabisa kuwa alikosa msaada japo alisikilizwa! Kwani Tanzania ni Magufuli ndiyo tuseme kwa sababu alifariki basi kila kitu kilisimama?
 
Unadhani Makonda atakomaa na hilo jambo la huyo tapeli mpaka lini??
Mkuu anachofanya Makonda ni kujipa umaarufu kwa vitu vidogo ambaya sio rahisi yeye kuvimalizia.

Atawajaza kwa maneno makali kuzikoromea hizo mamlaka zilizowapuuza, huyo tapeli ataswekwa ndani kwa siku moja, baada ya hapo inabidi mrudie hatua zilezile mlizofeli mwanzo.
Na mpaka hapo Makonda hamtompata tena ili awadaidie tena.
 
Kwa mfano wanawake waliotelekezwa na waume zao na kuachiwa watoto bila kuhudumiwa mahitaji ya msingi.

Unafikiri nani source ya tatizo? Je kila tatizo ni CCM?
Hayo ni maigizo tu tena ya kijinga.Hapo utawasikia wadada wanaanza kuwataja watu kama ilivyokuwa kipindi kile et lowasa,gwajima ndo amenipa minba! Hah kweli ujinga mzigo
 
Unadhani kulalamika 'live'' kwenye vyombo vya habari kutaondoa matatizo? Ile case ya yule mfanyabiashara wa Kariakoo ambaye inasemekena alijiua kwa kujipiga risasi huko Tabora ni funzo kwa mnaodhani kuwa kulalamika tu kunatosha.
Kuandamana napo ni njia moja wapo ya kulalamika live. Kama njia zote unafata na bado hakuna muhafaka ni hatua gani zaidi? Kumloga au kumpiga lisasi
 
Kuandamana napo ni njia moja wapo ya kulalamika live. Kama njia zote unafata na bado hakuna muhafaka ni hatua gani zaidi? Kumloga au kumpiga lisasi
''lisasi'' ni nini jombi! Lakini hapa wanazungumzia kulalamika!
 
Watu wameanza kulalamika leo? Mbona wakati wa Magufuli ndiyo ilikuwa ni kilele cha malalamiko? Makonda kaanza kusikiliza malalamiko leo? Huoni kuwa sisi matapeli tunaendelea kudunda huku ninyi wajinga mkipigwa ''mental masterbation''?
Mkuu kulalamika inakuja Kama last resort. Kama haki yako inaminywa na umefuata all due process. Wananchi wengi wanakimbilia kwa Makonda kwasababu haki zao zinaminywa.
 
Mkuu ndiyo maana nikauliza ''kulalamika kunasaidiaje? Yaani umekiri kabisa kuwa alikosa msaada japo alisikilizwa! Kwani Tanzania ni Magufuli ndiyo tuseme kwa sababu alifariki basi kila kitu kilisimama?

Nadhani jamaa alijiua baada ya msingi wa mawazo. Maana wamekaa vikao na Waziri Mkuu zaidi ya kimoja na hakuna hatua zilizochukuliwa. Nadhani kulalamika kwake kujifanya taifa lijue kinachoendelea na kuweka record straight.
 
Serikali inaruhusu wahujumu na matapeli nchini na wale mikopo kaush damu kama Platinum,Bayport n.k!

Eti ni sehem ya intelligence ya kuwatawala watz waendelee kuwa chini kiuchumi!!

Huyo unaemwita tapeli ni sehemu ya mpango kazi wa kitapeli kama Deci vile!!

Unakuta ni mtu ambae system inamtambua kabia na yupo Kwa malengo maalum!

Ukiona mtu mwovu hachukuliwi hatua ujue ni sehemu ya system tu ndivyo ilivyo!!

Hii nchi Kuna vitu vya ajabu sana vinaruhusiwa kwa sababu maalum!!

Unafikiri kwanini Rama was kariakoo alijipiga risasi Kwa kutapeliwa fedha !!?

We achana nae huyo jamaa!!kama hachukuliwi hatua ni dhahiri shahiri analindwa na mfumo kabisa!!

Hats hizi deals zinazopigwa plus wizi vinalindwa na na system kwa ujumla!kama havilindwi kwanini vipo!!?

Ndivyo ilivyo!
 
Mkuu nakubali unachosema. Ila kwa Sasa tupo desperate hivyo ni Bora atakaye tusaidia hata robo au nusu kuliko ambaye hawezi kutusaidia.
 
UWONGO!! Mhimili wa Mahakama hauingiliwi na paka yoyote kama Makonda
Soma sheria aliyozungumzia Makonda utaelewa vizuri, kwenye maelezo yake amesema lazima kuwepo na "checks".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…