Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kuandamana napo ni njia moja wapo ya kulalamika live. Kama njia zote unafata na bado hakuna muhafaka ni hatua gani zaidi? Kumloga au kumpiga lisasi
Mambo yakiendelea hivi usishangae anapigwa risasi na raia. Maana ameliweka jeshi la polisi mfukoni.
 
Nashukuru mkuu imenifumbua macho. Umeongea mambo ya msingi Sana.
 
Ipo siku mtanielewa vyema napomuona na kuwaambini kuwa Mwamba Mwenyewe Makonda kama kiongozi Mwenye uchungu na maisha ya watu wanaonewa na kunyanyaswa. Ipo siku mtafahamu kuwa Mwamba Makonda anapigwa vita na kushambuliwa na kuchafuliwa na watenda maovu ,wezi,matapeli,wauza madawa ya kulevya ,madhulumati na ambao matumbo yao yamejaza chakula cha dhuluma. Makonda amejitoa na kujitolea kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kusaidia na kuhakikisha watu wanapata haki zao.

Nitaendelea kumsemea na kutetea Mwamba Makonda hata nikiitwa chawa na kutukanwa matusi yote. Lazima mfahamu hatari kubwa iliyopo kwa mtu kupambana na wenye pesa au mamlaka au vyeo vikubwa wanaotumia nafasi zao kuonea watu na kuwakandamiza. Lakini Mwamba Makonda ameamua kutoa na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kuwapambania wanyonge. Halafu anatokea mlevi mmoja na mabango yake kichwani anaropoka mitandaoni au hadharani eti kuwa ni maigizo.hii yote ni kutaka kumkatisha tamaa Mwamba Mwenyewe Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.
 
''lisasi'' ni nini jombi! Lakini hapa wanazungumzia kulalamika!
Jombi ni nini kiongozi? Uwe Unatoa japo idea basi nini kifanyike unaweza kua na idea nzuri za kumsaidia mtu. Usiwe mtu wa kupinga tu bila kuja na wazo la mtu kumsaidia mwenyetatizo.
 
Mkuu econonist hii mada yako umeniwahi Tu kuandika aisee ila haya mawazo yako yalikuwepo kichwani mwangu hasa juu ya makonda huyu jamaa hata kama tunamkataa na kumkebehi Ila anachofanya yupo Sahihi kabisaa.
Sisi Tanzania huwa hatujui nini tunataka huyu makonda angekaa ofisini Tu tungelaumu kwanini hafanyi kazi lkn sasa anonekana yupo field anaoneka anaigiza yaani kwakifupi watanzania ni wajinga sana

Japokuwa CCM naichukia Ila makonda namkubali Sana siasa zake na ninamuunga mkono kwenye uongozi wake, makonda kama anasema hizi mada zetu naomba asirudi nyuma kwenye harakati zake za kusaidia watanzania wa Hali ya chini

MUNGU akutangulie Paul makonda
 
Upo Sahihi kabisaa mkuu!!!!!
Wengi ambao wanamkataa makonda ni watu wenye wivu Tu kama ilivyo kawaida ya watanzania ni watu wenye wivu wa maendeleo
 
Uko sahihi mkuu wangu, lakini hata huyo Makonda anasikiliza na kutatua kero nyepesi. Nakuhakikishia ukimpelekea Makonda hiyo kero hakuna kitu atamfanya, maana utakuta watu wa aina hiyo ndio huwa wanatumika kupora uchaguzi Ili ccm ikae madarakani.

Ukitaka kujua kupiga kelele hakuwatishi, Kuna yule jamaa alijiunganishia bomba la mafuta nyumbani kwake akakutwa, waziri mkuu aliunda hadi tume na akaahidi hadi kutoa taarifa hadharani, hakuna lolote limesemwa hadi leo! Wangekuwa na nia ya dhati wangewezeaha mifumo kufanya kazi.
 
Labda anaisaidia serikali kupunguza nakisi ya bajeti. Kama juhudi zote hizo na hakuna analifanyia kazi.

Kingine labda ni mshirikina, maana pia usibeze hiki kipengele, maana yasemwayo yapo.
 
Elezea hao One 2 One Focus Limited na huyo Mwamwega wamafanya utapeli gani au makosa yao ni yapi. Malalamiko mengine ya wabongo dhidi ya matajiri na biashara zao ni kwa sababu ya kukosa uelewa na hulks ya ujamaa wa Nyerere ya kubeba zaidi wasio matajiri.
 
Zile zilikuwa fix tu mkuu.

Ila ushauri mwingine mwepesi ni kuchukua sheria mkononi. Sisi tutasomewa tu kuwa wananchi wenye hasira kali, geshi linaendelea kuwatafuta.
 
Vyombo vya dola sio wagawa haki, mahakama pekee ndio kinapaswa kuwa chombo cha ugwaji haki na maamuzi ya nani ana haki. Kinachopaswa kufanyika ni mfumo wa Mahakama uboreshwe watu wasikimbile vyombo vya dola kupata haki kwa sababu ni precedent mbaya sana.
 
Uthubutu tu wa kuanzisha jambo binafsi naona unasaidia sana kuliko kutokufanya. Makonda endelee tu bila kujali limevuka mipaka gani, maana hao wenye mipaka yao hawafanyi kitu.
 
Njia sahihi ni watu wote kufuata utaratibu wa kimahakama au usuluhishi wa wanasheria kupata haki zao, ni jambo baya sana kuvigeuza vyombo vya dola kuwa wagawa haki, hiyo ni mifumo ya Kangoroo courts.
 
Mkuu nakubali unachosema. Ila kwa Sasa tupo desperate hivyo ni Bora atakaye tusaidia hata robo au nusu kuliko ambaye hawezi kutusaidia.
Hizo Kangoroo courts zinaweza kutuliza mambo kwa muda mfupi tu ila huwa zinaweza kugeuka na kuwa mwiba mkali.
 
Makonda amesema ni ngumu kupata haki mahakamani, anajua ni kwa kiwango gani mahakama zimeoza. Hivyo ametumia udhaifu huo kupatia kiki, badala ya kuhakikisha mahakama zinafanya Kazi kwa usahihi!
 
pigia mstari huyo tapeli ana baraka zote za hao wakubwa wa nchi. ukizaliwa afrika ni laana unayopaswa kupigana ama na wewe na lineage yako muwe high table au uondoke kwenye bara hilo la kuzimu.
nashukuru Mungu siishi huko ukimani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…