Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Mm simkubali sana sa100 ila kwa kauli chafu alizotoa kwa rais ambaye mm namuona kama mama kwa kweli kakosea na huyo mpuuzi mange ana wadhalilisha sana watu hana adabu hivi tunataka aje amtukane nani na kumdhalilisha nani ndo tutamchukulia hatua.
 
He is just a populist. Nothing more.

Ametatua shida gani za wananchi? Nipe mfano?
Alipokuwa,mwenezi CCM,tumeshuhudia alivyokuwa kimbilio la wananchi kwenye ziara zake [mikoa tofauti],jinsi alivyokabiliana na changamoto zao kwa kuwabana viongozi/watumishi wavivu, miungu watu,mafisadi,dhulumati n.k.na baadhi yao walipatiwa suluhisho hapohapo [kitu ambacho Samia S.H.hajawahi kufanya na hawezi],alipokuwa mkuu wa mkoa Dar es salaam alidiriki kutenga siku 2 za wiki,maalum kwaajili ya kuwasikiliza wananchi[malalamiko na kero zao]ofisini kwake.
 
..mbona Uvccm wanatukana viongozi wa upinzani matusi makubwa kabisa na watu wanavumilia?

..Rais aonyeshe uvumilivu na ukomavu kama kiongozi.

..Mtu huyuhuyu alimsingizia mwenzake ugaidi na akamfunga kwa miezi minane, leo kasemwa kidogo analialia.
Hivi alisingiziwa ugaidi ama Mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu halafu “Serikali kupitia kwa DPP ikaamua kuachana na kesi?

Kwanini alitoka gerezani na kwenda moja kwa moja Ikulu kuzungumza na Rais? Walizungumza nini?

Viongozi wa upinzani wanaotukanwa na wanavumilia ni kwamba wameamua kuvumilia kwa sababu sheria ziko wazi kwanini wasiwawajibishe watukanaji wao?
 
Mtoa mada umesahau kuamini waganga/kurogwa,kutoana mapepo,miujiza,maji ya upako,Imani za dini za kitapeli na kuombewa .

Watu wanategemea maendeleo yatoke kwenye hayo mambo 😂😂😂😂
 
Acha maneno jibu swali ametatua changamoto gani???

Yale yalikuwa maigizo tu kama maigizo mengine kuwarubuni watu msio na akili kama wewe.
 
Em ngoja tuone kunakuchaje...
Huyu Makonda akisurvive next 12 hrs..

Basi hatuna Nchi.
Ni kweli mkuu ikifika Jumatatu tarehe 15/04 kama Makonda atemdelea kuwa RC Arusha basi, nchi yetu itakuwa ya HOVYO
 
Na usipoamini hivyo vitu nafasi yako ni ndogo sana kwenye siasa na jamii
Ili kujihusisha na wajinga,unatakiwa kuwa sehemu ya hayo kimkakati ila sio kiimani maana ni uongo na Utapeli but wajinga wanajua Yana ukweli na watapata wanachotaka via hayo mambo
 

..mimi nilifuatilia ile kesi na nimeridhika kwamba ilikuwa kesi ya uongo na hila mbaya dhidi ya Mbowe.

..Na kama kweli Mbowe ni gaidi kwanini Dpp aliondoa kesi? Vilevile kwanini Rais alimkaribisha gaidi Ikulu?

..wanaotukana wapinzani ni viongozi wa Ccm, na serikali. Wengi wao ni wateule wa Rais wa Jamhuri na Mwenyekiti wa Ccm.

..Sasa tunajiuliza, kwanini Rais anateua watu wenye lugha za matusi na udhalilishaji?

..Malalamiko kwamba Rais anatukanwa yana maana gani ikiwa yeye mwenyewe ameteuwa ktk serikali na chama watu wenye rekodi za kutukana na kudhalilisha?
 

Srma Makonda anawin watu wa akili ndogo. Siyo wote wenye kipato cha chini wana akili ndogo.
 
Wewe ukijilidhisha kwamba kaonewa hiyo inatosha kubadili msimamo na maneno ya Mahakama? Wewe ni nani?

DPP aliondoa kesi kwa niaba ya Serikali, tujiulize mimi na wewe kwanini?

Na Mimi nimekuuliza kwanini alitoka Jela na kwenda moja kwa moja Ikulu kuzungumza na Rais ambae Serikali yake kupitia Mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu? Walizungumza nini?

Mtu kuwa mteule wa Rais na Serikali yake haina maana kwamba Tabia zake za hovyo ni wajibu wa Rais, awajibishwe huyo mtu kwa mujibu wa sheria na taratibu kinyume na hapo sympathy is for cowards.

Kwamba Rais anafanya makusudi kuteua watu ili wawatukane upinzani? Hao upinzani ni wajinga kiasi gani hawajui njia ya kufuata kuwawajibisha wakosaji wao?

Hiyo aya ya mwisho ni hoja kabisa kutoka kwako ama unatania? Kwamba Rais anapoteua anajua kabisa huko mbeleni mdomo wako utageuka choo Kwahiyo anafanya kusudi?
 

..Sawa.

..Wapinzani wanatukanwa.

..Raisi anatukanwa.

..Ngoma droo!!

..Kazi iendelee.
 
Kama naanza kukuelewa kwa karibu sana,Mbowe ni masta maind wa kasikazini,ni mpangaji wa matukio na sio matukioa madogo,Kama lile la kusema kapigwa kumbe alilewa akaanguka kwenye Ngazi akaumia mguu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…