Naona anazunguka tu mbuyu, mtalii anapokuja Arusha anajua nini anakuja kufanya, na anaweza kwenda popote muda wowote, tatizo kubwa ni hapa;
1. USALAMA DUNI
-Matukio ya uharifu mdogo mdogo na makubwa ni mengi kupita maelezo huko mitaani.
-Maeneo mengi usiku ni giza, hakuna taa za barabarani, mitaani, maeneo ya wazi, maeneo ya umma.
2. UCHAFU KUPITILIZA
-Barabara chafu
-Mitaro imeziba na imejaa uchafu
-Masoko machafu
-Migahawa michafu
-Vyoo vya umma vichafu
-Chemba za maji taka ziko wazi na kutiririsha maji machafu na vinyeji hadi katikati ya jiji.
3. USTAARABU DUNI
-Bei za bidhaa na huduma zimejaa ubaguzi na ujanja ujanja mtupu (Kuna bei za mtanzania na kuna bei za mtalii, Why? Mnadhani kuna mtalii anapenda huo ubaguzi wa wazi?)
-Viwango vya huduma na bidhaa ni duni kupita maelezo. (Yaani mpaka leo bado watoa huduma na wauza bidhaa wanashindwa kuweka price tag, bei zinatolewa mdomoni kwa kukuangalia rangi ya ngozi yako, umevaaje, unaongea lugha gani nk)
-Mipango miji mibovu. Yaani biashara na huduma zimetandazwa chini barabarani kila mahali.
-Urasimu (ni rushwa tu) umejaa kila kona, kuanzia barabarani kwa matrafiki (yaani wanaweza kukusimamisha bila kosa, wakakuweka zaidi ya robo saa barabarani kutafuta kosa), airport nk.
4. MIUNDO MBINU MIBOVU
-Mvua kidogo tope kila mahali
-Jua kidogo vumbi kila kona
-Barabara nyingi hazina mitaro, mvua ikinyesha kidogo hazipitiki
-Mitaa haina vibao, barabara hazina vibao.
Sasa warekebishe hizo mambo halafu uone kama kuna mtalii atakwepa kuja Arusha.