Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mimi naendelea kuwapeni habari tofauti tofauti na mchanganyiko bila kuchoka .pia msichoke maana maisha ndio haya haya na nchi yetu ndio hii hii na watanzania ndio hawa hawa.
Ipo hivi kuna wimbo umemuonyesha Mkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa Makonda akicheza na kuimba kwenye gari lake, katika wimbo unaoitwa NAMLETA MAMA SAMIA. Video hiyo ambayo imeendelea kusambaa na kufurahiwa na watu wengi juu ya wimbo huo ambao umetungwa na msanii wa bongo freva Diamond.
Mhessimiwa Makonda mwishoni wa wimbo huo baada ya kumaliza kucheza wimbo huo amesema tukutane 2025. Hii ikimaanisha ni miongoni mwa nyimbo kali zitakazotikisa na kutumiwa wakati wa kampeni za Urais wa Rais Samia ,ambaye mamilioni ya watanzania wamekuwa wakiipigia magoti na kuisihi sana CCM kuhakikisha jina la Rais Samia linarejeshwa kwa wananchi kama mgombea pekee wa CCM atakaye peperusha bendera yake ili wampigie kura za ndio kwa kishindo kama sehemu ya kutoa shukurani kwake kwa utumishi wake uliotukuka.
Tuendelee kutulia na kuendelea kufurahia utawala wa mama yetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan,ambaye anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Video nitaangalia namna ya kuwawekea ila kama unaweza ingia moja kwa moja kwenye instagram ya Diamond ujionee mwenyewe badala ya kuhadithiwa na Mwashambwa.
Mwisho nawasihi tu japo siyo kwa umuhimu,kuwa tuendelee kupendana sana watanzania,kuwa wamoja, tushirikiane, tusaidiane na tuwe kitu kimoja katika mambo yanayogusa maslahi ya Taifa letu.tusichukiane bila sababu wala kuumizana sisi kwa sisi. Duniani ni wapitaji tu ndugu zangu.hasira ya nini.wewe furahia maisha yako hata kama una lala njaa wewe jipe moyo tu kuwa kesho nayo ni siku Mungu atakupatia chakula.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.