Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda ametembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yaliyoathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha.

Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametembelea maeneo ya Sakina na Mianzini, maeneo ambayo yameathirika zaidi na mvua, kiasi kilichosababisha vifo vya watu 6 na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo,Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda amewataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua pamoja na kuhama katika maeneo yenye historia ya kuwa na mikondo ya maji.

Aidha Mh.Makonda pia amewataka viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha ikiwemo Maafisa wa mipangomiji kufanya vikao vya Dharura kwenye maeneo yao ili kupata Tathimini ya maeneo yao na hatari iliyopo kwenye makazi ya wananchi endapo Mvua zitaendelea kunyesha.

FB_IMG_1713131700576.jpg

FB_IMG_1713131706203.jpg
FB_IMG_1713131693889.jpg
FB_IMG_1713131687742.jpg
FB_IMG_1713131678238.jpg
FB_IMG_1713131673596.jpg

PIA, SOMA:

Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
 
Mh Makonda, kishimba, Mpina. Ni watu kwa kiasi chake wanasimamia wanachokiamini bila hofu ya mitazamo ya watu

Makonda kaibua madudu

Mleta madudu kaibuka

Wapishi wa madudu wakaanza vikao😄
 
jeshi la manyumbu, mavuta bangi na manywa visungura sio, au lile la mihemko na matusi 🐒

kwahiyo kikosi kazi ndio kimependekeza machafuko na mapinduzi ya kijeshi 🤣

🐒au hayo ya machafuko ya kijeshi ni mapendekezo yako na manyumbu wenzio baada ya kuvuta na kunywa visungura, mnajiona nyie ni Jeshi la manyumbu, right 🤣
Tulia 🌈
 
Ila CC TANAPA kadhalililka sana kwenye kile kikao
Tatizo lakuwapa watu wasimamie mambo ambayo siyo fani zao.Huyo mzee miaka yake yote alikua anashughulika na mambo ya uhasibu leo unamleta asimamie mambo yote ya utalii na uhifadhi plus jamii itakavyonufaika na hiyo taasisi lazima maelezo yapelee.
 
Wangapi wanaijua? Na inatangazwa vyakutosha? Ina nini chakufanya hadi mtu akija Arusha asikose kupita pale?
Inajulikana sana tu , na si tuu hiyo kuna makumbusho nyingine ipp karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa. culture heritage inatembelewa sana, wabongo ndio hawatembelei ( kama kawaida yao hawafhamini vya kwao)
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi naendelea kuwapeni habari tofauti tofauti na mchanganyiko bila kuchoka .pia msichoke maana maisha ndio haya haya na nchi yetu ndio hii hii na watanzania ndio hawa hawa.

Ipo hivi kuna wimbo umemuonyesha Mkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa Makonda akicheza na kuimba kwenye gari lake, katika wimbo unaoitwa NAMLETA MAMA SAMIA. Video hiyo ambayo imeendelea kusambaa na kufurahiwa na watu wengi juu ya wimbo huo ambao umetungwa na msanii wa bongo freva Diamond.

Mhessimiwa Makonda mwishoni wa wimbo huo baada ya kumaliza kucheza wimbo huo amesema tukutane 2025. Hii ikimaanisha ni miongoni mwa nyimbo kali zitakazotikisa na kutumiwa wakati wa kampeni za Urais wa Rais Samia ,ambaye mamilioni ya watanzania wamekuwa wakiipigia magoti na kuisihi sana CCM kuhakikisha jina la Rais Samia linarejeshwa kwa wananchi kama mgombea pekee wa CCM atakaye peperusha bendera yake ili wampigie kura za ndio kwa kishindo kama sehemu ya kutoa shukurani kwake kwa utumishi wake uliotukuka.

Tuendelee kutulia na kuendelea kufurahia utawala wa mama yetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan,ambaye anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Video nitaangalia namna ya kuwawekea .ila kama unaweza ingia moja kwa moja kwenye instagram ya Diamond ujionee mwenyewe badala ya kuhadithiwa na Mwashambwa.

Mwisho nawasihi tu japo siyo kwa umuhimu,kuwa tuendelee kupendana sana watanzania,kuwa wamoja, tushirikiane, tusaidiane na tuwe kitu kimoja katika mambo yanayogusa maslahi ya Taifa letu.tusichukiane bila sababu wala kuumizana sisi kwa sisi. Duniani ni wapitaji tu ndugu zangu.hasira ya nini.wewe furahia maisha yako hata kama una lala njaa wewe jipe moyo tu kuwa kesho nayo ni siku Mungu atakupatia chakula.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Hivi una muda hata wa kukumbuka kuwa kuna mama Yako mzazi alikuzaa
 
photo_2021-08-11_09-06-26.jpg
 
Jana nimeona kikao baina ya RC Makonda na wafanyabiashara wa hotel na TRA na tours. RC kauliza vitu vingi na kashangaa iweje mzungu atoke Ulaya aje kulala badala ya kutalii.

Napenda nitoe ushauri, wakati fulani tulisoma kozi na serikali ya China katika hizo kozi kuna kitu kinaitwa Night tourism, hapa maeneo mengi nchini China utalii unafanyika mpaka usiku. Mfano private tours at night in the city, museums.

Kuna maeneo unapata local food usiku mzima, wenzetu wana utalii wa mito sio kama sisi mito yetu yote tumekonect maji taka.

Kwa Arusha ili jiji liwe vibrant ni lazima shuguli za utalii ziwe 24hrs. Wengine wanapenda kwenda museums usiku pametulia, uliza Arusha kuna Museum inayoeleweka?

Mtalii anaweza kutaka local foods at night je zipo sehemu hizo? Usalama je? Naamini watu wa Arusha wanaelewa utamu wa hela ya mzungu kama mazingira mheshimiwa atapambana kuyaweka sawa jamaa watapiga kaz.

Nimemskia yule jamaa kichwa Chambulo anasema kalipa mil 23 kapewa risit ya mil 3. Yule ana ideas nyingi za kuhakikisha mzungu anabakiza nauli tu ya kurudi kwao. Hapo Arusha itapaa kiutalii.

TTB pale nothing creative nothing no museums hakuna tradition wataalam wamekaaa hata huko Dodoma kukimbiza madokezo ya poshoook tu.
Watalii wanakuja Arusha pekee? Arusha ni transit wakishuka wanalala kesho yake wanaenda Polini na either wanaondokea huko kwendza Zanzibar na kwingineko. Watalii hawakaagi Arusha mjini, wakae kutalii nini? kuna kitu gani pale? Bora waende Zanzibar.

Kwenye utalii wa miji Zanzibar ndio inawavutia kwa yale majengk na fukwe basi.
.Arusha mjini hakuna kivutio hata kimoja cha kuwa atract wao.
 
Tulia 🌈
Tulia ni mbunge asietikisika, anakubalika mno na anaependwa sana Jimbo la Mbeya mjini, lakini pia ni speaker wa bunge Tukufu la JMT, zaidi sana Ni Rais wa shirikisho la Mabunge duniani 🐒

au unazungumzia Tulia gani 🐒
 
Back
Top Bottom