Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda ametembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yaliyoathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha.

Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametembelea maeneo ya Sakina na Mianzini, maeneo ambayo yameathirika zaidi na mvua, kiasi kilichosababisha vifo vya watu 6 na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo,Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda amewataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua pamoja na kuhama katika maeneo yenye historia ya kuwa na mikondo ya maji.

Aidha Mh.Makonda pia amewataka viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha ikiwemo Maafisa wa mipangomiji kufanya vikao vya Dharura kwenye maeneo yao ili kupata Tathimini ya maeneo yao na hatari iliyopo kwenye makazi ya wananchi endapo Mvua zitaendelea kunyesha.




PIA, SOMA:

Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
 
Mh Makonda, kishimba, Mpina. Ni watu kwa kiasi chake wanasimamia wanachokiamini bila hofu ya mitazamo ya watu

Makonda kaibua madudu

Mleta madudu kaibuka

Wapishi wa madudu wakaanza vikaoπŸ˜„
 
Tulia 🌈
 
Ila CC TANAPA kadhalililka sana kwenye kile kikao
Tatizo lakuwapa watu wasimamie mambo ambayo siyo fani zao.Huyo mzee miaka yake yote alikua anashughulika na mambo ya uhasibu leo unamleta asimamie mambo yote ya utalii na uhifadhi plus jamii itakavyonufaika na hiyo taasisi lazima maelezo yapelee.
 
Wangapi wanaijua? Na inatangazwa vyakutosha? Ina nini chakufanya hadi mtu akija Arusha asikose kupita pale?
Inajulikana sana tu , na si tuu hiyo kuna makumbusho nyingine ipp karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa. culture heritage inatembelewa sana, wabongo ndio hawatembelei ( kama kawaida yao hawafhamini vya kwao)
 
Hivi una muda hata wa kukumbuka kuwa kuna mama Yako mzazi alikuzaa
 
 
Watalii wanakuja Arusha pekee? Arusha ni transit wakishuka wanalala kesho yake wanaenda Polini na either wanaondokea huko kwendza Zanzibar na kwingineko. Watalii hawakaagi Arusha mjini, wakae kutalii nini? kuna kitu gani pale? Bora waende Zanzibar.

Kwenye utalii wa miji Zanzibar ndio inawavutia kwa yale majengk na fukwe basi.
.Arusha mjini hakuna kivutio hata kimoja cha kuwa atract wao.
 
Tulia 🌈
Tulia ni mbunge asietikisika, anakubalika mno na anaependwa sana Jimbo la Mbeya mjini, lakini pia ni speaker wa bunge Tukufu la JMT, zaidi sana Ni Rais wa shirikisho la Mabunge duniani πŸ’

au unazungumzia Tulia gani πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…