Ni kweli unampenda Sana Makonda, na hii huwa inatokea mtu fulani kumpenda mtu fulani automatic, inatokana na ku share spiritual rim, njozi na maono ya pamoja.
Ni kweli Makonda kwako ni kijana mtiifu na mnyenyekevu amekuwa hivyo tangu akiwa Mkuu wa Mkoa, alipotoka, alipokuwa mwenezi na sasa Mkuu wa Mkoa Arusha
Kwako binafsi hakuna baya lolote alilofanya na sababu unampenda hata akifanya kosa kwako huwa ni kosa dogo la utoto ambapo unaamini atajirekebisha
Madhara ya tabia za Makonda na consistence ya tabia hizo
1. Hulka ya kupenda ukuu, cheo na sifa:
a) ilianza kuonekana alipokuwa Mkuu wa Mkoa alijilinganisha na mawaziri na kuonekana mawaziri hawana lolote dhidi yake Mkuu wa Mkoa, kuna wakati alikua na msafara mkubwa kuliko waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
Hulka hio ameendelea nayo alipokuwa mwenezi, alimdharau RC Chalamila mbele ya Kadamnasi, akamwagiza Waziri Mkuu Majaliwa kama yeye ndio Mkuu wa Chama, akifanya hivyo kwa mawaziri na ikapelekea baadhi yao kutokubaliana nae yupo Bashe ambaye alitoka hadharani kuonesha kutokukubaliana na maagizo ya Makonda swali je Cheo Cha katibu Mwenezi ni Command kwa Waziri Mkuu na Mawaziri .. Hilo nakuachia wewe Kadinali Pengo ujibu.
B. Akajipa msafara wa magari na kuwa yeye ndiye mtu anayewindwa Sana auwawe mara afanye ziara mkoani alale Dar kwa Maaskofu.
C. Akagoma kufuata maelekezo ya Katibu Mkuu Comred Nchimbi, Kadinali wewe unajua Askofu Mkuu wa Jimbo ndiyo mkuu wako wa kazi kama wewe ni padri au askofu msaidizi sharti ufuate maelekezo yake, kazi yako inakuwa kupeleka ushauri na mapendekezo na kuomba kibali cha utekelezaji. Makonda hakutaka kufuata uratibu wa kawaida kuwa ndani ya Chama Yuko chini ya Katibu Mkuu, Bali yeye alitaka ndio asikulizwe na aongoze, kwa kuwa hakuwa cooperative hii kitu imekisumbua Sana Chama ndipo Rais kaona isiwe tabu ampe ukuu wa Mkoa kwa sababu ni dhahili anagombana na kila mtu ndani ya Chama.
d. Imetokea tena alipofika Arusha, kujikusanyia Msafara wa Magari, Gari yake ya RC tena yenye bendera kupakia watoto wake (watu wa protocol wanaelewa zaidi je bendera na plate namba yenye cheo fulani inaweza kutumika ndivyo sivyo..?)
haya Leo tena kutuhumu mawaziri kuwa wanamtukana Rais hili jambo limefedhehesha Baraza la mawaziri, nchi na vyombo kwa ujumla, je ni kuwajulisha mawaziri kuwa hawezi kuwatii sababu kimsingi mkuu wa mkoa si mkubwa kwa Waziri ndio mana yuko chini ya Tamisemi. Kwan kauli hio Makonda kajitwalia uwaziri Mkuu wake na kuonesha baadhi ya mawaziri hawana hadhi ya kumtuma kwa kile tuu yeye anawaona wanamtusi Rais wa JMT
Hii tabia yake ya Ufitini, uchonganishi, kupenda madaraka, uzushi na uongo bado kwako Kadinali unaonaje ni makosa madogo....?
Vipi kwa Baraza la mawaziri wanaichukuliaje na wanamchukuliaje kijana wako kipenzi?
Viongozi wanaishi kwa kuheshimiana hata kama hawajakubaliana, mfano Kinana na Nchimbi, wapo washindanu January na Mwigulu wote hao si kitu kimoja lakini wanaishi kwa kuheshimiana bila kuvuka mipaka
Uungwana ni kitendo
Kama Kadinali utamwacha Makonda na tabia hizi lambda kwako ndio sifa za uongozi, Sisi tunasema Yetu Macho