Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Makonda anaishi wa fitina, chuki, kujipendekeza na kujifanya yuko karibu na viongozi. Kiufupi ukimuondolea hayo, hana lolote la kumfanya kustahili kupewa nafasi anazopewa.

Bahati mbaya nchi yetu saivi tumeachana na masuala ya merit katika kupata nafasi za juu za uongozi badala yake tunazingatia uchawa, kujipendekeza, fitina, chuki na kujuana.

No wonder in very few years to come tunaweza kuja kuwa failed state kama hatujabadilika.
 
Tarehe 13 mwezi uliopita, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa msimamo wake kama mkuu wa nchi na wa CCM kuhusu 'makundi' na 'watoto' wake kisiasa.

Katika hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Samia alisema kwa umakini, umadhubuti na wazi kabisa kuwa yeye hana makundi wala watoto ndani ya chama chake na Serikali.

Rais Samia akaenda mbele na 'kuwakemea' wote wanaojitanabaisha kuwa ni watoto wa Mama au wa kundi la Mama. Alihitimisha kuwa viongozi wote kwa ujumla wao ni watoto wake.

Jana, kwenye Maadhimisho ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, RC Makonda amesikika akijitanabaisha kuwa yeye ni mtoto wa Rais Samia. Amesikika mara mbili akisema 'Mama yangu' kwenye kauli zake, tena mbele ya Rais Samia.

Kwanini Makonda atofautiane na kukinzana na msimamo wa Rais Samia kwa kujitaja kama 'mtoto wa Mama Samia'? Makonda alilenga au analenga nini?
Wakati wa hotuba yake alimjibu nini Makonda kama ulisikiliza?
 
Maisha ya huyu kijana siku zote ni yale ya kumtegemea mtu wa juu. Hajawahi kuishi maisha ya peke yake.

Tangu anatoka kwao Kolomije, alifika mjini na kukishikisha kwenye familia ya marehemu Samweli Sitta, baadaye akaenda kwa marehemu Edward Lowasa, akahamia kwa kina Riz One, baadaye akamimbilia kwa JPM, na sasa yupo kwa Mama!

Huyu dogo mara zote hupenda kujishikisha sehemu ambayo itampa usalama wa kisiasa. Na akitoka kwa Mama ataangalia sehemu nyingine salama zaidi ya kujishikiza. Na hayo ndiyo maisha yake siku zote. Kiufupi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa huu mfumo wa kuishi maisha ya kinafiki na kujipendekeza kwa watu wa ngazi za juu ili kunufaika kisiasa na kiuchumi.
 
Tarehe 13 mwezi uliopita, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa msimamo wake kama mkuu wa nchi na wa CCM kuhusu 'makundi' na 'watoto' wake kisiasa.

Katika hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Samia alisema kwa umakini, umadhubuti na wazi kabisa kuwa yeye hana makundi wala watoto ndani ya chama chake na Serikali.

Rais Samia akaenda mbele na 'kuwakemea' wote wanaojitanabaisha kuwa ni watoto wa Mama au wa kundi la Mama. Alihitimisha kuwa viongozi wote kwa ujumla wao ni watoto wake.

Jana, kwenye Maadhimisho ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, RC Makonda amesikika akijitanabaisha kuwa yeye ni mtoto wa Rais Samia. Amesikika mara mbili akisema 'Mama yangu' kwenye kauli zake, tena mbele ya Rais Samia.

Kwanini Makonda atofautiane na kukinzana na msimamo wa Rais Samia kwa kujitaja kama 'mtoto wa Mama Samia'? Makonda alilenga au analenga nini?
Makonda sometimes 'yes' sometimes 'no'........
 
Back
Top Bottom