Kwema Wakuu!
Usijeleta u-serious wako uwapo mbele ya Watanzania. Mambo ya akili mingi watanzania hawayataki, mambo ya kweli watanzania sio Wafuasi wake.
Ndio maana kijamii sio ajabu ukawakuta Watu kama kína Mwijaku, Dotto Magari, Piere Liquid, kina Mange Kimambi, na wengineo wakiwa na influence ndani ya jamii ya Tanzania.
Watanzania wanapenda udaku, habari za uongouongo na uzushi, habari za kufarakana na kufarakanisha, umbeaumbea. Habari za connections za video za ngono ndio watanzania wanazozipenda.
Habari za usimba na Uyanga, udiamond na ualikiba. Ndio mambo yenyewe hayo.
Niliwahi andika makala fulani miaka kadhaa nyuma kuwa úkitaka kutoka na kufanikiwa hapa Tanzania, Basi wekeza kwenye mambo ya ujingaujinga.
Watanzania wengi kwenye ujinga hawahitaji Usimamizi mkubwa. Wataufanya kwa kiwango kizuri na kikubwa utakachokipenda.
Makonda na uongozi wa Tanzania unajua wananchi wa Tanzania wakoje na wanataka nini.
Asije akakudanganya mtu kuwa watanzania wanataka Katiba mpya. Nop!
Asije akakudanganya mtu watanzania wanahitaji sijui Maendeleo, nop!
Hilo sio hitaji la msingi la Watanzania.
Watanzania wengi wanahitaji furaha, na furaha ya ni kusikia habari za udaku, uongouongo, habari mbaya za Watu wengine.
Ukiwa mzuri kwenye drama hapa Tanzania wewe ni Lulu na soko lako ni kubwa mno.
1. Ukiwa mwanasiasa jifanye unakoromea wanasiasa wenzako. Wachimbe mkwara hadharani na jifanye unaweza kuwaweka ndani la wasipofuata maelekezo yako
2. Jifanye unasakwa kwa udi na uvumba ili uuawe na ushategewa mitego, mabomu, na sumu ili uuawe kwaajili ya kutetea wananchi.
3. Jifanye unasikiliza matatizo ya Watu. Watanzania wengi wanapenda danganya Toto.
4. Sema upo tayari kwa lolote ikiwezekana kufa kwajili ya wananchi.
5. Vunja sheria na katiba ya nchi kisa kutatua mgogoro unaotokana na kuvunjwa kwa hizohizo sheria.
Watanzania wengi sio Watu wa kuheshimu utaratibu, kanuni na sheria.
Ukiwa mtu wa sheria na taratibu na kujifanya unafuata kanuni upo kwenye hatari ya kuchukiwa na watanzania wengi.
Watanzania wanachojali ni kusaidiwa matatizo yao bila kujali sheria imefuatwa au laah! Hii ni kutokana na tabia ya ubinafsi.
6. Ita viongozi wa dini jifanye ni marafiki zako.
Hii itakufanya watanzania wakuone wewe ni mtu mwema na mpenda Mungu. Jambo ambalo wewe mwenyewe unajijua sio kweli.
7. Penda kuwabughudhi wenye vipato ikiwemo wafanyabishara na hakikisha unawatolea maneno ya vitisho mbele ya kamera na wananchi.
Watanzania wengi hujisikia furaha pale wanapoona wale Watu waliowazidi wakibughudhiwa.
Kamwe ukiwa kiongozi kama unataka umaarufu na kupendwa na wananchi wa kitanzania waliowengi jiepushe kuwa karibu na wenye uwezo na vipato.
Wachezee watanzania kekundu, mchana upo nao alafu usiku wakienda kulala unaenda zako kwa wenye navyo.
8. Watanzania huamini maneno mabaya zaidi kuliko mazuri.
Ukitunga propaganda ya ubaya wa mtu hasa mwenye kipato ni rahisi kwa watanzania waliowengi kuipokea na kuiamini.
9. Usisahau, watanzania wengi yaani asilimia kubwa ni majizi na hawana shukran. Vyovyote utakavyo wasaidia elewa kuwa kama utakuwa unaishi kweli yale uyasemayo yaani Haki kwelikweli na ukawa maskini ndio watakao kuwa wakwanza kukucheka na kukubeza.
Hao wenye Akili ni wachache mno. Na hakuna tija kisiasa kuwa upande wa Watu wachache. Hivyo tumia mbinu kulingana na wingi wa wahusika katika eneo ulilopo.
Acha Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam