Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Ungeweza kuandika hoja zako bila kumsifiasifia huyo jamaa. Kwanza hana kabisa hizo sifa unazompa. Huyo ni jangili tu asiyefaa kabisa katika nafasi yoyote ya uongozi

How did you know kuwa ni jangili, do you have any hard facts or evidence to prove your claims ?
 
Maisha ya huyu kijana siku zote ni yale ya kumtegemea mtu wa juu. Hajawahi kuishi maisha ya peke yake.

Tangu anatoka kwao Kolomije, alifika mjini na kukishikisha kwenye familia ya marehemu Samweli Sitta, baadaye akaenda kwa marehemu Edward Lowasa, akahamia kwa kina Riz One, baadaye akamimbilia kwa JPM, na sasa yupo kwa Mama!

Huyu dogo mara zote hupenda kujishikisha sehemu ambayo itampa usalama wa kisiasa. Na akitoka kwa Mama ataangalia sehemu nyingine salama zaidi ya kujishikiza. Na hayo ndiyo maisha yake siku zote. Kiufupi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa huu mfumo wa kuishi maisha ya kinafiki na kujipendekeza kwa watu wa ngazi za juu ili kunufaika kisiasa na kiuchumi.
Alianzia Mwanza kwa Meya wa Jiji akitokea Kolomije
 
How did you know kuwa ni jangili, do you have any hard facts or evidence to prove your claims ?
Hizo facts zipo on public record wala sina sababu ya kuzirudia. Aliyemteua na Makonda mwenyewe wote wawili hawafai kuliongoza hili Taifa. Hawawezi kushinda nafasi yoyote ya uongozi kwenye uchaguzi wa huru na haki.
 
Hizo facts zipo on public record wala sina sababu ya kuzirudia. Aliyemteua na Makonda mwenyewe wote wawili hawafai kuliongoza hili Taifa. Hawawezi kushinda nafasi yoyote ya uongozi kwenye uchaguzi wa huru na haki.

Tumeshawapa tume huru. We hope mtapunguza maneno
 
Kwema Wakuu!

Usijeleta u-serious wako uwapo mbele ya Watanzania. Mambo ya akili mingi watanzania hawayataki, mambo ya kweli watanzania sio Wafuasi wake.

Ndio maana kijamii sio ajabu ukawakuta Watu kama kína Mwijaku, Dotto Magari, Piere Liquid, kina Mange Kimambi, na wengineo wakiwa na influence ndani ya jamii ya Tanzania.

Watanzania wanapenda udaku, habari za uongouongo na uzushi, habari za kufarakana na kufarakanisha, umbeaumbea. Habari za connections za video za ngono ndio watanzania wanazozipenda.

Habari za usimba na Uyanga, udiamond na ualikiba. Ndio mambo yenyewe hayo.

Niliwahi andika makala fulani miaka kadhaa nyuma kuwa úkitaka kutoka na kufanikiwa hapa Tanzania, Basi wekeza kwenye mambo ya ujingaujinga.

Watanzania wengi kwenye ujinga hawahitaji Usimamizi mkubwa. Wataufanya kwa kiwango kizuri na kikubwa utakachokipenda.

Makonda na uongozi wa Tanzania unajua wananchi wa Tanzania wakoje na wanataka nini.

Asije akakudanganya mtu kuwa watanzania wanataka Katiba mpya. Nop!
Asije akakudanganya mtu watanzania wanahitaji sijui Maendeleo, nop!
Hilo sio hitaji la msingi la Watanzania.

Watanzania wengi wanahitaji furaha, na furaha ya ni kusikia habari za udaku, uongouongo, habari mbaya za Watu wengine.

Ukiwa mzuri kwenye drama hapa Tanzania wewe ni Lulu na soko lako ni kubwa mno.

1. Ukiwa mwanasiasa jifanye unakoromea wanasiasa wenzako. Wachimbe mkwara hadharani na jifanye unaweza kuwaweka ndani la wasipofuata maelekezo yako

2. Jifanye unasakwa kwa udi na uvumba ili uuawe na ushategewa mitego, mabomu, na sumu ili uuawe kwaajili ya kutetea wananchi.

3. Jifanye unasikiliza matatizo ya Watu. Watanzania wengi wanapenda danganya Toto.

4. Sema upo tayari kwa lolote ikiwezekana kufa kwajili ya wananchi.

5. Vunja sheria na katiba ya nchi kisa kutatua mgogoro unaotokana na kuvunjwa kwa hizohizo sheria.
Watanzania wengi sio Watu wa kuheshimu utaratibu, kanuni na sheria.
Ukiwa mtu wa sheria na taratibu na kujifanya unafuata kanuni upo kwenye hatari ya kuchukiwa na watanzania wengi.
Watanzania wanachojali ni kusaidiwa matatizo yao bila kujali sheria imefuatwa au laah! Hii ni kutokana na tabia ya ubinafsi.

6. Ita viongozi wa dini jifanye ni marafiki zako.
Hii itakufanya watanzania wakuone wewe ni mtu mwema na mpenda Mungu. Jambo ambalo wewe mwenyewe unajijua sio kweli.

7. Penda kuwabughudhi wenye vipato ikiwemo wafanyabishara na hakikisha unawatolea maneno ya vitisho mbele ya kamera na wananchi.
Watanzania wengi hujisikia furaha pale wanapoona wale Watu waliowazidi wakibughudhiwa.

Kamwe ukiwa kiongozi kama unataka umaarufu na kupendwa na wananchi wa kitanzania waliowengi jiepushe kuwa karibu na wenye uwezo na vipato.

Wachezee watanzania kekundu, mchana upo nao alafu usiku wakienda kulala unaenda zako kwa wenye navyo.

8. Watanzania huamini maneno mabaya zaidi kuliko mazuri.
Ukitunga propaganda ya ubaya wa mtu hasa mwenye kipato ni rahisi kwa watanzania waliowengi kuipokea na kuiamini.

9. Usisahau, watanzania wengi yaani asilimia kubwa ni majizi na hawana shukran. Vyovyote utakavyo wasaidia elewa kuwa kama utakuwa unaishi kweli yale uyasemayo yaani Haki kwelikweli na ukawa maskini ndio watakao kuwa wakwanza kukucheka na kukubeza.

Hao wenye Akili ni wachache mno. Na hakuna tija kisiasa kuwa upande wa Watu wachache. Hivyo tumia mbinu kulingana na wingi wa wahusika katika eneo ulilopo.

Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
How old are you?
we are celebrating 40 years of the late Tz Prime Minister E.M Sokoine while we are very united and committed to transform Tz on next level of economic, social and political development :NoGodNo:

the emergence of very strong young leaders like Paul Christian Makonda, seems that, the sokoine legacy of hard working is living:pedroP:
 
Asilimia kubwa ya sisi Watanzania tunaoenda kujadili watu na matukio yasiohusiana na maisha yetu kabisa.

Nipo Rufiji kuangalia athari za "the so called mafuriko" kwenye mashamba yangu, watu wote tumebaki tunajadili msaada wa 50M wa Mchengerwa badala ya nini kifanyike ili kesho maafa haya yasijirudie.

CCM wametuweza kweli kwa kutupandikizia mfumo wa hovyo kabisa wa maisha wa"trending".
 
Back
Top Bottom