Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwa sasa taifa zima limeweka itikadi za kisiasa pembeni na kumwangalia Paul Makonda kama Kiongozi anayeweza kulivusha taifa kwenye hizi nyakati ngumu Sana

Mungu wa Mbinguni mtangulie Kijana huyu Paul Makonda awafikishe Watanzania Canan

Kwako Lucas 😂😂😂
"Wananchi wamebubujikwa na machozi waliposikia makonda kateuliwa kuwa mkuu wa mkoa Arusha"
 
Kwa sasa taifa zima limeweka itikadi za kisiasa pembeni na kumwangalia Paul Makonda kama Kiongozi anayeweza kulivusha taifa kwenye hizi nyakati ngumu Sana

Mungu wa Mbinguni mtangulie Kijana huyu Paul Makonda awafikishe Watanzania Canan

Kwako Lucas 😂😂😂
Umewahi kupima ugonjwa wa akili?
 
Makonda ni Mwamba kwelikweli. Wapinzani wakisikia jina lake tu wanabaki wanatetemeka kama wagonjwa wa homa kali.
 
MAKONDA AAINISHA MPANGO KAZI WA VIPENGELE SITA:
LETS MAKE ARUSHA GREAT AGAIN!


April 8, 2024
Arusha


⦁ Mapokezi yamenitia moyo wa kuwa mtumishi mwema na mtetezi wa wanyonge. Kamwe sitaungana na fisadi kukandamiza haki zenu, nitakuwa sauti yenu mpaka ukamilifu wa dahali

⦁ Nawashukuru kwa maombi. Kwa dua njema mlionifanyia. Nimekoswa koswa mara tatu kupoteza maisha, na nawaambia, sitakufa bali nitaishi. Niyasimulie matendo makuu ya Mungu.

Nina mambo au mawazo sita. Lakini lazima nifanye kwanza ziara mniambie, ili yale tunayowaza sisi yafanane na majibu ya changamoto zenu. Nakuja kwenye wilaya zote sita tukutane. Ili kusudi tupate sauti moja.

La Pili: Hakuna maendeleo bila umoja. Tukishikamana bila kujali dini, kabila, chama, tutapiga hatua. Mkoa usiwe wa malumbano ya kisiasa, bali mkoa wa kujenga uchumi imara, na wa biashara kwa watu wake.

⦁ Sijaja kukandamiza wanasiasa. Sijaja kutangua torati. Wapinzani mkitaka kunishirikisha mnishirikishe. Mkitaka hata mafuta kama tunaweza tutachangia.

Jambo la tatu, najua Arusha ni mji wa kitalii. Rais Samia ameipendelea Arusha, hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje aungane nanyi. Takwimu za serikali za sekta ya utalii zinatofautiana kati ya Maliasili, na RAS wa Mkoa, na Bodi ya Utalii. Unajiuliza, hawa watu si ni serikali moja ? Which means vyumba hakuna! Kumbi za mikutano hakuna. Tutajenga kumbi mbili kubwa za mikutano. Tutajenga apartment ya vyumba 400, na kiwanja cha mpira cha watu 30,000. Tuache siasa za kunyoosheana vidole, hazituingizii pesa.

Jambo la nne. Ninalo tangazo jema kwa yeyote anaedai haki yake: Kwa neema na mapenzi ya Mungu utaipata. Kama niko nimekanyaga mahali hapa, na nina kibali cha Rais, basi haki yako utaipata. Hujui kusoma, hujui kuongea ukaeleweka, huna hela, nitakulinda na kukupigania!

Jambo la tano. Watendaji na watumishi wote Arusha popote ulipo, funga mkanda! Mkurugenzi, RPC, Mkuu wa Idara, DC, Uhamiaji, kaa kwenye kiti chako ueneee. Habari ya kutumia madaraka kuwakandamiza wanyonge, kupendelea wenye pesa imefika mwisho. Kwenye idara yako kama huwakudumii wananchi, cha mtema kuni utakiona.

⦁ Arusha tembeeni kifua mbele. Ya Kwamba Mtaheshimika kwa utu wenu, sio pesa, elimu wala connection. Wanaosema niketolewa uenezi, nimeletwa u RC, sasa CCM nilikuwa nasema wafanye wengine, huku nafanya mwenyewe. Ofisi yeyote ukienda wakikuhudumia vibaya njoo kwangu. Hospitali ukijibiwa vibaya, Polisi wakikunyima dhamana, njoo kwanguuuu... Silogeki! Hofu iliondoka na kitovu waliponikata...

⦁ Jambo la sita: Kamishna wa ardhi NJOO HAPA! Una miezi mitatu kumaliza migogoro ya ardhi. Mnongoza kwa rushwa! Na msijioendekeze kwangu kwa kunipa kiwanja, Arusha viwanja ninavyo. Ardhi ni kilio namba moja...

⦁ Afisa Mipango Miji NJOO HAPA! Mnazalisha squatter! Hakuna mipango miji, mmeshuhudua inajengwa bypass lakini hamkwenda mkapanga na kupima viwanja kuwe na barabara zinazopitika. Mnashinda kule Bulka na Sanawali kwa sababu kuna rushwa. Sasa una miezi mitatu tutakuita utoe ripoti umekuta migogoro mingapi, umetatua mingapi, umekuta watu wangapi hawana hati, umetoa hati ngapi. Na, umejipangaje kuhakikisha migogoro mingine isitokee... Migogoro ya ardhi inasababishwa na nyinyi wataalam wa ardhi! Mtendaji, Mtumishi, usipojipanga tunakupanga!

⦁ Uhamiaji: Mtu ana nyaraka zote, kwa nini passport ichukue siku 14? Na foleni ya Namanga foleni masaa matatu. Natka iwe mwisho dakika 60!

⦁ Mabango kila mahali, mara masaji, mara dawa za kienjeji, hapana. Tunataka screens. Watu wanatushangaa.

⦁ Sisi ni matajiri kuliko wanaokuja kutuhurumia! Maji Arusha yanatoka matope, na kuna suala la bili kubambikizwa. Zinakuja kufungwa mita za pre-Paid.

⦁ Ndugu zanguni, mambo ni mengi. Tutakaa mtanambia mnataka RC wa aina gani lakini kamwe sitawasaliti. Maombi yenu ndio yananiweka hapa. Wajane, vijana, wazee wananambia endelea. Sitawaangusha. Sitalumbana na mtu. Mwenye wazo la kutengeneza ajira, mwenye wazo la kujenga uchumi, kuboresha Arusha, mlango uko wazi.

⦁ KIla anaekuja Arusha apokelewe na kikombe cha kahawa. Ni mji unaotupatia pesa nyingi sana, hatuwezi kuuacha bure. Lets make Arusha Great Again.

⦁ Najua Yapo mambo ya Stendi. Ya soko. Ya boda. Ya dala dala. Ya Tatu Mzuka. Ya bajaji. Ya Wadudu. Nipeni muda.

⦁ Tarehe 12 tutampokea Rais katika tukio kubwa la kumuenzi Hayati Sokoine aliyefanya kazi ya heshima katika taifa hili. Ndio maana mimi ni mchanganyiko wa mtoto wa masai, wa jeshi, wa kisukuma... Sieleweki kwa sababu Mungu amejaa ndani yangu. Nimechukua combination zote nzuri ndo maana pa kunyooka tunanyooka kweli kweli.


⦁ Nimeongea na RPC tunaenda kuongeza nguvu ya ulinzi Arusha, maduka hayafungwi saa 11, saa 12 mbili. Zinakuja camera, taa za kutosha, patrol za baskeli za polisi, pikipiki, rescue team, mpaka helicopter za patrol. Kuhakikisha mnalindwa barabara.

⦁ Mungu wangu na awabariki sana

WATU EEEEEEEEEEEEEEHHHHHHHHHHHHH!


View: https://youtu.be/ijwCgxv5seg

SHANGWE NA VIGEREGE, NA VIGEREGERE, NA VIGEREGEE NA VIGEREGERE NA VIGEREGEREEEEEEEEEEE

Sawa umeandika but of all people you think your makonda can change Arusha?? Never on earth!
 
Leo jumatatu ataje hao wafadhili wa Mange kwani weekend yote hii ameendelea kuporomosha matusi tena mazito mazito,siyo anatingisha tingisha sambwanda lake tu.
Na wewe unaangalia na kusemea mataka ya mwanaume? Aisee dunia inaenda kasi
 
Makonda ni Mwamba kwelikweli. Wapinzani wakisikia jina lake tu wanabaki wanatetemeka kama wagonjwa wa homa kali.
Umwamba wake unaujua wewe tu anapounguruma kichogoni kwako,maana aisifuye mvua imemnyeshea,kutwa kucha unasifia umwamba wa nyamitako hivi hujistukii kuwa unaofanya ni upuuzi
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda ametembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yaliyoathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha.

Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametembelea maeneo ya Sakina na Mianzini, maeneo ambayo yameathirika zaidi na mvua, kiasi kilichosababisha vifo vya watu 6 na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo,Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda amewataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua pamoja na kuhama katika maeneo yenye historia ya kuwa na mikondo ya maji.

Aidha Mh.Makonda pia amewataka viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha ikiwemo Maafisa wa mipangomiji kufanya vikao vya Dharura kwenye maeneo yao ili kupata Tathimini ya maeneo yao na hatari iliyopo kwenye makazi ya wananchi endapo Mvua zitaendelea kunyesha.

View attachment 2963974
View attachment 2963975View attachment 2963976View attachment 2963977View attachment 2963978View attachment 2963979

PIA, SOMA:

Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
Kuna mwaka niliwahi kushawishiwa na mdau wangu ninunue eneo niweke mjengo. Picha hii inanikumbusha eneo nililoonyeshwa Unga Limited. Roho ilisita na nawapa heko wote wanaoweza kuishi maeneo kama hayo hapo hata kama ni karibu na mjini kati. 🥴
 
Kwa sasa taifa zima limeweka itikadi za kisiasa pembeni na kumwangalia Paul Makonda kama Kiongozi anayeweza kulivusha taifa kwenye hizi nyakati ngumu Sana

Mungu wa Mbinguni mtangulie Kijana huyu Paul Makonda awafikishe Watanzania Canan

Kwako Lucas 😂😂😂
Hata hao wazao wa Ibrahim wenyewe walishaachana na hizo mambo za kumsubiri messiah wa kuwapeleka Kanan. Wanajipeleka wenyewe. Yaani wanaisaka njia wenyewe kwa teknolojia, jasho na damu tu huku wakipanga na kupangua viongozi wao kwenye boksi la kura kwa kadiri wanavyojisikia. Hizo porojo za "wazalendo" wamemuachia kiduku mwenye kazi ya kulinda legacy ya ukoo wa Kim.

Tumerudi nyuma sana!

Halafu John, tafuta darasa makini uelimishwe maana hasa ya "itikadi; ideology". Nimeanza kuamini kuwa inawezekana ikawa kweli kuwa na wewe una uelewa ziro kama ilivyo kwa watanzania wengi.
 
Kwa sasa taifa zima limeweka itikadi za kisiasa pembeni na kumwangalia Paul Makonda kama Kiongozi anayeweza kulivusha taifa kwenye hizi nyakati ngumu Sana

Mungu wa Mbinguni mtangulie Kijana huyu Paul Makonda awafikishe Watanzania Canan

Kwako Lucas 😂😂😂
Toa magufuli na makonda katika uzalendo. Wale ni wauaji sana
 
Kwa sasa taifa zima limeweka itikadi za kisiasa pembeni na kumwangalia Paul Makonda kama Kiongozi anayeweza kulivusha taifa kwenye hizi nyakati ngumu Sana

Mungu wa Mbinguni mtangulie Kijana huyu Paul Makonda awafikishe Watanzania Canan

Kwako Lucas 😂😂😂
Well said
 
Back
Top Bottom