Utendaji kazi wa Makonda unamfanya afuatiliwe sana na wananchi wote. Alipoteuliwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kuna watu walisema hataliweza hili jiji. Kampana hadi sasa hivi wote wanaokuja wanaonekana wanapwaya sana.
Kawekwa nje ya game kwa muda na kwa utulivu kabisa kakaa kimyaa hadi pale mwenye mamlaka alipoona anafaa kumsaidia kazi na kumuingiza kwenye team. Huko kapigaaa hadi wenye chama lao wakaanza kusema anaonyesha madhaifu badala ya kusifu yaliyofanyika.
Siasa ni ngumu sana. Fitina ikaingizwa, kachomolewa ile nafasi na kuwekwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Siyo mbaya. Arusha ina hadhi yake kubwa tu hapa TZ.
Maneno yakaanza kuwa haiwezi Arusha. Kuna wadudu. Akaanza na wadudu wenyewe na kuwaweka kwenye mstari. Ikiwa hamjui, watu kutoa udenda Dar ilikoma kipindi akiwa mkuu wa mkoa Dar. Siyo Vita ndogo. Ila alijiyahidi sana.
Makonda ni mtu wa kazi
Makonda ni mbunifu
Makonda anapenda haki.
Siyo rahisi kuwa kiongozi Afrika. Fitina ni nyingi mno. Mtu akijitaidi, basi na apewe maua yake.