Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewatangazia wakazi wa Dar Es Salaam na waliolikimbia jiji warudi ili siku ya Jumapili ijayo wajitokeze mitaani kupigana kelele kwa uwezo wao wote, hapa tukumbuke sheria ndogo za jiji zinakataza upigaji wa kelele, kwa wito wa Mkuu wa Mkoa inamaana sheria hiyo itasimamishwa kwa muda. Ili mtu aweze kupiga kelele itamlazimu kuivua barakoa yake, je, siku hiyo ndiyo rasmi ya kuivua barakoa jijini Dar es Salaam?
MUNGU KATENDA MUUJIZA.
Tena kila mmoja aende kwa RC akapewe kispika cha sumu ya panya ili kelele zisikike vyema!
 
Mtu mweusi akili yake anaijua mwenyewe,,,endeleeni kushabikia ujinga tu mkidhani corona imeisha,,,na mnaoshabikia wengi mnaishi mikoani. Ila dar,arusha hali ni mbaya sana kunatisha.
 
Aisee mkuu hata mimi nina mashaka,nahofia watu wasije kujiachia halafu ikatambaa kwa kasi.

Mtaa ninaokaa wamekufa watu watatu vifo vya ghafla wiki iliyopita,haijaeleweka nini kinewaua ndio maana bado naishi kwa mashaka.
Tutaona na kuyasikia mengi mwaka huu, tumeishinda corona wakati hatujui takwimu ziko vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatujaweka lockdown yes? But also hatupimi. So utajuaje kama hatuna cases za corona kama hatupimi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unataka serikali iwe inazurura mabarabarani kama wehu na kusema tukapime? Huo ni wehu. Wewe ni daktari au muuguzi unatafuta posho za kuzurura kupima?

Kinachotakiwa elimu na imetolewa kuwa ukiona dalili hizi wahi hospitali inatosha,mtu akiona dalili za corona aende hospitali au apige namba husika wenyewe waje kumbeba
 
hapa tukumbuke sheria ndogo za jiji zinakataza upigaji wa kelele, kwa wito wa Mkuu wa Mkoa inamaana sheria hiyo itasimamishwa kwa muda. Ili mtu aweze kupiga kelele
kelele zinaruhusiwa tu kwenye sherehe mfano kwenye mechi kelele zipo sanaaa,ngoma za midundiko mitaani zipo sanaa ,matarumbeta ya harusi kelele sana tu tunashangilia simba na yanga mitaani wakifunga sembuse kusherehekea send off ya corona

tutapiga kelele sana tu
 
.......Ndio maana kuna wawili siku hizi hawaachi kupiga kelele kila siku, wanaisema sana Chadema; kumbe mmeshawalipa, halafu mbaya zaidi wanawatumia mpaka waumini wao kwenye mambo yao binafsi.Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo likishakubaliwa na Askofu Shoo hakuna wa kupinga kwa upande wa dhehebu hilo!
 
7D983E88-E667-4617-AC28-14026F28F7BE.jpeg
 
Nasema hivi haturudiii ng'oo mpaka yule jamaa arudi!! yaani mpaka aje tena dar asiporudi na sisi haturudi sisi pia tunajipenda kuliko tunavyompenda yeye hata sisi tunakupenda kwetu.JAMANI ROMA EMBU WASIKIE NDUGU ZAKO ETI WANATAKA URUDI MJINI
 
Herd immunity. Hii project anayoifanya bwana mzee si nzuri ihivyo. 60% waugue ili 40% wapone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukizingatia weledi na uwezo wa kula vyakula stahiki vya kuimarisha afya kwa wengi wetu ulivyo duni sijui...
Wengi wanashangilia...!!!
Wameambiwa wapige kelele na vigeregere...
Tahadhari ni muhimu... za kuambiwa...
 
Sio siri kuna baadhi ya watanzania akili ni kiduchu kusema kweli!!.. mi nnachojua kauli ile imetolewa kwa watu waelewa na haimaanishi kwenda kupiga mikelele kama mwehu ama kupayuka tu..

Ukifanya hivyo basi jua wewe ni zero brain muda mwengine sio kila kauli mnaichukulia serious kiviile yatawashinda ndugu zangu..
 
Siku ya jumapili itakuwa siku ya send off party ya kuiaga corona Tanzania na kuifungisha virago forever iende kwa mumewe shetani

Makanisa mengi yatafanya hiyo ibada ya send off .Tunaomba kila mmoja ahudhurie ibada siku hiyo

Upatapo tangazo hili mtaarifa na mwingine tufike kwa wingi makanisani JUMAPILI HII ya tarehe 24 May 2020
Tukutane kwa gwajima!
 
Hivi unawezaje kumshinda adui yako bila kuwa na data? Mambo mengine sijui nisemeje! au tueleweje! sijui ni mizaha!
 
Mtu mweusi akili yake anaijua mwenyewe,,,endeleeni kushabikia ujinga tu mkidhani corona imeisha,,,na mnaoshabikia wengi mnaishi mikoani. Ila dar,arusha hali ni mbaya sana kunatisha.
Acha uongo wengi tuko dar nikiwemo mimi hiyo hali mbaya ilko wilaya gani eneo gani mtaa gani?
 
Back
Top Bottom