RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Shangilia huku ukitazama picha yake.Picha sio roho! Polisi ni wale wale
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shangilia huku ukitazama picha yake.Picha sio roho! Polisi ni wale wale
Hili ni funzo kuwa hawa wajinga wote wapo at risk ni swala la muda tu nani atachafukwa roho na kuwashusha kama ubuaMkatoliki, mseminari mpiga kinanda. Pole Emma. Mungu akupumzishe vizuri. Uliamka uko salama hujui nini kitatokea kazini kwako. Pole mdogo wangu.
Ni askari walioajiriwa kwa mtindo wa baba kanitumaYaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako...
Hii habari kama haijapikwa... basi kama ni kweli... ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia.... wadau wanasema kaacha dona kizembe sana....
Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia... any way RIP wazee, acheni tamaa...
Huyo aliekimbilia barabarani na silaha yake baada ya kujeruhiwa ina maana alishindwa hata kujaribu kutumia silaha yake?au risasi ilimtia wenge(najaribu kuwa tuu)any way mungu awapumzishe pahali pemaAnaandika Christopher Cyrilo.
___
PC Emanuel Keralyo Waitara. Amezaliwa 24/12/1991, Kabila Mkurya. Ni askari wa kikosi cha FFU aliyeuawa kwa kushambuliwa na Bw.Hamza kwa kushtukiza.
Kabla ya tukio hilo, Hamza alionekana maeneo ya ufukweni akiwa na mawazo sana. Hata watu waliomsalimia hakuwajibu, ni kama vile alikuwa kwenye dunia yake tofauti. Labda alishaona dunia si mahali salama tena kwake.
Punde, akatoka ufukweni na kurudi uelekeo wa barabara kuu ya Ali Hassan Mwinyi. Akafika kwenye kibanda cha polisi kilichokuwa pembeni ya barabara, akachomoa bastola yake ndogo kutoka kiunoni, akawapiga risasi askari wawili waliokuwemo. Askari mmoja alikufa papo hapo, mwingine alikimbia kuelekea baharini.
Hamza alimvua silaha askari aliyekufa na kuivaa shingoni. Kisha akamfuata askari aliyekimbilia baharini ambaye alikuwa ameishiwa nguvu kutokana na jeraha la risasi. Akampiga risasi nyingine kummalizia kisha akachukua bunduki yake. Hapo akawa na bunduki mbili alizopora baada ya kuwaua Polisi.
Hamza akarudi barabarani na kuanza kuwatafuta askari wengine ili awaue. Alifanikiwa kumuona askari wa barabarani (trafic), akiongoza magari eneo la makutano ya barabara karibu na ubalozi wa Ufaransa. Akamfyatulia risasi na kumuua. Akayapita magari binafsi na daladala za abiria akitafuta askari wengine.
Akamuona askari wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA, wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa. Yule askari akataka kukoki silaha kupambana na Hamza lakini akachelewa. Hamza akamuwahi, akampiga risasi na kumuua. Kisha akasogea eneo la ubalozini kupambana na askari wengine waliokuwepo. Lakini polisi wengine wakawa wamefika na katikati ya mapambano wakamuua.
Moja kati ya askari waliouawa na Hamza ni PC Emanuel Keralyo (pichani). Anatajwa kuwa mtu mwema asiye na shida na mtu. Anazungumzwa vizuri na askari wenzie hadi na jamaa waliosoma na kukua nae. Kijana mtulivu, mwenye kumheshimu kila mtu.
Zipo taarifa kuwa Hamza alidhulumiwa madini na askari. Lakini inadaiwa askari waliouawa sio wale waliomdhulumu. Kama ni hivyo, basi dhuluma ya askari wachache wasio waadilifu imegharimu maisha ya askari wasio na hatia. Mungu awapumzishe kwa amani.!View attachment 1909791
AK47 ni bunduki kubwa mkuu tena sana ila mtu wa kawaida tu anaweza kuitumia wala haina ugumu wowote, South Sudan wanatumia wachunga ng'ombe. Huyo Hamza amesomea Misri sio ajabu alipata mafunzo ya kutumia silaha huko ambayo kawaida nchi za wenzetu.Mimi. AK47 sio pisto kijana wala sio baruti za mlipuko AK47 ni kitu kingine mzee unless useme hufahamu chochote
Juzi chanel ten imetangaza mfanya biashara aliekamatwa na madini feki .polisi ni polisi
Akiwa anawapiga chadema huwa hana sura ya utu acha tushangilie tuWale mliokuwa mnashangilia vifo vya Askari waliouawa jana, mmoja huyo hapo angalieni picha yake wakati mnashangilia.
Akiingia barabarani kama Hamza mtamlaumu?JembeKillo, Mkuu jana wametoka kumpiga dereva wangu wa daladala hapo banana bila sababu, eti wana haraka kwanini anasabisha foleni, walivyojibiwa kuna ajali, kuna gar zimepigana pasi, ndo wanashangaa wakati wameshamuumiza mkono hadi umevimba balalaa na kidonda juu. Wanatumia nguvu nyingi, akili kidogo
polisi wasikie tu ukiingia angle zao utowateteapolisi ni polisi
Pole poti police leo wamekuwa wakuonewa?Hivi kuna justification gan ya kusema huyo jamaa alidhulumiwa na polisi? Na kama alidhulumiwa ndio ajichukulia sheria mkononi? Personally naamin yule jamaa ni jangiri tu wala sio muuza madin . Mnataka kuwaonea polisi bure
Mungu anasemwa itakuawa police?Tusiwasemee vibaya hawa Askari ni sehemu ya ndugu zetu
Every action is equal to opposite reaction police tulieniYeye ndiye wa kwanza kuumizwa hadi aue hao askari? Ingekuwa ni hivyo basi kila anayeumizwa angekuwa anaua na kungekuwa na mauaji kila siku. Hajafanya vizuri kuua hao askari wasiokuwa na hatia yeyote.
Hii ni chai aliyotuletea. Akili zisizo na cheti cha sekondari zinatambua hili. Askari amejeruhiwa anakimbia na silaha kujificha kisha anafuatwa kuuwawa na raia mmoja mwenye kitambi ambaye kabla ya hapo alimvua askari silaha na kwenda kuitumia? Hata kama askari ni untrained kiasi gani ila hayuko wa hiviYaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako...
Hii habari kama haijapikwa... basi kama ni kweli... ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia.... wadau wanasema kaacha dona kizembe sana....
Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia... any way RIP wazee, acheni tamaa...
Wabongo si kwamba hamuelewi ni dharau tu.Yaani mtu una silaha, umejeruhiwa unakimbilia ufukweni, huo muda anamvua askari mwingine silaha we unakimbia, anakufuata ulipokimbilia anakufyatulia risasi, anachukua tena silaha yako...
Hii habari kama haijapikwa... basi kama ni kweli... ni uzembe wa huyo askari aliyekimbia.... wadau wanasema kaacha dona kizembe sana....
Hizo nguvu za kukimbia ni bora angejihami, mbinu bora ya kujilinda ni kushambulia... any way RIP wazee, acheni tamaa...
Hakuna mwenye uwezo wa kumsema Mungu
[emoji23][emoji23][emoji23]So wameandika alichokisimulia yule maza aliyeenda baharini kujisaidia