Pele na Magoli yake 1,000

Pele na Magoli yake 1,000

Alikuwa anahesabia magoli yake hadi mechi za ndondo
Najaribu kuwaza:

Haya Magoli 1000 ambayo nimekua nikiyasikia toka midomoni mwa Kaka zetu, wajomba pengine wazee na vikongwe kuhusu Pele na Magoli yake 1000 ni Chai kongwe kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa soka ?

Huku ndiko yalipotoka Magoli msiyoyajua kukamilisha Idadi ya Goli Mbombo Goli Buku.

Goal Machine kahenya mno kufika alipofika Mana Kuna rundo la Sheria, mifumo ya kisayansi na manedeleo mengi ktk soka kuzidi Zama za Gwiji.

Swali: Goli Buku Gwiji kazitolea wapi ?
View attachment 3227230
 
Yaani Mkuu, mimi naamini kitendo cha Wazungu kumkubali Pele miaka ile ambayo ubaguzi dhidi ya watu weusi ulikuwa bado na nguvu,
Wwnakimbilia ubaguzi Kama hoja.
Wasahau waliompa tuzo Ni hao hao weupe ...Je walimpa tuzo kibaguzi dhidi ya weupe wenzao ?
 
Huyo Romario mwenyewe ana ugomvi na fifa kuhusu magoli yake, yeye anadai ana 1000+ wakati fifa wanasema ana 700+,
Kapigana till 41 na issue kubwa ilikuwa hiyo hiyo ya Pele.
Sio mjinga
Kigezo unachotumia kutambua ya mwingine kitumie kutambua ya kwake.
Hii favour inatokea wapi.
Au Romario mbaguzi ?
 
Ni kweli rekodi ya izo goli 1000 kwa maana ya video zake tunaweza tusiwe nazo kutokana na changamoto ya teknolojia wakati Pele anacheza mpira.

Lakini uyo mjomba alikua moto wa kuotea mbali. Nimeangalia marudio ya mechi zake nyingi sana. Sio highlights za magoli yaani mechi nzima. Pele alikua balaa.

Ingawa bado siamini kama kuna mchezaji wa mpira aliwahi kutokea mwenye kipaji cha kutoa burudani zaidi ya Ronaldinho, shida ndio alidumu kwa muda mfupi sana
 
Mie kwa kufunga, bican simkatalii, ila unadhani kwanini pele yupo kwenye mada ya nani mchezaji bora wa dunja kwa muda wote na bican hayupo, unaweza ukajiuliza na ukapata jibu.
Mzambia chitalu alifunga goli 100+ kwenye mwaka wa kalenda ya fifa, ila rekodi hii haitambuliki fifa wanaitambua ya messi,
We unaniambia muandishi wa habari, mie nakwambia rais wa fifa ndio alitoa certificate hito ya goli 1000

Katika hizo unazoita intercontinental matches, pele kawafunga kina madrid, kina inter, benfica na wengineo, pele huyo huyo katika mechi 14 za world cup ana double figures, ana goli 12 na assist 10, kina becknebuer, johan crujfy, yule superstar wa madrid aliyekipiga spain na Argentina, ewaaah, bwana alfredo di stefano, hao wote wanakwambia pele ni kiumbe kingine.
Odir Cuna ninHazina ya Santos usimdogoishe ni mtu wa kuheshimika na mmoja waliopigania Hadi hayo 448 yawekwe kwenye stats za pele.
Usimdogoishe mtunza data huyu.

Certificate wamempa why Ronaldo atambulioe ndio mwenye Magoli mengi ?

Au unafikiri Hawa wengine hawakucheza mechi za Aina hiyo ?

Kutambua na kuheshim mchango wake kwa kumpatia Cheti Ni kuelewa umuhimu wa Pele katika soka na Historia ya miamba ya soka kwa ujumla.

Kikubwa kinachomtenga na wenzie Ni Mafanioio ya National Team World Cup tournaments winner (3x) mbili akishiriki kikamilifu moja akichukua akiwa juu ya mbao Kama sijakosea.
 
Ni kweli rekodi ya izo goli 1000 kwa maana ya video zake tunaweza tusiwe nazo kutokana na changamoto ya teknolojia wakati Pele anacheza mpira.

Lakini uyo mjomba alikua moto wa kuotea mbali. Nimeangalia marudio ya mechi zake nyingi sana. Sio highlights za magoli yaani mechi nzima. Pele alikua balaa.

Ingawa bado siamini kama kuna mchezaji wa mpira aliwahi kutokea mwenye kipaji cha kutoa burudani zaidi ya Ronaldinho, shida ndio alidumu kwa muda mfupi sana
Hili halipingiki kuwa aliwatesa Sana kipindi hicho.
 
Kwa namba zozote mtakazompa bado pele ni balaa, nikikwambia uniletee goli hizo wanazosema hazifai kuhesabiwa utaweza? Pele kacheza game 10 hivi akiwa na timu ya jeshi na alifunga goli kati ya 10 mpaka 13 hivi, zitoe hizo..
Kuna mambo ukifuatilia utaona ni chuki tu na nongwa, mwaka 1969 anafunga goli la 1000 kwenye uwanja wa maracana vs vasco da gama, video ipo YouTube, pele alipewa cheti chenye saini ya raisi wa fifa akiwa mchezaji wa kwanza kufikisha hizo goli 1000, sasa tuseme bwana stanley rous aliyekuwa rais wa fifa wakati huo aliongopea ulimwengu?

Habari ni ndefu sana siwezi andika vyoote.

Kwa nyongeza tu pele ni mfungaji bora wa freekick namba 2 ama 3 nyuma ya fundi juninho pernambucano.
Katika game 14 za world cup kafunga goli 10 na ana assist 10,nitajie wachezaji mnao warate na pele mwenye jeuri ya kufanya hivi world cup.
Pele alikua ni habari nyingine ni mchezaji Bora wa muda wotee.. gifted
Kipaji Cha pekee Sanaa...watu walikua wa piga rafu Sanaa Ila jamaa alikua ni extraordinary kafanya makubwa Sanaa
NB.
Umenikumbusha misemo mbali mbali UTASIKIA UMECHEZA KAMA PELE IKIWA NA MAANA UMEFANYA JAMBO KWA USTAADI.

Enzi izo tunacheza ukitoa mpira nje langoni Kwako yaani Kona tatu ni penalty...yaani Kona mbili ya tatu ni penalty 😊
 
Kudanganywa kuhusu nini mkuu ni kwamba enzi za zamani watu walikuwa wanapigwa kiatu balaa, na ilikuwa ni vigumu sana mtu kumaliza msimu kwa kucheza mechi zote lazima baadhi uwe unauguza maumivu leo hii mtu akiguswa tu anakwenda chini imekuwa kama basket

Mkuu unajua mano amano.., kama wewe ni mkali kama Pele Kocha anakuwekea mtu anakuganda yaani hata ukitaka kwenda kunywa maji anakusubiri na hapo unapigwa viwiko vya kutosha..., Mkuu acha kabisa hawa jamaa walikuwa vitani na kipindi kile timu chache zilikuwa zinapanda kama leo kipindi kile defender anakusubiri huko umfuate ili akupige ndaruga....
Zama hizi mpira umekuwa na matakwa ya lazima mengi mno.
Sio kwa washambuliaj Wala viungo.
Pressing initiator striker,mild field outnumberd striker anatakiwa kujoin na makolokolo mengi tofauti na ile trun n shoot ya Zama zile mengine utajijua.
Kutoka attack attack attack now ni Attack Counter attack

Na mpira umechenji toka kukaba Hadi umkute mtu ndio ujione umekaba Hadi kuzuia eneo mpira unakaa na uelekeo wa adui mwisho kuficha njia.

Uhuni upo na utaendelea kuwepo
Huyo Messi tu fainali zote anazocheza anakandwa, Big matches anakandwa miguu rejea Copa America zote

Na lazima tuelewa Hakuna Rafi ndogo Mana kitu unachokiona kidogo katika soka kinaweza kumaliza career ya mtu
 
Hivi mnadhani mifumo na mbinu ndio zimeanza sasa au sio? Kwamba zamani kulikuwa hakuna mbinu ni wapo wapo tu, kwamba kila mtu ni mwendo wa 4-4-2 au sio? 🤣😂
 
Odir Cuna ninHazina ya Santos usimdogoishe ni mtu wa kuheshimika na mmoja waliopigania Hadi hayo 448 yawekwe kwenye stats za pele.
Usimdogoishe mtunza data huyu.

Certificate wamempa why Ronaldo atambulioe ndio mwenye Magoli mengi ?

Au unafikiri Hawa wengine hawakucheza mechi za Aina hiyo ?

Kutambua na kuheshim mchango wake kwa kumpatia Cheti Ni kuelewa umuhimu wa Pele katika soka na Historia ya miamba ya soka kwa ujumla.

Kikubwa kinachomtenga na wenzie Ni Mafanioio ya National Team World Cup tournaments winner (3x) mbili akishiriki kikamilifu moja akichukua akiwa juu ya mbao Kama sijakosea.
Umesoma vizuri, ila kuelewa ndio imekuwa changamoto, hakuna sehemu nimemdogosha bwana cuna, nimekuuliza ile certificate ya utambuzi wa magoli 1000 aliyopewa na rais wa FIFA unaionaje, kwako FIFA wana uzito gani, rais wa fifa ndio alikubali goli hizo 1000 na hiyo ni mwaka 69, miaka miwili mbele ndio anaondoka santos, 6 mbele ndio anakuja kustaafu,
Ujumbe wangu mkuu ni kuwa FIFA mwaka 69 walikubali kuwa pele kafunga goli 1000, miaka kadhaa mbele IFHSS na wenzao ndio wanakuja kuzikataa goli sio 1000.

Naona unataka kumdogosha kwenye world cup ni ukweli usiopingika world cup ya 62 aliumia hatua za awali mechi vs hungary ile kama sikosei, mwaka 66 aliumizwa tena, mbona walishindwa kubeba ndoo!?
Sawa ila chukua maradona, messi, jumlisha cristiano ronaldo, fanya na zidane kama kachumbari, na gaucho iwe chumvi
Alichokifanya world cup ni rekodi kali mechi 14 goli 12 assist 10,
World cup 1958 akiwa bwana mdogo wa umri lati ya miaka 17 mpaka 18 hivi, anafanya matusi, katika ile hat trick anafunga goli mbili za kideo, inapigwa krosi anaweka mali gambani, ndani ya box anampa mtu kidari, kisha anapachika wavuni 😂🤣
Mwaka 70 akiwa na miaka 30+ anaiongoza brazil kutandaza soka safi na kuchukua ndoo, na almanusura game vs Uruguay afunge goli la kideo, yale magoli ya magenious kina dennis berkgamp 🤣😂

Mwaka 74 ni yeye mwenyewe ndio aligoma kucheza world cup, na angecheza kuna hati hati brazil wangebeba lile kombe sijui mngekuwa mnasema nini leo.
 
Kapigana till 41 na issue kubwa ilikuwa hiyo hiyo ya Pele.
Sio mjinga
Kigezo unachotumia kutambua ya mwingine kitumie kutambua ya kwake.
Hii favour inatokea wapi.
Au Romario mbaguzi ?
Hapa unaniambia mimi au FIFA?
 
Zama hizi mpira umekuwa na matakwa ya lazima mengi mno.
Sio kwa washambuliaj Wala viungo.
Pressing initiator striker,mild field outnumberd striker anatakiwa kujoin na makolokolo mengi tofauti na ile trun n shoot ya Zama zile mengine utajijua.
Kutoka attack attack attack now ni Attack Counter attack
Hivi unajua historia ya formations na tactics haya mambo ya Total Football yameanza tangia enzi na enzi; kwahio unadhani counter attacts zimeanzia jana ? Kitu ambacho hakiwezi kubishiwa ni kwamba sasa hivi strickers wanalindwa na marefa sio kama zamani..., sasa kama hilo hulijuia huenda tunaongelea mpira wa kwenye x box au playstation
Na mpira umechenji toka kukaba Hadi umkute mtu ndio ujione umekaba Hadi kuzuia eneo mpira unakaa na uelekeo wa adui mwisho kuficha njia.
Kwahio ? ofcourse kama huwezi wala huruhisiwi kumpiga paranja mtu basi zone marking makes sense, lakini kipindi kile sio kwamba kulikuwa hakuna zonal marking bali na bado buti utapigwa.., tofauti kubwa ya sasa hadi mabeki inabidi wawe skilled sababu kazi yao sio kuzuia pekee bali ni part of attacking thus ndio maana nikasema madefender wa zamani wangepata shida sana kucheza leo lakini sio strikers, strikers wa sasa they have it easier
Uhuni upo na utaendelea kuwepo
Huyo Messi tu fainali zote anazocheza anakandwa, Big matches anakandwa miguu rejea Copa America zote

Na lazima tuelewa Hakuna Rafi ndogo Mana kitu unachokiona kidogo katika soka kinaweza kumaliza career ya mtu
Wewe unaongelea kukandwa ndio unaona hatari ?!!! Hivi unajua zamani kulikuwa hakuna straight red card ila ni watu kama Pele walivyokuwa wanapigwa kiatu ndio FIFA ikaamua ilete Red ?!!!! Sasa niambia mtu kama Pele amecheza kipindi ambacho hata Red hakuna, alafu ufananishe then and now ? Really !!!!
 
Kila nabii na zama zake..

Binafsi pele nimemfuatilia sana, video za youtube, video zake za full game, amini nakwambia huyu mzee alikuwa fundi mnoo.

Sheria za siku hizi zimepunguza ukali wa kuvunjana, watu walikuwa wanamrukia mitama ya hatari.
Tizama game yao vs Portugal world cup ya mwaka 66 kama sikosei, alipigwa viatu vya hatari, ikabidi awe anachezea mguu wa kushoto zaidi, ila baada ya game hii akasema hawezi cheza tena world cup, ndio mwaka 1970 fifa wakaanzisha red card katika kombe la dunia.
Viwanja havikuwa rafiki sana, viatu walivyokuwa wanavaa ni mazito sio kama ya sasa na bado alifanya kitu.
Game aliyofunga goli la 1000 ilikuwa kimbembe hapo uwanjani, game ilikiwa vs vasco da gama. Alikula viatu vya hatari, ilipigwa krosi inaelekea kwake kufunga, mtu akaona usinitanie, akajifunga, akawa anaend kufunga chuma ya buku mtu akamlamba mtama, ili kama ni penati iwe anaweza akakosa, hiyo yote kulinda heshima wao wasiwe kwenye rekodi ya kufumgwa goli la 1000

Respect kwa huyu legend.

Kwangu mimi.
Pele kisha messi wengine watafata.
Mipira ilitengenezwa kwakutumia Ngozi ya Ng'ombe, ilikua na weight yakutosha...Watoto hawezi kujua haya
 
Hivi mnadhani mifumo na mbinu ndio zimeanza sasa au sio? Kwamba zamani kulikuwa hakuna mbinu ni wapo wapo tu, kwamba kila mtu ni mwendo wa 4-4-2 au sio? 🤣😂
UMekimbilia kujibu ila hapo Nina uhakika hujapaelewa kabisaa.
Na lazima uelewe kwenye formation walikiwa wakienda na 4-2-4.
 
Total Football yameanza tangia enzi na enzi; kwahio unadhani counter attacts zimeanzia jana ? Kitu ambacho hakiwezi kubishiwa
Total Football ( Dutch Philosophy ) haikuwa ya kila mtu toka ianzishwe na Ajax 1970's Hadi kuwa ajenda ya Utaifa kwa Waholanzi.

Attack Attack Attack hii inazungumzia mtu anayejihusisaha na upande mmoja wa mchezo Yani jukumu lake ni kushambuoia tu.

Attack Counter Attack
Hii inazungumzia mtu anayejihusisaha na vipindi viwli vya mchezo Yan mkiwa nao na msipokua nao ( Shambulia Kaba Shambulia ).
Najua hapa ulipoteana chief.
Hivi unajua historia ya formations na tactics haya mambo ya Total Football yameanza tangia enzi na enzi; kwahio unadhani counter attacts zimeanzia jana ? Kitu ambacho hakiwezi kubishiwa ni kwamba sasa hivi strickers wanalindwa na marefa sio kama zamani..., sasa kama hilo hulijuia huenda tunaongelea mpira wa kwenye x box au playstation

Kwahio ? ofcourse kama huwezi wala huruhisiwi kumpiga paranja mtu basi zone marking makes sense, lakini kipindi kile sio kwamba kulikuwa hakuna zonal marking bali na bado buti utapigwa.., tofauti kubwa ya sasa hadi mabeki inabidi wawe skilled sababu kazi yao sio kuzuia pekee bali ni part of attacking thus ndio maana nikasema madefender wa zamani wangepata shida sana kucheza leo lakini sio strikers, strikers wa sasa they have it easier

Wewe unaongelea kukandwa ndio unaona hatari ?!!! Hivi unajua zamani kulikuwa hakuna straight red card ila ni watu kama Pele walivyokuwa wanapigwa kiatu ndio FIFA ikaamua ilete Red ?!!!! Sasa niambia mtu kama Pele amecheza kipindi ambacho hata Red hakuna, alafu ufananishe then and now ? Really !!!!
Unavyoandika ni Kama kwenye soka Ni Pele ndio amechezewa rafu peke yake.
Mpaka Sasa rafu zipo kadi zipo na Kuna watu hawapewi na wanawaumiza watu VAR inashuhudia mfano Romero wa Spurs WC alimpiga kiwiko lloris kipa wa France na Hakuna kadi.
Chief rafu zipo na zitaendelea kuwepo.
 
Umesoma vizuri, ila kuelewa ndio imekuwa changamoto, hakuna sehemu nimemdogosha bwana cuna, nimekuuliza ile certificate ya utambuzi wa magoli 1000 aliyopewa na rais wa FIFA unaionaje, kwako FIFA wana uzito gani, rais wa fifa ndio alikubali goli hizo 1000 na hiyo ni mwaka 69, miaka miwili mbele ndio anaondoka santos, 6 mbele ndio anakuja kustaafu,
Huwezi kuayongelea Magoli 1000 bila kumjumuisha Odir aliyelalama zile Mechi za kirafiki wazizingatie.

Rudi nyuma fuatilia kwanini Pele alituma barua ya Pongezi siku Messi anapovunja rekodi ya Goli nyingi ndani ya Klabu moja yaani kufikia kile alichokifa ya yeye ndani ya Santos then Anza kujudge kuhusu uzito wa FIFA.

FIFA hawajanyooka Kama wengine wanavyodai wabaguzi, wen uoendeleo na wafanya biashara na Mimi nimo kusema hawajanyooka na Sio wakuwaamini kwa kila kitu.
Rejea tuzo zao na kashafa zake.
 
UMekimbilia kujibu ila hapo Nina uhakika hujapaelewa kabisaa.
Na lazima uelewe kwenye formation walikiwa wakienda na 4-2-4.
World cup 70 italy alikuwa na mfumo gani!?
Mifumo imeanza toka kipindi hiko mzee.
 
Huwezi kuayongelea Magoli 1000 bila kumjumuisha Odir aliyelalama zile Mechi za kirafiki wazizingatie.

Rudi nyuma fuatilia kwanini Pele alituma barua ya Pongezi siku Messi anapovunja rekodi ya Goli nyingi ndani ya Klabu moja yaani kufikia kile alichokifa ya yeye ndani ya Santos then Anza kujudge kuhusu uzito wa FIFA.

FIFA hawajanyooka Kama wengine wanavyodai wabaguzi, wen uoendeleo na wafanya biashara na Mimi nimo kusema hawajanyooka na Sio wakuwaamini kwa kila kitu.
Rejea tuzo zao na kashafa zake.
Hapa tutakesha, haya umeshinda mkuu.
 
Back
Top Bottom