Pendekeza tozo nyingine Serikali ya Samia iichukue

Pendekeza tozo nyingine Serikali ya Samia iichukue

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Screenshot_20220819-062145_Chrome.jpg


Humu ndani tunaye Ndugu Waziri Mwigulu Nchemba, tutumie fursa ya uwepo wake kumkumbusha tozo zingine ambazo amezisahau. Ni kama akiziota usiku tu kesho anakuja nazo.

Mimi naanza na tozo ya ugali, ugali utoe kodi. Mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei za nafaka watu wengi sana watakula ugali. Piga idadi ya tonge mara idadi ya tonge kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi. Tonge likiwekwa kishimo liwe na tozo kubwa kidogo. Hapo serikali itapata bilioni 900. Tozo nyingine ya haraka haraka ni Simba na Yanga, kila tukifanya utani wa jadi kuwe na tozo.
 
Serikali ianzishe TOZO za:-
(a) Pumzi. Kila aliye hai alipe tozo hii.
(b) Usingizi. Kila alaye alipe tozo hii
(c) Ngono. Kila aliyebalehe alipe tozo hii
(d) Kuona. Kila mwenye macho alipe tozo hii.
(e) Kusikia. Kila mwenye masikio yanayofanya kazi alipe tozo hii.
(f) Shibe. Kila anayekula alipe tozo hii.

Stakayeshindwa kulipa tozo hizi ahamie Burundi.
 
hakuna cha bure katika ulkmwengu huu, lazima tulipe tozo kwa maendeleo yetu.
unadhani maendeleo yataletwa bila tozo?! thubutu!!! hata hao wanao pinga tozo wanalifahamu hilo, ila nia yao ni kuona Serikali inashindwa kuleta maendeleo ya wananchi.
 
Serikali ianzishe TOZO za:-
(a) Pumzi. Kila aliye hai alipe tozo hii.
(b) Usingizi. Kila alaye alipe tozo hii
(c) Ngono. Kila aliyebalehe alipe tozo hii
(d) Kuona. Kila mwenye macho alipe tozo hii.
(e) Kusikia. Kila mwenye masikio yanayofanya kazi alipe tozo hii.
(f) Shibe. Kila anayekula alipe tozo hii.

Stakayeshindwa kulipa tozo hizi ahamie Burundi.
Tozo ya kuona 👍🤣🤣
 
Kuwe na utaratibu wa mashabiki wa Yanga na Simba kuchangia 1000 kila will kwa serikali.Hivi hawa wachezaji wa kigeni wanaojazana Bongo wanalipa Kodi ipasavyo?Tusije tukawa tunlipa sisi walimu kwa Ela hii ya tembele lakini Mayele na Mzungu hawalipi.
 
View attachment 2327988

Tunaye Ndugu Waziri humu Mwigulu Nchemba. Tutumie fursa ya uwepo wake kumkumbusha Tozo zingine ambazo amezisahau. Ni kama akiziota usiku tu kesho anakuja nazo.
Mimi naanza na tozo ya ugali. Ugali utoe kodi. Mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei za nafaka watu wengi sana watakula ugali. Piga idadi ya tonge,mara idadi ya tonge kwa siku kwa wiki kwa mwezi. Tonge ikiwekwa kishimo iwe na tozo kubwa kidogo. Hapo serikali itapata bilioni 900.
Tozo nyingine ya haraka haraka ni Simba na Yanga. Kila tukifanya utani wa jadi kuwe na tozo.
Ipo siku atatamani kuifuta hiyo kauli lakini itakua amechelewa.
 
Katika waziri wa fedha wa hovyo kuwahi kutokea ni huyu, Mwigulu sijawahi kumwelewa Kila wizara anazopitia, Sijui Samia anamenelea nini, Shime Shime maamuzi yetu na Hasira yetu tuihifadhi tukaitumie kwenye sanduku la Kura 2025. Tuitoe lichama hili Madarakani akili iwakae sawa.
 
Back
Top Bottom