Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hakuna cha bure katika ulkmwengu huu, lazima tulipe tozo kwa maendeleo yetu.
unadhani maendeleo yataletwa bila tozo?! thubutu!!! hata hao wanao pinga tozo wanalifahamu hilo, ila nia yao ni kuona Serikali inashindwa kuleta maendeleo ya wananchi.
Kuna kiongozi mmoja 002 alipoambiwa kuwa Kuna pesa chache mtaani hivyo hakuna mzunguko.View attachment 2327988
Humu ndani tunaye Ndugu Waziri Mwigulu Nchemba, tutumie fursa ya uwepo wake kumkumbusha tozo zingine ambazo amezisahau. Ni kama akiziota usiku tu kesho anakuja nazo.
Mimi naanza na tozo ya ugali, ugali utoe kodi. Mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei za nafaka watu wengi sana watakula ugali. Piga idadi ya tonge mara idadi ya tonge kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi. Tonge likiwekwa kishimo liwe na tozo kubwa kidogo. Hapo serikali itapata bilioni 900. Tozo nyingine ya haraka haraka ni Simba na Yanga, kila tukifanya utani wa jadi kuwe na tozo.
Siko kibaruani na Wala sijawahi kuwa Chawa ila mimi ni raia mzalendo najua nini kinawasibu watu Vijijini..
Nyie mumerundikana huko Dar hakuna mnachojua zaidi ya mdomo.
Tulia bro. KaushaBefore tozo maendeleo yalikua yanaletwa na nini?
Tupia kapicha ka mapaka😃😃
Hapa watajenga mpaka vituo vya afya mwezini kwa pesa watakazopata.(c) Ngono. Kila aliyebalehe alipe tozo hii
Hizi ni hisia tuu ila in most cases pesa inatumika vizuri..Tatizo linapokuja ni pale ambapo utasikia pesa zimetumika vibaya au zimeibwa sijui bilioni ngapi huko hiyo ndo hukatisha zaidi watu tamaa kabisa, ingekuwa leo hii tupo kwenye hatua nzuri ya kiuchumi naamini hizi tozo watu wasingeongea sana, ubaya unakuja unakamuliwa tozo ila output inaonekana kwa darubini...UFISADI.
🤣🤣🤣Tupia kapicha ka mapaka😃😃
Hii tozo ya kuona unamaanisha vile wanaume tunaangalia makalio sio ?Serikali ianzishe TOZO za:-
(a) Pumzi. Kila aliye hai alipe tozo hii.
(b) Usingizi. Kila alaye alipe tozo hii
(c) Ngono. Kila aliyebalehe alipe tozo hii
(d) Kuona. Kila mwenye macho alipe tozo hii.
(e) Kusikia. Kila mwenye masikio yanayofanya kazi alipe tozo hii.
(f) Shibe. Kila anayekula alipe tozo hii.
Stakayeshindwa kulipa tozo hizi ahamie Burundi.
Ndiyo hivyo mjue kabisa kuwa walipa Kodi tunakata tamaa sometimes kwa kuona pesa za serikali zinatumiwa hovyo...value for money ipi hiyo?, ina maana siku zote hizo serikali haikuwa na hao watu, kwa kweli Kodi na tozo laiti Kama zingetumika vizuri tungekuwa na taifa zuri sana...Kama huyu raisi akifanikiwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji tutafika mbali ila Kama ni porojo zinazoongelewa hapa basi muda utakuwa ni mwalimu mzuri, napenda zaidi kutoa muda.Hizi ni hisia tuu ila in most cases pesa inatumika vizuri..
Hata hivyo Ili kukabiliana na hilo kwani hikuona maelfu ya ajira za Takukuru na Wakaguzi wa ndani Ili kusimamia value for money?
Ndiyo hivyo mjue kabisa kuwa walipa Kodi tunakata tamaa sometimes kwa kuona pesa za serikali zinatumiwa hovyo...value for money ipi hiyo?, ina maana siku zote hizo serikali haikuwa na hao watu, kwa kweli Kodi na tozo laiti Kama zingetumika vizuri tungekuwa na taifa zuri sana...Kama huyu raisi akifanikiwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji tutafika mbali ila Kama ni porojo zinazoongelewa hapa basi muda utakuwa ni mwalimu mzuri, napenda zaidi kutoa muda.