Kweli kabisa. Nchi hii tuna Almasi, Dhahabu, madini aina zote, Makaa ya mawe, Copper, Uranium, na mengine chungu nzima. Tumezungukwa na Maziwa makubwa ya Africa, Tuna Mito ya kutosha, ardhi yenye rutuba kubwa, vivutio vya utalii chungu nzima na vyenye kuongoza ulimweguni. Tuna Bandari zaidi ya 4.
Leo kila Mtanzania alitakiwa aishi katika nchi yake kwa raha na alitakiwa alipwe na Serikali kila mwezi kama benefits za mapato ya Mali ghafi zetu. Sisi sio watu wakukamuliwa na kulipishwa mikodi na mitozo. Serikali iwajibike kufanya kazi yake na kuhudumia wananchi. Sio yenyewe itake wananchi waihudumiye Seriali. Mpaka lini????
Ni nani anayenufaika na hizo tozo na kodi??? Kila kitu tunakopa, sasa tozo na kodi zinafanya kazi gani??? Hatuna uongozi bora huo ndiyo ukweli wenyewe. Tusidanganyane kabisa. Tokea uhuru hadi Leo ni miaka 60 na zaidi. Hivi tunaweza kujivunia kuwa tumeendelea??? Tutazame nchi kama Singapore, hawana chochote zaidi ya Bandari. Leo wako wapi?? Miaka 50 iliyopita sisi tulikuwa na uchumi mzuri kushinda wao, leo tazama wao wako wapi na sisi tuko wapi?? Tofauti ni sawa na Mbingu na Ardhi.