Pendekeza tozo nyingine Serikali ya Samia iichukue

Pendekeza tozo nyingine Serikali ya Samia iichukue

View attachment 2327988

Humu ndani tunaye Ndugu Waziri Mwigulu Nchemba, tutumie fursa ya uwepo wake kumkumbusha tozo zingine ambazo amezisahau. Ni kama akiziota usiku tu kesho anakuja nazo.

Mimi naanza na tozo ya ugali, ugali utoe kodi. Mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei za nafaka watu wengi sana watakula ugali. Piga idadi ya tonge mara idadi ya tonge kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi. Tonge likiwekwa kishimo liwe na tozo kubwa kidogo. Hapo serikali itapata bilioni 900. Tozo nyingine ya haraka haraka ni Simba na Yanga, kila tukifanya utani wa jadi kuwe na tozo.
Kuwepo na tozo ya chawa a.k.a viroboto maana kwa sasa limekuwa janga kwa taifa kila ukifanya uchawa unatozwa 100k
 
Na narudia tena.
Mheshimiwa SAMIA
tuondolee huyu Mwigulu,aliyelewa fedha zetu,na anayeona hwezi kufanywa chochote.
CCM tubadilike pia.
Kweli watz wengi ni vichwa matikit mwenye nchi hii ni Nan mwigulu au uyo mama yenu ujinga afanye yeye lawama atupiwe mwigulu kweli ebu tujaribu kutumia kidogo hata ubongo wetu acheni kufanya uyo bibi hausiki ye ndo mkuu wa serikali
 
Katika kitu ambacho nafurahia ni hizi tozo. Hadi leo nashindwa kuelewa kwa nn zilichelewa

Ukiona huwezi kulipaa, hama
 
Nyie mnadhan wale wabrazili wanasajiliwaje, mnajua mishahara yao, kocha wa SBS Bw. Hancy hela anayolipwa mnajua ? So tuvumiliane tu, no way tutalipa tu tozo
 
Kuwe na utaratibu wa mashabiki wa Yanga na Simba kuchangia 1000 kila will kwa serikali.Hivi hawa wachezaji wa kigeni wanaojazana Bongo wanalipa Kodi ipasavyo?Tusije tukawa tunlipa sisi walimu kwa Ela hii ya tembele lakini Mayele na Mzungu hawalipi.
😄😄😄Achana na Mayele na Mzungu,nchi itajengwa na wananchi wenyewe,wananchi Ni Mimi na wewe.
Tozo ni kwa MAENDELEO YETU.
 
Hii sio kauli ya kiongozi makini
 
Naombaa tulipe Tozo za kutumia barabaraa...!! Wakiona haitoshi watuueee
 
hakuna cha bure katika ulkmwengu huu, lazima tulipe tozo kwa maendeleo yetu.
unadhani maendeleo yataletwa bila tozo?! thubutu!!! hata hao wanao pinga tozo wanalifahamu hilo, ila nia yao ni kuona Serikali inashindwa kuleta maendeleo ya wananchi.
Acha mtizamo hasi weee, kukusanya mi tozo/kodi tu k wakati huna nidhamu kwenye matumizi haiwezi kukusaidia hata siku moja kuleta maendeleo, usione wazungu wamefika hapo ukafikiria ni wajinga, wao ni walipaji kodi wazuri sana lakini hiyo pesa inakwenda kutumika inavyotqkiwa hapi kwanini maendeleo yasionekane?!!hizi nchi za kiafrika karibia zote ni shida tu, mfano mzuri angalia kwenye bajeti zake, kila mwaka pesa inayotengwa kwenye miradi ya mandeleo ilivyokubwa kulinganisha na zile za matumizi ya kila leo, kama semina, warsha, hapo uje utegemee maendeleo gani?kila leo pesa zinapigwa tu wanaozipiga, ndio wafadhiri wa vyama vilivyoko madarakani!!
 
Watu hawana tatizo na kulipa kodi, tatizo lingine ni kuwa hizo kodi zinafanya nini ?

Yaani ukiacha vitu alivyofanya mwendazake, hawa wendawazimu wamefanya nini kwa matrilioni ya mikopo na hizo Tozo ?
Wanaweka mawe ya msingi na kufungua nchi na kukosa usingizi kwa kuwazia aina mpya ya tozo toka kwa wananchi! 😃😀🙌
 
Kweli watz wengi ni vichwa matikit mwenye nchi hii ni Nan mwigulu au uyo mama yenu ujinga afanye yeye lawama atupiwe mwigulu kweli ebu tujaribu kutumia kidogo hata ubongo wetu acheni kufanya uyo bibi hausiki ye ndo mkuu wa serikali
Soma kwa makini uelewe.
Acha papara zako.
 
Back
Top Bottom