View attachment 2327988
Humu ndani tunaye Ndugu Waziri
Mwigulu Nchemba, tutumie fursa ya uwepo wake kumkumbusha tozo zingine ambazo amezisahau. Ni kama akiziota usiku tu kesho anakuja nazo.
Mimi naanza na tozo ya ugali, ugali utoe kodi. Mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei za nafaka watu wengi sana watakula ugali. Piga idadi ya tonge mara idadi ya tonge kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi. Tonge likiwekwa kishimo liwe na tozo kubwa kidogo. Hapo serikali itapata bilioni 900. Tozo nyingine ya haraka haraka ni Simba na Yanga, kila tukifanya utani wa jadi kuwe na tozo.