Pendekezo la Kidiplomasia: Diamond Platnumz Apewe Pasi ya Kibalozi (kama hana)

Pendekezo la Kidiplomasia: Diamond Platnumz Apewe Pasi ya Kibalozi (kama hana)

Na. M. M. Mwanakijiji

Naomba kupendekeza kuwa huyu kijana apewe rasmi hati ya kusafiria ya Kibalozi (Diplomatic Passport). Nimekuwa nikifuatilia jinsi anavyoshirikiana na wasanii wengine ndani na nje ya nchi lakini pia jinsi gani anakubalika katika sehemu mbalimbali za Afrika. Nimefuatilia kwa karibu ziara yake inayoendelea huko Afrika ya Magharibi.

Ndugu zangu,

1. Hakuna Mtanzania ambaye si mtu wa serikali anayetangaza jina la Tanzania kama Diamond.

2. Kwa ndani ya miaka 10 hivi kijana huyo ameweza kutoka kuwa "the boy from Mbagala" to a "global phenom". Muda si mwingi, kijana huyu ataanza kupasua kwenye majukwaa makubwa ya nchi za Kimagharibi (siyo yale ya ukumbini tu). Kuna watu wenye majina ambao nao watataka kijana huyo awemo..

3. Kwa vile sasa ni mtu wa "kimataifa" Diamond aachane na haya malumbano ya kijiweni na siasa na "wadogo" zake. Ni lazia aanze kujionesha kuwa ni mtu wa namna yake.

Serikali itambue mchango wake - siyo tu katika kutoa ajira lakini pia katika uchumi. Hivyo:

1. Serikali impatie passport ya hadhi ya juu kabisa.
2. Anaposafiri nje ya nchi, Balozi zetu ziwe na taarifa na pale ambapo kuna balozi zetu basi anapoenda ni lazima apokelewe na kukutana na mabalozi wetu.
3. Apewe nafasi ya kubeba jumbe za kibalozi na hata kukutana na viongozi wa serikali huko anakokwenda na kubeba ujumbe kurudisha nyumbani.
4. Kwa jinsi anavyovutia vijana ni wakati makampuni ya Kitanzania (namaanisha hapa ya "Kitanzania" yashirikiane na serikali kumtumia Diamond katika kufungua biashara zao zaidi. Uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa tukijifungia ndani tu; ni lazima makampuni yetu yaanza kusambaa katika nchi za Kiafrika. Diamond kama jina na mjumbe anaweza sana kushawishi.
5. Ni vizuri kuhakikisha kuwa usalama wake anaposafiri. Hili watu wa serikali na kampuni ya Diamond wanahitaji kukaa chini kuona jinsi gani watahakikisha. Je, mnajua watu kama kina Jay Z, Beyonce, wanaposafiri kwenda nje ya nchi watu kama FBI wanajua na mara nyingi wanahusishwa kuhakikisha usalama wao?
6. Jeshi la Polisi lianzishe kitengo cha Ulinzi wa Watu Maalum (VIP Protection Unit) ambacho ni pembeni ya kile kinacholinda viongozi wa serikali. Kitengo hiki kitakuwa kinatoa ulinzi kwa watu wetu mashuhuri wanaposafiri nje ya nchi .. na kadhalika na kadhalika..

Ni mawazo mengine kem kem...
Mahaba niue
You are not serious!
What's happening??
Huyu mzinifu mdhalilishaji wanawake ndio apewe diplomatic passport??! you must be joking
Mkosa adabu
Hii ya woman abuser peke yake hastahili heshima
Anawatumia na kuwadhalilisha sana wanawake ( wengi watasema wanajipeleka lakini haimfutii yeye sifa mbaya 'abuser' period)
 
Asante lakini turudi nyuma kidogo na kujiuliza hivi sasa kati ya Samatta, Hasheem Thabeet na huyo kidudu chini wenu nani angalau anastahili kupewa huo ubalozi kwa kigezo mnachotumia cha kuitangaza Tanzania nje ya inchi? walikuwepo akina Balisidya waliopeperusha bendera nje ya mipaka ya Tanzania mpaka Japan, akina mzee Morris, Mzee Mwinamila, akina Hemedi Maneti na akina Jah Kimbute walitembea Afirika na huko juu walifika lakini hawakupewa VIP passport sembuse mcheza vigodoro? kama mna mapenzi na mahaba nae basi chagueni hoteli mkanywe nae chai
Sasa samatta na hashimu wana umaarufu gani wakumzidi diamond?
 
Mahaba niue
You are not serious!
What's happening??
Huyu mzinifu mdhalilishaji wanawake ndio apewe diplomatic passport??! you must be joking
Mkosa adabu
Hii ya woman abuser peke yake hastahili heshima
Anawatumia na kuwadhalilisha sana wanawake ( wengi watasema wanajipeleka lakini haimfutii yeye sifa mbaya 'abuser' period)
Ebu tuambie amewazalilishaje hao wanawake?
 
Hapana mkuu sijaielewa lete maelezo zaidi kivipi itamletea matatizo?
Pasi za kibalozi zina urasimu wake mkubwa sana kwenye kuomba viza.

Zina mchakato unaozishirikisha serikali zaidi.

Ukienda kuomba viza ubalozini kwa watu, wanakuchukulia kama kiongozi wa kiserikali, inabidi uwape taarifa maalum kwa muda muafaka, zishirikishe serikali, waandae kukupokea kama kiongozi wa serikali.

Pia, zinabeba wingu fulani la kijasusi. Ni kawaida majasusi wa kiserikali kupewa pasi za kibalozi. Hivyo mtu anayepewa pasi ya kibalozi bila ya kuwa na kazi ya kueleweka ya kiserikali anajiwekea wingu hili la kushukiwa kuwa jasusi.

Diamond kwa sasa anajulikana kiasi cha kwamba hiyo pasi haitamuongezea kitu, sana sana itamuongezea urasimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanganyika wanaheshimu mtu/kitu kutoka nje tu hasa kama ni Nigeria ila vya kwao wanaona takataka tu. Hii lazima wakatae ila hapo hapo waulize kuhusu Nigeria utasikia majibu yao. Nashangaa kama Nigeria inaishobokea TZ kiasi hiki.
 
Asee!Nahisi mimi ndo nazeeka kwa kasi sana!Diamond huyu huyu?Kwa muziki upi?
Ila hadi we Mzee unamkubali hivyo,nahisi kwangu sio uzee tu,huenda hata akili zangu zimevurugwa!
Sijawahi kuburudika vilivyo na Diamond,ninachokiona nyimbo zake zilikuwa zinabebwa sana na clouds kiasi kwamba ukilala Diamond,ukiamka Diamond hadi akili inalazimishwa kuzizoea!
Kwa maoni yako kwangu ni kali ya kufunga mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwahiyo wewe ndo kipimo cha kukubalika kwa Dayamondi?
 
Pasi za kibalozi zina urasimu wake mkubwa sana kwenye kuomba viza.

Zina mchakato unaozishirikisha serikali zaidi.

Ukienda kuomba viza ubalozini kwa watu, wanakuchukulia kama kiongozi wa kiserikali, inabidi uwape taarifa maalum kwa muda muafaka, zishirikishe serikali, waandae kukupokea kama kiongozi wa serikali.

Pia, zinabeba wingu fulani la kijasusi. Ni kawaida majasusi wa kiserikali kupewa pasi za kibalozi. Hivyo mtu anayepewa pasi ya kibalozi bila ya kuwa na kazi ya kueleweka ya kiserikali anajiwekea wingu hili la kushukiwa kuwa jasusi.

Diamond kwa sasa anajulikana kiasi cha kwamba hiyo pasi haitamuongezea kitu, sana sana itamuongezea urasimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo nimekuelewa mkuu Asante.
 
Ngada aka BWIMBI limepungua mtaani kwasasa,mkimkbidhi hiyo Passport ya Diplomat unataka MATEJA waongezeke? Unajua Diplomatic Immunity?
 
Mahaba niue
You are not serious!
What's happening??
Huyu mzinifu mdhalilishaji wanawake ndio apewe diplomatic passport??! you must be joking
Mkosa adabu
Hii ya woman abuser peke yake hastahili heshima
Anawatumia na kuwadhalilisha sana wanawake ( wengi watasema wanajipeleka lakini haimfutii yeye sifa mbaya 'abuser' period)
Wanaharakati wenye hisia kali mmepata pakusemea
 
Pasi za kibalozi zina urasimu wake mkubwa sana kwenye kuomba viza.

Zina mchakato unaozishirikisha serikali zaidi.

Ukienda kuomba viza ubalozini kwa watu, wanakuchukulia kama kiongozi wa kiserikali, inabidi uwape taarifa maalum kwa muda muafaka, zishirikishe serikali, waandae kukupokea kama kiongozi wa serikali.

Pia, zinabeba wingu fulani la kijasusi. Ni kawaida majasusi wa kiserikali kupewa pasi za kibalozi. Hivyo mtu anayepewa pasi ya kibalozi bila ya kuwa na kazi ya kueleweka ya kiserikali anajiwekea wingu hili la kushukiwa kuwa jasusi.

Diamond kwa sasa anajulikana kiasi cha kwamba hiyo pasi haitamuongezea kitu, sana sana itamuongezea urasimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bi Sandra akiisoma hii amueleweshe mwanae pia.
 
Angekuwa anapiga muziki na kuutangaza wa kitanzania ningeunga mkono. Muziki anaopiga ni wa kuungaunga kutoka vyanzo mbali mbali. Tuna mambo muhimu ya kufanya na si huu ujinga. Hizo diplomatic passport wapewe watu wenye kufanya vitu vya maana na siyo zitolewe kama pipi.
Ila ndio anatangaza taifa kuliko boya yeyote unayemuheshimu wenyewe wanamuitaga Tanzanian artist
 
Diamond hana originality. Siwezi kumkubali mtu mwenye dragon style ku copy and paste. Kwa Watanzania wengi wanaweza kuona ni kiboko lakini kwa wanaojuwa muziki hasa hawawezi kumuweka Diamond katika level hiyo unayoona wewe awepo. Let him come up with his own style and bits na zikubalike atleast continentally ndio tutaweza kum regard that highly. You are way over rating the dude. To me, Remi Ongala, Zengekala, na Mwinshehe were far superior to the dude.

Having said all that, he is doing the best he can under the circumstances! If Africa was a human body, then TZ would be an a*ss.
Afrika ndio ishamkubali na dunia ya muziki inatambua uwepo wake we endelea kukaza tu tukatae au tukubali that kid is representing us kuliko mtu yeyote tumpe support tu
 
Mzee naona unazeeka kwa kasi. Unajua vigezo vya hiyo Diplomatic Passport? Sio njugu zile kwamba kila mtu anaweza pewa.

Unafikiri kwa nini Samata, Hashim Thabit, n.k hawajapewa hiyo pasi?

Unforgetable
Hivi hao ulowataja unawafananisha na diamond kwa lipi... Au sababu wapo kwa wazungu
 
Naunga mkono hoja... anaibeba nchi maelfu wameipenda Tanzania kupitia yeye, maelfu wameijua Tanzania na kukipenda kiswahili kupitia yeye.
 
Back
Top Bottom