SiliconValley
Member
- Oct 17, 2018
- 56
- 59
Ni mawazo mazuri ila ktk serikali isiyo na mipango endelevu. Ni sawa na kile tulichofanya ktk mashindano ha afcon, au tunavyo mpa sapoti dhaifu Samatta, na pia tumemsahau H. Thabit. Tazama bunge lilisafiri kwenda Misri kushangilia kabumbu, bila kujua mikakati ipi ilitumika kufika huko, mpaka sasa Taifa halijui Samatta kafika vipi Genks, wala nchi Haijui H.Thabit yuko wapi, na hakuna anaejua Hassan Mwakinyo katoka Chimbo gani?????? sasa kurukia na kumpa Diamond Vipaumbele ulivyosema ni sawa na mshabiki asiengalia move ya mpira ila anasubiri goli lifungwe ashangilie. Kabla yakushauri ningependa uishauri serikali ni jinsi gani inaweza kuifanya sector ya michezo na sanaa ikawa kama ya USA, badala ya kuwatumia wasanii kwenye campaign tu,Je Serikali ya Marekani inakusanya kodi kiasi gani toka ktk sanaa na michezo, Je? Ni kwa nini sisi hatukusanyi, jibu ni fupi sana, sector hizo zote hapa kwetu sio Revenue channel, hivo ni kama sector ya ufugaji, ishauri nchi yako iwekeze kwenye mipango, mipango itaibua watu, na mipango italeta vyote ulivoshauri, wamarekani wana mipango ndiyo maana leo unaweza kutazama ktk mtandao na kujua acount ya Bank ya Jay Zee, P Diddy, Drake, Shakira nk wana kiasi gani benk cha fedha, je wewe unajua Diamond ana kiasi gani bank. Hujui kwa kuwa hiyo sector hapa nchini ni kama uwindaji haramu tu. Namaliza kwa kusema to live without a plan is plan to fail, and our nation has fail on this matter.