Pendekezo: Majina ya viongozi yaondolewe miradi ya umma

Tumekubaliana, ni miaka kumikumi tu! fanya, acha kumbukumbu, sepa. Usifute kumbukumbu za wenzako, weka za kwako
 
Na wale walikuwa wamefurika uwanjani siku ya msiba wake ni mbu siyo watu?.Kwani wewe usipomkubali JPM basi ni lazima na watu wote wasimkubali!
Unaweza kukuta watu wengi wamehudhuria msiba wa ndugu yako ukadhani wanampenda , kumbe wengine wamekuja kuthibitisha kama kafa kweli
 
Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa Majina yao kwenye Mali na miradi ya Nchi, Hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.

Kwa mfano, si sawa kwa Stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi luis , uwanja wa soka wa Taifa, Viwanja vya Ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa Majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa, hii ni kwa sababu Mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka Jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake, huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza Majina hayo na kwa mchakato upi?

Kusimamia Ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba Mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi, hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za Umma, Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya Maeneo ulipo mradi huo, mfano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, Daraja la Busisi, Barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi nk.

Lakini mali za umma kama Stendi ya Mbezi luis kuiita Jina la Mtu mmoja ni sawa na Ubaguzi uliojaa ubinafsi.

Napendekeza Stendi ya Mbezi iitwe STENDI YA MABASI YA MIKOANI YA MBEZI LUIS, Jambo hili linaweza kuondoa nuksi , laana na mikosi itokanayo na kutumia Jina la Mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe, Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam.

Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basini rahisi sana, Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui basi iitwe ofisi ya Magufuli Kisiwandui.

Naomba kuwasilisha.
Hakuna shida kamanda, huko ni kuwahenzi viongozi wetu waliopita.

Tuungana katika kukemea rushwa kamanda ambayo imekuwa ni adui wetu mkubwa wa maendeleo hapa nchi

Imefika sehemu ofisi za umma ndio zinakandamiza haki ya kupata elimu kwa mtoto wa kike hapa nchini.

Rejea tukio la huko Mbogwe Mkoani Geita, diwani wa kata ya Ikunguigazi alivyo shirikiana na mtendaji wa kata hiyo, kumdhulumu mtoto wa kike hasipate haki yake ya kupata elimu
 
Erythrocyte, wewe ni mwanamke na kamanda shupavu lakini hadi sasa nakushangaa umekuwa kimya utaki kuchangia mada inayohusu Mwl aliyempiga mimba huko Mbogwe Mkoani Geita na diwani na mtendaji wa kata kufunika kwa kula rushwa.

Vipi ukimya wako unaashiria nini, kwamba umekubali unyanyasaji kwa mtoto wa kike?
 
Viongozi wa Tanzania waliopo na waliopita wamepachika au wamepachikiwa Majina yao kwenye Mali na miradi ya Nchi, Hili jambo halina maana wala tija yoyote ile.

Kwa mfano, si sawa kwa Stendi ya mabasi ya kimataifa ya Mbezi luis , uwanja wa soka wa Taifa, Viwanja vya Ndege, madaraja, vivuko, shule, hospitali na mali nyingine za Taifa kupewa Majina ya viongozi, wawe hai au wamekufa, hii ni kwa sababu Mali za umma zimegharamiwa na kodi za wananchi, hivyo si haki kuweka Jina la kiongozi, eti kwa vile tu vitu hivyo vilijengwa wakati mhusika akiwa madarakani, wala hata hakutumia hela za mfukoni mwake, huku ni kukengeuka, halafu ni nani anayependekeza Majina hayo na kwa mchakato upi?

Kusimamia Ujenzi wa kitu chochote katika nchi haimaanishi kwamba Mhusika anayo hati miliki ya jina lake kupachikwa kwenye huo mradi, hii ni kwa vile pesa zilizotumika kujenga miradi ya nchi si zake binafsi, ni hela za Umma, Majina yanayopaswa kuitwa miradi hiyo yawe majina ya Maeneo ulipo mradi huo, mfano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, Daraja la Busisi, Barabara ya Mwendokasi, mradi wa umeme Kinyerezi nk.

Lakini mali za umma kama Stendi ya Mbezi luis kuiita Jina la Mtu mmoja ni sawa na Ubaguzi uliojaa ubinafsi.

Napendekeza Stendi ya Mbezi iitwe STENDI YA MABASI YA MIKOANI YA MBEZI LUIS, Jambo hili linaweza kuondoa nuksi , laana na mikosi itokanayo na kutumia Jina la Mtu mmoja tu tena ambaye hajawahi kuwa mkazi wa eneo hilo na wala hajawahi hata kupanda mabasi yenyewe, Uwanja wa Taifa wa soka urudishiwe jina lake la awali na jina la Nyerere liondolewe kwenye uwanja wa ndege, urudi kuwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam.

Kama tunataka kuwaenzi marehemu wetu au hata viongozi waliopo, basini rahisi sana, Majina yao yawekwe kwenye ofisi za vyama vyao, kwa mfano badala ya kuita ofisi ya chama Kisiwandui basi iitwe ofisi ya Magufuli Kisiwandui.

Naomba kuwasilisha.
Ushauri wako wa KIPUUZI UNAPUUZWA.

Maana unapoelekea utataka hata pesa ziondolewe picha za waasisi.

Chuki mbaya sana.
 
Duu! Gongola mboto, Musa Hasan(Msasani), Mwananyamala, Bibi Titi Mohamed road, Azikiwe avenue yote hayo ni majina ya watu.

Alli Hassan Mwinyi stadium .

Kazi ipo.

Mavufuli mwamba. Kila siku tunakukumbuka.
 
Huwa natamani sana kuwaheshimu watu ka Erythrocyte ila mada kama hizi ndio zinafanya nione dhahiri kwamba hata tukiamua kuwapa nchi watatuletea Ujinga kama huu
We una kiwango gani cha ufahami hapa duniani. Unafahamu angalau kwa ufupi yanayoendelea duniani? Amka usingizi kijana km shida bi kupungukiwa elimu rudi darasani elimu haina mwisho. Tanzania si kisiwa, pili Tanzania km nchi changa mambo mengi imejifunza na inaendele kujifunza kutoka nchi zilizoendelea. Huu ni mtindo wa dunia nzima inaoutumia kuenzi viongozi wake. Viongozi wa Africa wanafanya mkutano wao wa mwaka katika jengo la mwl. Nyerere lililoko mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Kinachokusumbua wewe ni kitu gani, roho ya wivu au chuki zisizo na sababu au roho ya uchawi maana kwangu mimi we si mtu wa kawaida. Tulia kijana jifunze dunia inavyoishi hata hicho chombo ulichotumia kutuletea hii message imetoka duniani huko. Tuishi dunia inavyoishi acha kupoteza muda wako kuwaza vitu vya hovyo ndiyo maana mnakuja kuumwa magonjwa ya ajabuajabu.
 
Erythrocyte, wewe ni mwanamke na kamanda shupavu lakini hadi sasa nakushangaa umekuwa kimya utaki kuchangia mada inayohusu Mwl aliyempiga mimba huko Mbogwe Mkoani Geita na diwani na mtendaji wa kata kufunika kwa kula rushwa.

Vipi ukimya wako unaashiria nini, kwamba umekubali unyanyasaji kwa mtoto wa kike?
Hiyo habari imeandikwa wapi ? kumbuka kwamba GEITA INAONGOZA KWA UKATILI DUNIANI , ikifuatiwa na Mogadishu , ya 3 ni Urusi
 
Tukimaliza haya tunakuja kwenye hela
Usimwamini mtu anayetumia kilevi hata kama ni babako,

Maana anaweza kuongea Yeye na POMBE ikaongea kumjibu au wote wawili, POMBE na MTU vikaongea Kwa pamoja ukashindwa kuelewa.
 
Back
Top Bottom