Pengine Unamsikia tu Shetani Juu juu. Humfahamu Vizuri na Unasema ni Adui Yako

Pengine Unamsikia tu Shetani Juu juu. Humfahamu Vizuri na Unasema ni Adui Yako

Kwa hilo andiko lako umepotosha japo sijasoma lote nimeishia pale uliposema eti shetani alikuwa kama "waziri mkuu kwenye serikali ya Mbinguni"

Mnamuongezea sifa za kijinga na kumpamba bila sababu. Hakuna sehemu kwenye Biblia inasema kuwa shetani alikuwa nani au "kiongozi wa malaika kama wengi wanavyoamini na kufundisha" hata kama sijasoma andiko lako lote naamini kwa sentensi hiyo hapo juu unamaanisha hivyo. Yeye alikuwa kerubi kama makerubi wengine mkuu na kusema ana mamlaka ndio maana alikaa na kupiga story na Yesu kule jangwani kwa simu 40 pia ni uongo. Biblia inaeleza Yesu alifunga siku 40 jangwani na aliposikia njaa yaani siku ya mwisho ndipo Ibilisi alikuja kumjaribu pitia chakula na sio kama alikuwa anapiga naye story hizo siku 40.

Infact, nje ya mada yako. Je unamjua mzee Sweya Makungu Mstaafu mmoja hivi kule Iringa?
Na Yesu alikuwa anamjibu kwa Nidhamu alafu ndio mwana wa Mungu huyo,,,Jamaa ni mkubwa na ana nguvu mnoo kudhidi fikra zetu wanadamu na uwezo wetu,,Kama alivyo Sir God,,na majamaa "nadhani ni washikaji mnoo sisi ndio tunawachonganisha"
 
Na rose mhando naye alitudanganya kwenye wimbo wake eti ya kuwa "Nanukuu!!Shetani Ana Mapembeee""
Hahahahahaha . Rose pmj na watu wengi wanamzungumzia shetani ktk muonekano wa Ulimwengu wa roho ambao hauwezekani kuonekana ktk Ulimwengu wa mwili.. Shetani na malaika zake au majini hawawezi kuja Kwny Ulimwengu wa mwili wakiwa na ile taswira yao ya Ulimwengu wa roho..


Ukisoma kitabu cha ufunuo shetani na Mungu wametumia namba 7 Kama alama zao za utisho ,nguvu , ukuu na ukamilifu kwa muonekano wao wa kiulimwengu wa roho... Ufunuo inasema Mungu ana roho 7 , Yesu ana pembe 7 na macho 7 vinavyowakilisha roho 7 za Mungu ..

Shetani pia ktk kitabu hicho kinaonesha ana vichwa 7 , pembe 10 na vilemba 7....


Hiyo ni taswira yao ktk Ulimwengu wa roho ambao mwanadamu hawezi kuuona ...
 
shetani anapenda madalaka sana.

Watu wanagombea URAIS huyu Lucifer huyu haya bana.
 

Attachments

  • b1aa63434161f222323011896ae463bf.jpg
    b1aa63434161f222323011896ae463bf.jpg
    67 KB · Views: 26
Mtu anakaa eti faya faya faya,,,,my freeendi unampiga faya malaika msitaafu ????? Akipigwa kimbola kidogo TU imeeenda
 
Wewe utakuwa apostle sio bure katika yote umeona sadaka tu. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
SIo.
Na sadaka ni sehemu ambayo hatuwez epuka. Kwamganga tunatoa mtu sasa kwa Mungu tunatoa nn mkuu.
Inawezekana kwakuwa najua sana nguvu ya sadaka. Sala/kuomba na kufunga ndo maana nikagusa hapo
 
Pengine unamsikia tu shetani juu juu, humfahamu vizuri na unasema ni adui yako.

Unawezaje kupambana na adui usiyeijua nguvu yake?

Anafafanua kwa ufupi Mwl . Makungu m.s
0743781910

Kamwe Usimfananishe shetani na majini , mapepo , mizimu wachawi n.k. Ambao una uwezo wa kufanya nao vita kirahisi tu hata kwa kuweka mfupa wa nguruwe mlangoni na harufu ya bangi ndani ya chumba..

Unapotaka kufanya vita na adui ili umshinde kwanza elewa uwezo wake na mifumo yake inavyofanya kazi..

Umewahi kujiuliza kwann majini na mapepo yalikuwa yakimuona Yesu yanahangaika,yanapiga kelele, yanagalagala, yananywea na kukimbia lkn shetani alikaa na Yesu wakapiga story, wakajadili vifungu vya biblia na kubishana kwa hoja kwa siku 40 nyikani? ( Soma Vitabu vya injili).

Umewahi kujiuliza iliwezekanaje shetani aliyepigwa pmj na jeshi lake kule mbinguni akafukuzwa akatupwa duniani, lkn wana wa Mungu (wako wengi siyo Yesu tu-ntakufafanulia ktk andiko lijalo) walipokuwa wanakwenda kujihudhurisha mbele za Mungu mara kadhaa siku tofauti tofauti shetani pia alikuwa anajumuika pamoja nao katkat yao mbele za Mungu na wale wana wa Mungu wala hawakumfukuza na Mungu alipomuona wakajadiliana naye juu ya mustakabari wa wanadamu duniani. (Soma kitabu cha Ayubu) .

Na unajua mwisho wa siku Mungu alimwambia nini shetani juu ya Ayubu? Alimruhusu shetani amfanyie mambo / mapigo yote anayotaka lkn kasoro jambo moja tu "asiitoe roho yake".
Hii maana yake nini? Mungu akikaa pembeni , Shetani ana uwezo wa kutoa roho ya mtu.
Kwahiyo wale ambao hata wakiona watu wamekufa kinyama kwenye ajali wanakimbilia kusema " kazi ya Mungu haina makosa . Ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu" , Jiepusheni kumsingizia Mungu Kila kitu . Kazi nyingine ni kazi za shetani zina makosa...

Shetani ni adui yako mkubwa unayepambana naye kwahiyo unatakiwa kumfahamu vizuri.

Shetani Kabla hajaasi mbinguni na kuwa shetani Alikuwa ni malaika mkuu anayeitwa jina zuri lenye utukufu Lucifer ( Nyota ya asubuhi) .

Alikuwa na uwezo mkubwa Sana wa ajabu kuzidi malaika wengine wote aliopewa na Mungu mwenyewe mpk akajiona Kama yupo sawa na Mungu . Na ndiyo maana robo tatu ya malaika ilimuamini na ikaamua kuungana naye kupigana na Mungu. Wakiamini Lucifer atashinda .

Wanadamu wanaimba mpk sauti ya 4 . Lkn unaambiwa Lucifer Alikuwa anaimba sauti mpk sauti ya 12 peke yake..

Akinyanyua mabawa yake akiyashusha zinalia sauti za vinanda tupu.

Alikuwa ndiyo kiumbe wa karibu Sana na Mungu kuliko malaika wengine . Maana yake Ni kuwa alimuelewa na kuielewa mipango mingi ya Mungu.

Aikuwa ni Kama waziri mkuu ktk serikali ya mbinguni . Kwahiyo Alikuwa na mamlaka makubwa ktk kuiendesha ile serikali ..
Na tafsiri nyingine Ni kuwa alielewa Siri nyingi za serikali ya mbinguni..

Mungu ni roho , shetani ni roho na malaika ni roho ( hawana umbo maalumu lkn wana uwezo wa kujiweka na kujigeuza ktk umbo lolote ..
Na mwanadamu wa kwanza kabisa kuumbwa aliumbwa ktk umbo la mwanadamu lkn lenye roho ya uungu (nusu Mungu) ndani yake.. Ndiyo maana Alikuwa na uwezo wa kakaa nao na kuzungumza nao wanyama na miti na wakaelewana..

Najua hujanielewa vizuri hapo . Ngoja nikupe hii.
Mungu aliumba vitu vyote kwa kutamka neno tu na kwa kutumia umoja , yaani " na liwepo anga ,likawa". Lakini ilipofika muda wa kumuumba mwanadamu Mungu hakutumia neno tu na aliongea kwa nafsi ya wingi.

Yaani " na tumfanye mtu kwa mfano wetu " .
Unajua Alikuwa anawaambia wakina Nani ?
Na huo mfano ni wa sura au jinsia pekee?
Na unajua kwann shetani alichukia kuumbwa mwanadamu?

- kwanza uelewe mwanadamu aliumbwa ile siku ya 6 ya uumbaji baada ya Mungu kuwa kaumba vitu vyote vya msingi kabakiza vichache. Ilikuwa Siku 1 kabla ya kupumzika . Na shetani alichukia kuumbwa mwanadamu . Hii maana yake ni kuwa wakati mwanadamu anaumbwa tayari mbinguni kulikuwa na viumbe tyr vimeshaumbwa ( malaika) na shetani (Lucifer) ndiyo alikuwa malaika mkuu . Soma Mwanzo sura ya 2 ..

"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu"..

-Mungu anasema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu". Siyo sura pekee yake au jinsia bali ni mtu mwenye nusu uungu na uwezo ndani yake Kama walivyo wao kule mbinguni. Ndiyo maana shetani alichukia maana Mungu alihamishia mapenzi kwa mwanadamu kuliko kwa malaika.

Nimegusia jinsia hapo juu. Biblia haijawahi kusema Kama Mungu ana jinsia . Lkn biblia inaweka wazi kuwa wana wa Mungu wana jinsia .. Tukianzia na Yesu . Na wale wana wa Mungu walioshuka duniani nyakati za Nuhu na wakavutiwa na binti za wanadamu na wakawaoa wakazaa nao ,wakazaliwa watu wenye uwezo wa ajabu ,hodari na majitu (Giants) wanefili.. (soma Mwanzo 6:1> )... Japokuwa ktk jambo hili la kitheolojia kuna nadharia 2 zinapingana na Kila mmoja ameachwa aamini nadharia anayoitaka yeye.. Wapo wanaoamini wana wa Mungu walioshuka na kuzaa na wanadamu zama hizo walikuwa ni malaika toka mbinguni.. Na wapo wanaoamini wana wa Mungu hao walikuwa ni watoto wa uzao wa Sethi wacha Mungu wa Kipindi kile .. Biblia haijafafanua kwa uwazi tofauti ya wana wa Mungu waliotajwa ktk Ayubu na hawa waliotajwa nyakati za Nuhu.
Swali la kujiuliza na kujiongeza Ni kuwa " kwann baada ya wana wa Mungu hawa kuzaa na wanadamu walizaliwa binadamu wenye sifa na uwezo mkubwa tofauti na binadamu wa kawaida"?

Shetani anaijua vizuri biblia kuliko unavyoijua wewe . Ndiyo maana Alikuwa anabishana na Yesu kwa vifungu. Na anaitumia Kila siku ili apate njia za kukupoteza wewe kwa kutumia hiyo hiyo biblia.
Kwahiyo kama unadhani unaweza kumtisha shetani kwa kuishika biblia au rozali au msalaba bila kuwepo na roho ya Mungu pembeni yako unajidanganya.

- Huwa tunayatoa mapepo na majini ndani ya mtu na wakati mwingine yanajitaja Hadi majina ( makata,subiani,maimuna,n.k) . Lkn Ulishawahi kusikia tumemtoa shetani ndani ya mwili wa mtu na akajitaja na jina kuwa mm ni Lucifer?

Sisi watu wa Tanga na Zanzibar kuna wakati Huwa tunakutana na majini tunayaona live . Lkn nani aliishawahi kukutana na Lucifer?

- Mungu anamwambia Musa " hakuna mwanadamu atakayeniona akaishi" .
Pengine hii ni sababu ya pili iliyomfanya Musa afe mapema .. baada ya Musa kung'ang'ania Sana kutaka kumuona Mungu sura yake , Mungu alimziba Musa macho na alipopita akamuachia Musa akamuona kisogo na mgongo..

Shetani naye huiga Kila kitu kinachoendeshwa ktk ufalme wa Mungu . Kwahiyo huwezi kumuona Lucifer wewe na imani yako ndogo hiyo.

Shetani na malaika zake pamoja na kumuasi Mungu ,walipigwa kule mbinguni lakini hawakuuliwa. Zingatia neno " hawakuuliwa" . Wakatupwa duniani .
Tena Biblia inasema " Ole ole kwa wanadamu maana yule mshitaki wenu ametupwa kwenu " .. Na ukumbuke ana hasira za kupigwa.
- Mwanadamu alipomuasi Mungu Kipindi cha Nuhu akafutwa na gharika . Kipindi cha sodoma akafutwa na moto .. Lkn shetani hakuuliwa alitupwa kwetu .

Huyo ndiyo adui unayeshindana naye wewe.. Umjue jinsi alivyo . Sijui km unanielewa..

Shetani alipotupwa duniani hakuna sehemu Biblia inasema kuwa aliondolewa au kunyang'anywa zile nguvu zake na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao mbinguni kuliko malaika wote .. Uwezo uliomfanya yeye ajione ni Kama Mungu .
Sasa fikiria huyo ndiyo kiumbe unashindana naye wewe ..

Ndugu yangu bila uwepo wa roho ya Mungu ndani yako na pembeni yako , utamchukia shetani tu lkn hutaweza hata kuligusa tu pindo la vazi lake . Tena siyo wewe utakayeshughulika naye ,ni Mungu mwenyewe.

Shetani anapenda ukuu, utukufu , na kuabudiwa km Mungu anavyoabudiwa.

Shetani Anapenda usafi , harufu nzuri za pafyumu, marashi ,udi , uvumba, manemane na marhamu . Kama vile tu Mungu anavyopenda . ( Soma torati ya Musa). Ndiyo maana majini yananukia kupita kiasi..

Anapenda damu na nyama kupita kiasi kuliko sadaka yoyote ile . Kama vile tu Mungu alivyokuwa anapenda Kabla ya kifo cha Yesu . ( Soma Agano la kale uone jinsi Mungu alivyokuwa anapenda damu na harufu nzuri ya nyama ya kuchoma km sadaka ) . Mungu aliacha ila shetani ameendeleza . Unajua kwann ? Damu huwa inaongeza nguvu na uwezo kwa viumbe vilivyo ktk ulimwengu wa roho. Kawaulize wachawi wanapotaka kuboost nguvu zao wanafanya nn..

Hakuna kiumbe kinachomfikia shetani kwa uzuri wa sura anapokuwa ktk umbile la kimwili.. unawakumbuka wale malaika walioenda kwa lutu kule sodoma na gomora jinsi walivyokuwa wanawavutia wale wajinga wa sodoma wenye ushetani ? Basi Lucifer kabla hajawa shetani ndiyo alikuwaga kiongozi wao kule mbinguni na hakuna malaika Aliyekuwa anamzidi kwa lolote.
Huwa tunafanya makosa Sana kumchora shetani na sura ya kutisha kiasi kwamba watoto wanakariri hivyo na inakuwa rahisi kuanguka ktk dhambi ya uzinzi maana wanakutana na sura nzuri nzuri tu bila kujua kuwa hao ndiyo vibaraka wa Shetani wapo kazini ..

Shetani anao uwezo wa kufanya miujiza ya kumponya mtu ( soma ufunuo atagundua mengi) ..
Ndiyo maana leo hii yapo baadhi ya makanisa yanayotilia mashaka ktk miujiza wanayofanya.
Kama unalijua neno la Mungu unawagundua kirahisi.

Shetani anao uwezo wa kumtoa mtu mapepo /majini. Pitia habari za beerizebuli ktk injili utagundua hilo..
kwahiyo usidanganywe na miujiza ya mtu , mpime huyo mtu kwanza.

Shetani anao uwezo wa kumpa mtu mafanikio . Na hilo linajionesha wazi kabisa ktk mahojiano yake na Yesu kule nyikani..
Kwahiyo usitamani mafanikio ya mtu bila kujua kayatoa wapi?

Shetani anao uwezo mkubwa wa ubunifu wa kisayansi na kiteknolojia. Na wanadamu wengi tunaingia kwny mitego ya shetani anayetumia akili nyingi kwa ujanja sana..
Ndani humo humo ya teknolojia nzuri tu kunakuwa na kajambo kadogo tu ka kishetani ndani yake.. Anachotaka ni kuona watu wanafanya kinyume na maagizo ya Mungu anavyotaka. Na kwa kuwa watu wengi hawasomi maandiko basi hawajui iwapasavyo kuenenda na wanapotea..

Tawala nyingi, mamlaka na falme za duniani zipo chini ya/ zinaendeshwa na shetani Lucifer. Rejea maagizo ya shetani kwa Yesu kule nyikani. Shetani huzishikilia tawala za dunia ili maamuzi yanayopitishwa na tawala hizo yawe ni ya kumkufuru Mungu na kumtukuza yeye. Ndiyo maana leo Kuna mambo km ya haki za ndoa za jinsia moja . Soma vizuri habari za mnyama ktk kitabu cha Ufunuo utaelewa.

Huyo ndiyo shetani Lucifer tunayedhani tunapambana naye direct kumbe tunapambana na vibaraka wake tu ..

ANGALIZO MUHIMU
Andiko hili halijaandikwa ili kumsifia shetani ,bali kuelezea ukweli halisi wa Shetani ( Lucifer) ili kukufanya ndugu mpendwa kujua nguvu ya adui unayepambana naye .
Ukiijua nguvu na uwezo na mbinu zake utajua jinsi ya kumkwepa/ kupambana naye..
Na usipambane na shetani bali mkwepe au muite Mungu apambane naye kwaajili yako.. Wewe Huna uwezo wa kupambana na Lucifer peke yako..

Makungu m.s
0743781910
Wewe jamaa hakika umenena. Huwa nawaona wakristo hasa wenye makanisa ya msisimko, wanampa uzito mdogo sana shetani, kuliko uhalisia.

Fikiria Ile vita kule MBINGUNI, Mungu alishindwa kumuua shetani kupitia majeshi yake. Japokuwa shetani MBINGUNI hakuwa mwanajeshi, alikuwa muimbaji tu. Fikiria Mwanajeshi anaenda vitani na mwimbaji lakini nguvu zinatoshana.

Angalia pia Shetani ambavyo amekupa akitibua mipango ya Mungu, Kila mpango wa Mungu ametibua. Siyo Mchezo.

Mwamba Shetani siyo Lele mama.
 
Je uwepo wake, tunaweza kuthibitisha kisayansi?
Ulimwengu wa roho unafanya kazi kinyume na asili aliyoumbiwa mwanadamu na sayansi . Uwepo wake hauthibitishwi kisayansi sawa na ambavyo uwepo wa Mungu hauthibitishwi kwa sayansi. Uwepo wake unathibitishwa kwa njia kiroho kwa wanaotumia nguvu zake. Au kwa matokeo yanayotokana na nguvu zake tunayoweza kuyaona..
 
Back
Top Bottom