Kutokuwa na katiba ni tofauti na kuwa na katiba mbovu. Na siyo kwamba hawana katiba. Kwani katiba ni kitu gani zaidi ya muongozo? Unataka kuniambia hawana muongozo?Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Hakika.Maana niliuliza hapa mtu akivunja katiba nini kinafuata?Hakuna aliyejibu.Kama iliyopo tu inavunjwa na ni kawaida wala anayevunja hashtuki,hata ikiwekwa katiba gani haitasaidia kitu.Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Uko sahihi kabisa.Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,
Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake
Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza
"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Soma vizuri na uelewe....Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Uingereza wanayo katiba sema haijaandikwa acha kudanganya watu hapaPengo yuko sahihi hata uingereza kipaumbele chao sio katiba na hawajawahi kuwa na katiba na hawatarijii kuwa na katiba. kipaumbele ni kero halisia za raia wake kutatuliwa. Askofu pengo yuko sahihi asilimia 100
UK wana values na customs ambazo kwazo ndio muongozo labda tuanze kujadili aina za katiba otherwise funga domo lako usidanganye hapaHiyo unwritten constitution koko yako iweke basi. Katiba isiyoandikwa ilipitishwa lini weka mwaka ilipopitishwa na bunge la uingereza na kupigiwa kura na wananchi. Weka hapa huo ushahidi