Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo nae ni mwananchi wa Tanzania, ana uhuru wa kutoa maoni
Angesimama kama yeye siyo kukaa mbele ya press na kuanza kupayukwa kwamba yaliyosemwa sio msimamo wa Kanisa Catholic,keshajiona Askofu wa taifa sasa na hana mamlaka ya kutusemea waamini wote Tanzania awasemee wa Dar anaowaongoza
 
Zipo seminary nyingi za kikatoliki zinaitwa st Mary.. mf ile ya hapo mbalizi mbeya inaitwa st mary mbalizi... kuna moja iko hapo pwani inaitwa st. Mary's pia au maarufu kama Visiga seminary
Fatilia vizuri ujue mmiliki wa hiyo st.Mary ya Mbeya na hiyo ya pwani utajua kua hizo shule hazina muunganiko na kanisa Katoliki. Hizo mkurugenzi wake ni Mchungaji Mama Rwakatare.
 
Rais akitaka kuongea na Papa anawasiliana na Balozi wa Vatican hapa Tanzania,sio Pengo
Sio kweli balozi wa Papa hawezi mwaproach direct lazima apitie kwa pengo kiprotocol sababu akienda direct balozi wa Papa atampelekea kardinali aone pengo anasemaje Kama askofu wa magufuli jimbo la dar es salama magufuli lazima apitie kwa pengo kwanza hawezi enda ubalozi wa Vatican straight
 
Bwana mdogo fala ni wewe unaocopy gazeti zima na kulileta humu.

Askofu Pengo ni bosi wa jimbo kuu la Dar, anayo haki ya kuongea kama kardinali na anaitumia.

Anayo haki ya kusema kuwa askofu wa Rulenge hayupo right kwenye hoja zake. Muwe mnaelewa mantiki zima ya maongezi ya mtu kabla ya kuanzisha mijadala isiyo na mashiko.
Askofu Pengo na Askofu Rulenge wana hadhi sawa.

Ukadinari hata Padre anaweza kuteuliwa kuwa kadinari. Kajambe mbele huko.

Adui wa mtu mweusi ni mweusi mwenzake! Hizi picha zinaonyesha weusi walilazimika kuvuliwa nguo katika mgodi wa Mwadui ili tu wakaguliwe kama hawajaiba Madini ya almasi! Aliyekuwa anawakagua ni weusi wenzao! Walipofanya kazi weusi wenzao walikuwa nyuma kulinda wasiibe! Ilikuwa ukiingia mgodini bila ruhusa ni faini kubwa sana au kupoteza maisha! Picha zote hizi zimepigwa mwaka 1951 huko katika mgodi wa Mwadui! Watu weusi wanavyotendeana ni jambo la khatari!

FB_IMG_1507473386768.jpg
FB_IMG_1507473398289.jpg
FB_IMG_1507473409356.jpg
 
Huyo hata asipofukuzwa umri wake na mawazo yanaonyesha amefikia mwisho

Badala atende haki kumalizia safari yeye ndio kwanza anafanya kinyume chake

Hata hivyo huyu ni Mfarisayo tu hivyo usishangae anacho kitetea

Fikra zake Pengo kwa sasa hivi hazina tofauti na za Moses Kulola. Wote wanatia aibu. Wanazeeka vibaya bila shaka.
 
Nakupongeza kwa uliyoyaandika. Na nakupa hapa nyongeza:

1. Kwa waliosoma walau classical philosophy, Pengo is INSTRINSICALLY EVIL. Hiyo yatosha kumwelezea alivyo.
2. Askofu Niwemugizi ana mamlaka kamili na timilifu ndani ya Jimbo la Rulenge. Ana haki na wajibu wa kulisemea jimbo la Rulenge. Anakuwa summoned na Papa peke yake.
3. Pengo ni mkuu wa jimbo la Dar es Salaam peke yake. SIO mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania.
4. Pengo wala sio Rais wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania ambaye ndiye "msemaji" wa kanisa la Tanzania.

Niwape mfano... Pengo amewatenga wanamaombi...lakini hao wanamaombi wakiwa nje ya Dar es Salaam ni waamini halali katika majimbo mengine.
Huyo uliemtaja unamsifia kwasababu anawaunga mkono kwenyesiasa zenu? Siku moja atakapowakosoa mtaanza kumsema vibaya. Waacheni wachungaji wafanye yao ninyi mbaki na siasa zenu za ajabu.
 
Fala wewe soma hapa.

HIVI karibuni, gazeti la Daily News (ISSN 0856-3812, No. 11,152) katika ukurasa wake wa mbele liliandika hivi, (.."in D'Salaam, the Head of Roman Catholic Church in Tanzania, Polycarp Cardinal Pengo, trumped wisdom for personal gratification and welfare of the nation at large"..).

Jioni Machi 14, 2014, nilimsikiliza Januari Makamba akitoa mchango wake wa maoni kwenye Bunge la Katiba. Wakati anahitimisha, alituasa tuheshimu maoni ya viongozi wa dini waliopendekeza Serikali mbili, akiwemo Polycarp Kardinali Pengo.

Hii ilikuwa wiki moja baada Samuel Sitta kuwatembelea Polycarp Kardinali Pengo pamoja na Mufti wa Tanzania, Issa Shaaban Simba.

Kwa asiyeujua muundo wa Kanisa Katoliki, ikitangazwa kwamba Samuel Sitta katoka kwa Mufti kisha amekwenda kwa Polycarp Kardinali Pengo, ni rahisi kudhani ilikuwa ni ziara ya kuwatembelea viongozi wa dini wa ngazi ya kitaifa.

Hata mimi utotoni nilikumbatia dhana kwamba, Laurean Kardinali Rugambwa ndiye aliyekuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, kwani aliwapa daraja maaskofu 26, wakati Polycarp Kardinali Pengo amekwishawapa maaskofu 24.

Nilipokumbatia dhana ya pili kwamba Mkuu Kanisa nchini ni Rais wa Baraza la Maaskofu, nikajiona nimetumia hoja ya kisomi zaidi!

Nilipoanza kusoma nyaraka rasmi za kanisa, hasa Sheria za Kanisa ziitwazo "Code of Canon Laws", ndipo nikagundua sikuwa na ukweli wowote katika zile dhana mbili.

Hizi "Canon Laws" ibara zake hutajwa hivi, Can. 381, zinatosha kumwelewesha yeyote muundo wa Kanisa Katoliki. Zinataja mamlaka ya askofu, askofu-mkuu, kardinali, rais wa baraza la maaskofu na zaidi.

Hakuna ibara inayoonyesha kwamba kuna "mkuu wa kanisa", au "msemaji wa kanisa" katika nchi yoyote.

Kinyume chake, sheria ya kanisa, Can. 381(1) na Can. 391(1), zinasema kwamba askofu jimboni, ndiye mkuu na mwenye madaraka jimboni.

Ibara hii inatokana agizo la mkutano wa maaskofu uitwao Vatican II, uliotoa hati iitwayo "Lumen Gentium" ibara ya 27, isemayo kwamba, askofu jimboni ni mwakilishi wa Yesu na si mwakilishi wa Papa au chombo chochote.

Vilevile, hakuna andiko la kanisa linalotaja maneno "makao makuu". Badala yake jengo la kanisa liitwalo "Cathedral" ndilo lenye mamlaka ya uaskofu.

Kwa wale wanaopenda neno "makao makuu", basi afadhali waseme "Cathedral" ndiyo "makao makuu" ya kanisa jimboni.

Pale Roma, "Cathedral" ni kanisa liitwalo "St. Lateran's archbasilica". Kumbe, makao "makuu ya Kanisa Katoliki duniani", siyo anakoishi Papa yaani kule Castle Gandolfo au pale Vatican, bali ni hapo "St. Lateran archbasilica".

Hata kanisa maarufu lililopo Vatican, yaani "St. Peter's basilica", lina hadhi ndogo iitwayo "basilica", wakati hili la "makao makuu" linaitwa "arch-basilica", hadhi kubwa kuliko makanisa yote Katoliki duniani.

Ibara ya 390 na 436(3) ya sheria za kanisa, zinamkataza askofu (bishop) pamoja na askofu-mkuu (arch-bishop) wasiendeshe misa kwenye "Cathedral" bila ruhusa ya askofu mwenye jimbo.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo au askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, hawawezi kuendesha misa kwenye "Cathedral" ya Ifakara, bila kwanza kuruhusiwa na askofu Salutaris Libena.

Pia, kwa kutumia sheria, Can. 763, askofu wa jimbo, mfano pale Ifakara, amepewa mamlaka na Papa kumpiga marufuku askofu yeyote duniani asihutubie lolote jimboni Ifakara ikihitajika kufanya hivyo.

Mwaka 2004, Joachim Kardinali Meisner, alitumia ibara hii kumkataza askofu Jacques Gaillot asiingie jimboni Cologne, kwani alikwishachokwa kuigawa nchi kwa kauli zake alizoziita "ni maoni yake binafsi".

Nimechagua ibara hizi chache kuonyesha mamlaka ya askofu, uone kwamba, hakuna askofu hata mmoja nchini aliye juu ya mwingine.

Sasa tuone ukardinali ni nini?

Mkatoliki akitaka utumishi wake utambulike rasmi kikanisa, lazima atasajiliwa au kusimikwa kwenye kundi linalotambulika. Mara nyingi huwa ni jimboni au kwenye jumuiya ziitwazo "religious".

Zamani kila aliyesimikwa hivyo aliitwa "kardinali". Lakini kuanzia karne ya tisa, neno "kardinali" lilibaki kutumika tu kwa walioitwa na Papa wakahamia na kusimikwa upya Roma.

Padri aliyehamishiwa Roma, huko alisimikwa kwenye kanisa lililoitwa "titular church". Hiyo ikawa aina ya kwanza ya makardinali, wakijulikana kama "cardinal-Priest".

Baadaye mashemasi nao wakawa wanahamishiwa Roma, huko wakapewa vituo vilivyoitwa "deaconia". Ikawa aina ya pili ya makardinali waitwao "Cardinal-Deacon".

Kazi za Papa zilipoongezeka, akahitaji msaada wa maaskofu kutoka majimbo jirani yaliyoitwa "Suburbicarian Diocese". Hali ya maaskofu hawa kuwa karibu na kuhitajiwa Roma, kukawafanya waitwe "Cardinal-Bishop".

Hizi ndizo aina tatu za makardinali. Zipo hadi leo, yaani "Cardinal-Deacon", "Cardinal-Priest" na "Cardinal-Bishop".

Kuanzia mwaka 1150, Papa alianza kuwaita makardinali kwenye vikao vya kumshauri, ambavyo hadi leo vinaitwa "Consistory".

Mwaka 1179, haki ya kumchagua Papa mpya, ikaacha kuwa ya wanajimbo wengine wa Roma, bali ikabaki kwa "makardinali" tu kwenye mkutano unaoitwa "Conclave". Mwaka 1975, Papa Paul VI alifupisha umri wa kardinali kuhudhuria "Conclave", yaani chini ya miaka 80.

Tumeona kwamba, kitendo cha kupewa ukardinali na Papa, ni uhamisho wa kwenda Roma. Uhamisho huo unamfanya awe mwanajimbo wa Roma, ambaye kama haishi Roma, basi kokote aliko duniani anafanya umisionari.

Ile aina ya "Cardinal-Bishops" bado hupewa lile kanisa liitwalo "Suburbicarian Diocese". Siku hizi "Cardinal-Deacons" hupewa hata yale makanisa, "titular church".

Ile aina ya "Cardinal-Priest", wengi hawaishi Roma kwa sababu ya umisionari wao mbali na Roma. Mmojawapo ni Polycarp Kardinali Pengo, anayeongoza Jimbo la Dar es Salaam, lililo kilomita 6043 kutoka Roma.

Je, mtu anapewa ukardinali baada ya kufikia ngazi ipi ya utumishi? Teodolfo Kardinali Mertel, alipewa ukardinali Machi 15, 1858 akiwa hajapata hata ushemasi. Machi 20, 1556 Reginald Kardinali Pole alikuwa ameshakuwa kardinali kwa miaka 20 na ameshashiriki "Conclave" tatu akiwa hajawa padri.

Kuanzia Februari 2, mwaka 1983, Papa John Paul II aliwapa ukardinali mapadri saba, waliobaki na upadri wao bila kuwa maaskofu.

Watano kati yao wameshafariki ambao ni Henri Kardinali de Lubac, Avery Kardinali Dulles, Aloys Kardinali Grillmeier, Joseph Kardinali Congar, Leo Kardinali Scheffczyk. Wawili kati yao wako hai, yaani Roberto Kardinali Tucci na Albert Kardinali Vanhoye.

Papa Benedict XVI, naye ana mapadri wanne aliowapa ukardinali bila kuwa maaskofu. Watatu wamekwishafariki, ambao ni Domenico Kardinali Bartolucci, Urbano Kardinali Navarrete, Umberto Kardinali Bett. Aliye hai ni Josef Kardinali Becker.

"Roman Curia" ni jopo linalomsaidia Papa kuendesha kanisa lote duniani. Karibu timu yote "Roman Curia" huripoti shughuli zake kwa "Secretariet of State".

Hivyo, "Secretariet of State" ana majukumu mazito ndani na nje ya Kanisa, kwani Papa anaweza kusifiwa au kulaumiwa ndani na nje ya kanisa kwa sababu tu ya utendaji wa huyu "Secretariet of State".

Nafasi hii ya "Secretariet of State" sasa inashikwa na Pietro Kardinali Parolin, aliyeachiwa na Tarcisio Kardinali Bertone.

Wote Kardinali Bertone na huyu Parolin ni maaskofu. Lakini mwaka 1848, nafasi hii ilisimamiwa vizuri na Giacomo Kardinali Antonelli, ambaye alikuwa shemasi tu hadi kifo chake Novemba 06, 1876.

Papa anaweza kumpa mtu ukardinali kwa siri, yaani "Cardinal in pectore". Serikali ya China ilipomfunga askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai, haigundua kwamba akiwa humo gerezani alipewa ukardinali kwa siri mnamo Juni 30, 1979.

Kardinali yeyote, kama alivyo Polycarp Pengo, siyo mwakilishi wa nchi kama Tanzania, kwani, hakuna jimbo wala parokia inayoitwa Tanzania.

Tumeona kwamba ukardinali ni kuwa mwanajimbo wa Roma au jirani na Roma (suburbcarian). Hivyo, hata inavyoelekeza sheria ya kanisa, Can. 357(1), kardinali ni mwakilishi wa parokia yake pale Roma yaani "titular chuch", ambayo ya Polycarp Pengo pale inaitwa Nostra Signora de La Salette.

Lakini ibara hiyo 357(1), bado inamdhibiti kardinali kwamba, hata hiyo parokia yake pale Roma, haruhusiwi kuiingilia kiutawala, kiuendeshaji au kinidhamu.

Hivyo, eneo pekee duniani ambako Polycarp Pengo ana mamlaka ya uchungaji, utawala, uendeshaji au nidhamu, ni ndani ya mipaka ya Dar es Salaam tu (rejea, Can. 381(1).

Wakati mabaraza ya maaskofu yanashamiri duniani, baadhi ya maaskofu waliitaadharisha Vatican kwamba, ama baraza zima au rais wa baraza hilo, ataweza kujikuta anaingilia ukuu wao jimboni na kugeuka kuwa mkuu nchini.

Hivyo, Papa aliiweka ibara ya 455(4) makusudi kulinda huo ukuu wa askofu wa jimboni, ili asiingiliwe kwa namna yoyote na baraza zima au rais wa baraza la maaskofu.

Hivyo, ibara hii inatosha kukuthibitishia kwamba, rais wa baraza la maaskofu, si kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, wala si mkuu wa maaskofu nchini.

Hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, naye eneo pekee la ukuu wake, ni mipaka ya Jimbo la Iringa tu.

Mkutano wa makardinali wote duniani na Papa yaani "consistory", hauna mamlaka ya kutoa tamko kisha liitwe kuwa ni la Kanisa Katoliki duniani. Huo ni mkutano wa askofu wa Roma na wanajimbo wake.

Wakati mkutano wa maaskofu wote duniani na Papa, ndicho chombo kikuu kupita vyote kiitwacho "magisterium", chenye mamlaka ya kuamua lolote ndani ya Kanisa Katoliki.

Ibara ya 1121 ya Katekism ya Kanisa Katoliki inasema, askofu haachi kuwa askofu hadi kifo chake, hata akijiuzulu madaraka.

Lakini ukardinali ni tofauti. Padri Louis Billot alikuwa kardinali kwa miaka 16 ,alipojiuzulu ukardinali Septemba 21, 1927, akaacha kuwa kardinali.

Hivyo, uaskofu ni nafasi ya juu zaidi na nyeti zaidi ndani ya Kanisa Katoliki, kuuzidi ukardinali.

Lakini, siku hizi, msemaji akishamtambulisha kardinali, anafuata askofu-mkuu, kisha askofu, baadaye mapadri na kuendelea, halafu mwishoni anasema "itifaki imezingatiwa"!

Tumeona kwamba "Secretariet of State" wa "Roman Curia", yaani Kardinali Antonelli, hata upadri hakuufikia. Tumeona, kwamba hata leo, wapo hai na wametajwa humu makardinali watatu ambao hata uaskofu hawajaufikia.

Pia, mifano mitatu ifuatayo nchini Albania, Switzerland na Italy, inakufahamisha kwamba Papa John Paul II, amewahi kufanya jimbo liwe na padri ambaye ni kardinali, wakati askofu wa jimbo hilo si kardinali.

Jimbo la Chur (Switzerland), halijawahi kuongozwa na askofu ambaye ni kardinali. Lakini padri Hans Urs von Balthasar wa humo, alitangazwa kwenye orodha ya makardinali Juni 28, 1988.

Mei 25, 1985, hayati askofu Antonio Mistrorigo wa Treviso (Italy), alishuhudia padri wake Pietro Pavan akipewa ukardinali wakati mwenyewe hakuwahi kuwa kardinali.

Novemba 26, 1994, hayati askofu Franco Illia wa Shkodre (Albania), alishuhudia padri wa jimbo lake yaani Mikel Koliqi akipewa ukardinali wakati yeye mwenyewe hakuwahi kuwa kardinali.

Kumbe, yaliyotokea Albania kwa Kardinali Koliqi, yanaweza kabisa kujirudia Tanzania, yaani padri wa jimbo moja tu nchini anakuwa kardinali, wakati hakuna askofu hata mmoja nchini aliye kardinali.

Hivi, ikitokea hivi, halafu huyo padri ambaye ni kardinali, akusanyike na maaskofu wote nchini ambao si makardinali, je, wapenzi wa ile "itifaki", wataizingatia vipi ile itifaki yao?

Ukitaka kuvijua "vyeo" ndani ya Kanisa Katoliki, sharti utulie na kuvisoma.Vinginevyo, unaweza kuhutubia tuheshimu mawazo ya mwenye "cheo" fulani, ukidhani ndiye mkuu hapa
Aiseeee aiseee mkuu atakaye pinga haya bhasi
 
Mkuu, msiwe kama mbumbumbu wa kisiasa, sio kila mtu awe na mawazo au fikra kama zenu.

Askofu Pengo kiumri ni mkubwa, lakini sio kigezo cha kugeuka kupelekeshwa na mawazo yote ya vijana ambao bado wanajiona wakamilifu kimawazo na kimaono.

Kustaafu atastaafu yeye mwenyewe lakini yupo sawa kabisa kwenye suala la kupinga mawazo ya askofu wa Rulenge.
Usijitie wazimu km wale wapuuzi wa vijijini wanaopita kudanganya walezi na ma house girl wa vijijini kuwa wao sijui ni master na ujinga mwingine. Wewe unayejidai una AKILI HUJUI KUWA PAPA BENECICT ALIJIUZULU? Unajua sababu aliyosema? Alikuwa honest enough kukiri afya yake kiakili haiwezi tena ongoza wakatoliki zaidi ya bilioni moja duniani. Sio kwamba alikuwa kachoka hivyo, yule mzee ni msomi vibaya, kachapisha vitabu vingi sana na alikuwa ndio engine ya ukatoliki kifikra, na alikuwa sharp mbaya ingawa alianza umwa umwa ila sio km hata pengo. Pengo ni mgonjwa kila angle. Pengo alichofanya ni kuthibitisha alichosema Gwajima.
 
Rais akitaka kuongea na Papa anawasiliana na Balozi wa Vatican hapa Tanzania,sio Pengo
Protocol Ya kanisa tofauti na secular magufuli lazima kwanza awasiliane na askofu wake pengo na pengo ndie apeleke kwa balozi wa Vatican
 
Jinga wewe, Askofu Pengo na Askofu Rulenge wana hadhi sawa.

Ukadinari hata Padre anaweza kuteuliwa kuwa kadinari. Kajambe mbele huko.

Adui wa mtu mweusi ni mweusi mwenzake! Hizi picha zinaonyesha weusi walilazimika kuvuliwa nguo katika mgodi wa Mwadui ili tu wakaguliwe kama hawajaiba Madini ya almasi! Aliyekuwa anawakagua ni weusi wenzao! Walipofanya kazi weusi wenzao walikuwa nyuma kulinda wasiibe! Ilikuwa ukiingia mgodini bila ruhusa ni faini kubwa sana au kupoteza maisha! Picha zote hizi zimepigwa mwaka 1951 huko katika mgodi wa Mwadui! Watu weusi wanavyotendeana ni jambo la khatari!

View attachment 604608View attachment 604609View attachment 604610
nani aliyekwambia kuwa Pengo ni bosi wa askofu wa Rulenge?. Pengo kaeleza kadri ya ufahamu wake na hii sio mara ya kwanza kwake kuongea.

Kama wewe haumheshimu Askofu Pengo sisi wengine tunamheshimu sana. Sio kwa umri wake tu, bali kwa kazi kubwa ya kiroho ambayo humu ndani hakuna anayeweza kuielezea mpaka ikaeleweka.
 
Aiseeee aiseee mkuu atakaye pinga haya bhasi
Pengo aongee na waumini wake wa Dar es salaam tu ndipo kwenye mamlala yake, akivuka tu kiluvya kuingia Kibaha hana mamlaka.

Kwa sababu ccm imejaa mijitu mijinga ilikuwa inamtumia Pengo wakidhani cheo chake ni kama cha Mufti kwa waislamu kwamba Mufti ni Tanzania nzima.

Hatutochoka kutoa elimu hii ili ukweli uwe wazi na watu wajuwe kweli.
 
Rais akitaka kuongea na Papa anawasiliana na Balozi wa Vatican hapa Tanzania,sio Pengo
Sio kweli hata vikanisa vya uchochorini huwezi wasiliana hata na askofu hadi suala lako ulipeleke kwa padri wa kigango au Mchungaji wako. Balozi wa papa hupokea masuala kwa kardinali hapokei straight. Hata akipewa straight atayarudisha kwa kardinali for comments
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?

Kwani ameshindwa kumweleza hukohuko mpaka alitoe public? hii ni kuliingiza kanisa katika malumbano ya kisisa na kuligawa kanisa! kama ameona mwenzie kakosea angelishawishi kakao cha baraza la maaskofu ndipo baraza litoe tamko!
 
Duuh huku kachukuliwa Pengo kule Mufti Jamaa wanajua kucheza na Majority sema tumesanuka atuwasikilizi hao vibalaka
 
Back
Top Bottom