Inasikitisha sana kuona hizi nyumba 2 muhimu zinaunguzwa, pamoja na uzuri wa nyumba ya Peniela na vitu vingi vya thamani vilivyokuwemo, kuna kile kibox alichopewa na John Mwaulaya, hajakifungua kujua kuna nini sijui hatima ya hiki kibox.
Nyumbani kwa Mathew ilikuwa ni nyumba ya thamani nyumba ambayo Mathew aliamini kuwa ni sehemu salama kuliko sehemu yoyote.
Lakini kulikuwa na vitendea kazi muhimu hii ikiwa ni pamoja na magari yake, lakini kulikuwemo na kitu cha muhimu zaidi ambacho kiliwagharimu muda pamoja na uhai wa baadhi ya watu, kitu hiki ni zile nyaraka za siri zenye formula ya kutengeneza virus hatari, hii nayo sijui hatima yake.
Ngoja nione mtunzi atakavyo fix hii sintofahamu ya haya mambo pamoja na mengine.
Kitu kingine na ambacho nilikiona mapema ni Mathew kuwaamini sana washirika wake na kuwaonyesha mambo mengi ya siri pale nyumbani kwake, hili jambo limemgharimu.
Poor Elibariki.