Pentekoste iliyochangamka

KIWANGO KIKUBWA CHA UWEZO WA IBILISI NI KUIGIZA MAMBO YA KIUNGU
 
MALAYA wamejazana makanisani. wahubiri hawana neno tena vinywani mwao. kile wanakitaka ni sadaka tuuu.
aibu kwenu mnaojiita wahubiri na watumishi mliojituma
 
kuna ndugu yangu amekuwa kama mganga anazunguka nyumba yake na machumvi ananyunyizia. uo sio ukristo kamwe haujawahi kuwa . ni ushirikina uliovalishwa jina la ukristo. pentekoste imeozaaa.
 
Neno Ni lenyewe, wewe ndio sio mwenyewe, umepotoka kabisa. Kumbuka ulimwengu wa Giza una vitu unavyotumia, vifaa mbalimbali Kama chungu, ngozi za wanyama, vibuyu nk.
Vilevile ulimwengu wa Nuru una vifaa mbalimbali ambavyo vimetumika na watakatifu na vinaendelea kutumika. Mf. Mafuta, maji, chumvi nk. Hivi huwakilisha ulimwengu wa nuru. So mtu akitumia hivyo ibadani sio kwamba anakosea hasha Bali wewe ndio unakosea kwa kuwapa watu uzito wakuwaamini watumishi wa Mungu. Na watu Kama wewe yesu kasema Ni heri kufungwa jiwe nakutoswa baharini.

Watumishi wa Mungu wanajitahidi kufundisha vizuri lkn watu Kama wewe ambaye hujui hata neno Wala huamini ktk miujiza Ni tatizo. Kwani Ni muujiza gani ambao wewe umewahi ukubali kwamba umetoka kwa Mungu?

Hao akina mwamposa wanakusanya pesa nyingi lkn sio kwamba wanafikia level za roman catholic ambao wanafanya biashara wanna maseminali, Wana mahospitali, wanauza vitabu, rozali, nk. Mwamposa kuuza maji tu unaona kakumalizia hela zote wakati pesa hizo zinatumika kuendeleza kazi ya Mungu. Acheni fikra potofu.
s
 
Roman haijawahi kuwa na hali mbaya kufikia hatua ya kufananishwa na pentekoste
pentekostre ingeanza zaman za romani basi ingekuwa na uozo kuliko roman ilipofikia. pentekoste inamuda mchache tuu ila imeenda njia ya kuzimu mapema mnooo.
singeli ba bolingon hazina sehem mbele za mungu.
hata uimbaji si wauvuvio tena ni kama wakina DIAMOND.
ubaya hakuna wakusimama na kuhubiri injili tena ya kweli.
 

unaweza kunionyesha kwenye maandiko baada ya kuja kwake Bwana yesu sehem wametumia hivyo?
maana hio ndio injili, maji hutumika ila si maji ya kununua.
mafuta hutumika lkin si ya kununua.
hio injili unayoisema sijaiona kwenye maandiko
 
Aibooo wanamwita Sir God Dady!!!😄😄😄Aisee Yani Kote mvurugano Tukienda Pentecost uko ni miujiza Roman Papa haeleweki😁😁 Lutheran nako wachungaji wanapenda Sadaka🤣🤣 na mali Sabato nako Chali wachungaji Hawasomeki🤣🤣 huku kwa ndgu zetu Wa Kobazi Majinii woiii utayapandisha kama Tuzo point za Halotel🤣🤣 Sijui nihamie Buddhism Yani nifuate Mafundisho ya Yesu na Mungu tu maana huku kwingine kunanichanganya kama CCM na CDM
 

kama umeshindwa kuona jambo la wazi kama hilo MUNGU akujalie.
woote hao ni roho ile ile iliokuwa kwa roman imehamia kwa pentekoste.
mungu amekuwa akiwaagiza nenda moto fulan ama katumie kitu fulani. pia kumbuka walikuwepo weengi wenye ukoma ila si woote waliambiwa wakajitose kwenye maji.
 
umenifurahisha sanaa sanaaaaaa.
inasikitisha kusikia wanamuita Mungu jina la mzaha kama ilo.
kiufupi biblia inasema yesu atakataliwa na makanisa watamtupa nje ya kanisa atakuwa anabisha hodi yeye atakaemsikia afungue atakula nae.

ila neema ilitujia sisi watu tusio wa israel baada ya waisrael kumkataa masihi. biblia inasema na sisi tutamkataa ili injili iwarudie israel tena watubu
 
Nyie si ndio mnaopiga kelele kuwa uislamu unamkandamiza mwanamke,,endeleeni kuwapa madhabahu akina Zumaridi lkn ukweli mbinguni mtapasikia tu..


Nipo pale..
 
unaweza kunionyesha kwenye maandiko baada ya kuja kwake Bwana yesu sehem wametumia hivyo?
maana hio ndio injili, maji hutumika ila si maji ya kununua.
mafuta hutumika lkin si ya kununua.
hio injili unayoisema sijaiona kwenye maandiko
Tuliza akili wewe usiwe mpingaji wa kila kitu, ufalme utakupitia kushoto alafu hao unaowaona waongo wakapasua. Mchungaji yeyote anakundi Sasa usifikiri Jambo la kuwa na kundi Ni mchezo mchezo, wale Mungu huwaangalia kwa ukaribu mno.

Kipindi Cha yesu alipakwa mafuta, yesu mwenyewe alitumia tope kumfumbua mtu macho. Majuzi mwamposa kauza tope hizohizo tu kule mbeya lkn makelele kibao.

Iko hivi; huduma ya neno Ni gharama kubwa mno ukitaka kuamini hili jaribu kujenga kakibanda kadogo alafu Pima gharama ndipo utakuja kujua sadaka kwa mwamposa haziibiwi.

Unafata upepo wa maneno ya wachawi ambao wamejaribu nguvu ya Mungu na kushindwa unafikiri watakuwa na maneno mazuri kwa watumishi? Lazima wataiponda huduma, Sasa na wewe usivyo na tafakari unaungana kwenye ngoma yao mnacheza kwa pamoja pasipo kushtuka kwamba umeshapotezwa kitambo tu huku ukijipa moyo kwamba fikra zako zipo sahihi.
 
Tapeli yule acha kumficha yule Mmalawi alielowea Zambia na kufanya biashara ya mafuta Tunduma na Mbeya usifikiri hatumjui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…