Mtu ambaye bado hata haujui maana ya Ulimwengu unapata wapi nguvu na akili ya kuhoji kuhusu Kanisa katoliki?
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia.
Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu;
aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele. Amina.