Pep Guardiola, Mwalimu bora wa miaka yote

sababu kubwa ya pep kuondoka bayern ni kutaka kuleta mpira wa pasi pale kitu ambacho wajerumani hawakitaki hao bayern toka pep ameondoka wamechukua UEFA? ...Mbona kocha hawamtimui?
Carlo ancellot alipofukuzwa, alikua anaifundisha ndanda kumbe [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji119]
 
Alipokuja epl wakasema hawezi beba.maneno kibaooo mara epl ligi ngumu ina top 4,sio kama la liga ina top 2.sasa kaanza kazi,wamebak vinywa wazi.pepo limehamia uefa.hawez beba uefa na akibeba mie nanya.akibeba uefa,mludi hapa mtuoneshe sehemu nyingine ya kuhamisha pepo la maneno ya hovyo kabisa.maana mmeanza kusema katumia pesa kibao,wakati mou juzi analaumu pesa ilikuwa ndogo.soka la sasa ni mijihela a.k.a "toa pesa upate kombe".halafu kuna kitu hakipo sawa sio kwamba ukitumia tyu pesa bila uchaguzi sahihi wa mahitaji ya mfumo wako,ama kocha mzuri utapata mafanikio...la hasha.lazima uzingatie hayo na ndo yanayotoa picha ya wewe n kocha wa aina gani.kuwa kocha mzuri hakukufanyi wewe "kumfingia"ukasema tutaona kama atabeba uefa..kwani asipobeba uefa na akabeba epl wewe unadhurika na nn au asipobeba epl akabeba uefa tatizo liko wapi.tuache ushabiki kizuri kisifiwe na kizuri kidogo kikosolewe ili kiwe kizuri zaid.
 
Acha wivu wa kike we jamaa. Pep Gandiola kwa sasa na kabla ni kocha bora toka alipokuwa barca mpaka Bayern na sasa City.

Pep ndio kocha mwenye rekodi ya kushinda game 18 mfululizo kwenye ligi 5 bora ulaya kwa maana ya la liga, Serie A, Epl, Bundesliga na ligue 1. Ameweka rekodi akiwa na munich. Anategemea kuifikia kama si kuivunja jumamosi dhidi crystal palace.

Ni kocha anayejiamini. Si sawa na Fergie na Wenger. Hawa wamekaa kwenye club 1 kwa zaidi ya m
Iaka 20. Yeye anakaa miaka 3-4 anaondoka kutafuta chalenge nyingine.

Kafundisha ligi 3 kubwa ulaya. Akitoka hapo ataenda italia baadae france
 
Ilaa jamani mbona ligi ndio kwanza mbichi hii..! Kumpa pep 100% ya kuchukua Epl , Ni kushusha hadhi Epl kwakweli... [emoji23][emoji23]
Sitotegemea kumuona pep aking'aa kwa round ya 2 mbele ya Arsenal ,Liverpool en Chelsea lazima wamtoboe tu.
Karata yangu ya Epl ipo kwa WENGER 100% , Mornho 90% na Klop kwa 85 % [emoji23][emoji23]

Hata kama anaongoza Kwa gape ya 15 points. Pep kwa WENGER Ni mchumba tu. [HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG]
 
Kweli hasira hasara.umeudhika na nn bro!!?mpaka pep akawa njiani kuolewa na wenger!!!
 
Umepiga mle mle,
 
Kwa sasa man city ni kama msalaba wa jumuia.kila nyumba lazima upite.[emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji122][emoji119][emoji119][emoji119] Pep ni bonge la kocha. Af anatumia sana akili huyu jamaa..anakufanya ww ndio upaki basi[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Uwekezaji umelipaje? Mwaka jana alitoka kapa! Msimu wa mwaka huu haujaisha! Sasa unasemaje uwekezaji umelipa? Au kuongoza ligi ndiyo kulipa kwenyewe?
Kuongoza ligi ndiyo kulipa kwenyewe Mkuu. Kuhusu msimu uliopita ndiyo kwanza alikuwa ameanza kazi, na kumbuka ana falsafa yake ktk kufundisha Mpira. Sasa ulitaka afike na kuchukua ndoo? Sasa hakuchukua kila msimu huj jibu unalo bila shaka...
 
Waambie hao
 
If you look at EPL table, you will notice that the gap between United and city is too big and the gap between United and Chelsea is very close so is the rest of the teams.
Which means Man city is in another league [emoji2]
 
Kifupi wasiopmpenda Kaja!!! Ubishi mwingi usiokuwa na tija tu. Ndiyo maana kuna baadhi huwa wanasema Messi10 eti siyo bora kisa kacheza ligi moja tu, swali je! Timu yake ya taifa iko Spain? Hata Hivyo ushawahi kuona wapi Mfalme ana hama Kingdom?...

Utawasikia eti Oooh Pep Gardiola hawezi EPL?? Swali Je! Man City iko League gani duniani? Subirini, akichukuwa na ndoo ya UCL sijui mtasema NINI tena? Labda mtasema eti Oooh kabahatisha tu!!!!

Pep Gardiola ni Kocha bora sana hata mkibisha lakini ipo siku mtakubali tu...
 
Nimoto
 
Jamaa unajitoa ufahamu au?
Unasema Bayern kombe la bundesliga ni lao miaka nenda rudi unasahau walilikosa miaka miwili ya utawala wa Dortmund wazee wa BVB enzi za Klopp.
Unasahau juzi juzi tu baada ya kuondoka Josep Guardiola babu Carlo Anchelotti kafanya vibaya sana hadi kafukuzwa?
Kwani huyo Anchilotte sio zaidi ya Bashite?
Unatumia kilevi gani mchambuzi fake wa soka?

Kuhusu kutochukua tena UEFA subiria utayakana haya maneno yako. Hata ukifuta post yako kumbukumbu itabaki hapa kwangu na nitakukumbusha tuombe uhai.
 
Hata Omog alipewa sifa lukuki,leo hii Manyara hataki kumsikia.
 
Angalia bajeti na thamani ya kikosi chake.
 

Wengi mnabishana ila hamjui historia wala nini mnabishia. Maswali yako yote nimejibu kwenye comments baada ya hiyo ambayo umeniqote.

Ancelotti alifukuzwa baada ya kugongwa vibaya first leg na PSG UEFA sio ligi. Kama hata hili dogo tu hujui acha kujiita mshabiki wa soka. Hili ndo kombe wanalotaka ambalo si Carlo wala Pep aliweza kuwapa. Mbona hawakuvunja kandarasi alipofungwa kwenye ligi, kwanini UEFA tena game moja tu ambalo halikua na athari yeyote maana bado wangepita makundi? Jibu ni, UEFA is what matters most kwao sio ligi ambayo wameshinda mara 27. Pep alifeli Bayern

Nikumbushe siku Pep akishinda UEFA na timu nyingine yeyote ile nitakutumia muamala mpesa, ubaya hiyo siku haitakuja kutokea tena. Kule mtoto halali na hela
 
Mkuu unakumbukumbu ndogo sana au unajitoa ufahamu.
Kwanini baada ya Guardiola hawajafanya vizuri sana kama wakati alipokuwepo?
Unajua kwanini Luis Enrique alilalamikiwa sana kuuwa mfumo wa ushindi wa Barca ambao ndio falsafa ya Club yao?

Luis Enrique alileta mfumo wa miguvu na direct play kwenye midfield ya Barca, mwanzo walipata mafanikio kidogo lakini alipoondoka Xavi mambo yakabadilika yakachangia kuondoka kwa Luis Enrique pale Barca. Nimekupa maelezo haya ujue kwamba kufikia viwango vile na ukali ule wa Barca ni kutokana na Ubora wa kocha Guardiola na falsafa ya team ambayo ndio jamaa alitaka kuipeleka Bayern na sasa anaipandikiza Man City.

Nitaku-follow ili niweze kukumbuka siku Guardiola akinyakua tena UEFA. Nitakukumbusha na hiyo pesa yako utaninunulia chupa ya mvinyo inaitwa Barolo toka Southern Italy ambayo imehifadhiwa miaka angalau mitatu(3). Tafadhari nunua kabisa sasa hakikisha ni Dry Red Wine.
 

Nitakununulia huo mvinyo bila tashwishwi yeyote ile, tena mimi ndo nitakukumbusha, tatizo hiyo siku haitakuja kutokea tena.

Hapo hapo kwa Enrique ndo mnapojifunga sababu Luis kashinda kila kitu ambacho Pep alishinda Barca, hata baada ya kuondoka kwa Xavi bado Luis alishinda UCL na ligi, je nae ni kocha bora mithili ya Pep? Ila Luis huyo huyo alifeli vibaya alipokuwa Italy kabla ya kwenda Nou Camp. Ndo maana tunasema Messi, Iniesta na Xavi walifanya makocha waonekane bora ilhali hawana lolote lile.
 
Mkuu makocha wenye lolote niwapi?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…