Pesa haihitaji kelele, ukiona mtu anajitapa, mpuuzie. ‘GSM wa Katoro’ kafanya matusi aseee

Pesa haihitaji kelele, ukiona mtu anajitapa, mpuuzie. ‘GSM wa Katoro’ kafanya matusi aseee

Hao hao wanaomwaga pesa ukifika mskwao utapiga yowe, hawajui kuwekeza wanapenda sifa na mashindano
Kabisa Kuna dogo tumesoma nae mwanza green view miaka hiyo aliacha shule kaenda kwenye DHAHABU Kwa baba yake kapiga pesa kibao sijui alifanyaje akafulia balaa, sijui kama asharud I top tena sijamcheki miaka, ila Kuna dogo alikua burn CD pale geita town alimake pesa sio poa
 
PICHA linaanza Kijiji cha katoro, geita. Ni sherehe ya send off tu si harusi, bibi harusi kapewa bilioni Moja na milioni mia nne kama zawadi ya wana kamati, kabebwa kwenye helicopter, gari zilizopo kwenye msafara tu balaa Mzee, Dola zimetunzwa Kwa msanii alikiba, sio poa watu wana hela.

Kuna yule jamaa wa Singapore mtumieni zile shots asafishe macho, pesa HAITAJI KELELE.

Harusi za wachaga nilizani ni za kitajiri kamati tu wanatia milioni mia mbili mia tatu, Jana ndo nika gundua hao jamaa ni machenchele tu pesa ya kawaida sana, halitoshi mjini ni ndogo sana, kubwa Kwa sisi masikini.

View attachment 3628591
View attachment 3628596

Yaani Send off mtu anazawadia Bilioni. Enzi za JPM haya mambo hayakuwepo...VIKOSI KAZI vingekuwa tayari vimeshafanya kazi yao.

Anyway yote Maisha tu, ila sidhani kama ni sifa kujiona una hela, Mimi naona kama ni ushamba tu wa wawasukuma kushika hela uzeeni
 
Kabisa Kuna dogo tumesoma nae mwanza green view miaka hiyo aliacha shule kaenda kwenye DHAHABU Kwa baba yake kapiga pesa kibao sijui alifanyaje akafulia balaa, sijui kama asharud I top tena sijamcheki miaka, ila Kuna dogo alikua burn CD pale geita town alimake pesa sio poa
Kiufupi kila mtu anayo bahati yake!
 
Hakuna cha ajabu hapa. Mnaijua net worth ya mtoa zawadi?

Ukitaka kuyaangalia mambo kwa usahihi yaweke kwenye context sahihi. Consider them in relative terms, not absolute terms!

Mtu ambaye net worth yake ni TZS 5 million akitoa zawadi ya TZS 1 million (20% ya net worth yake) atakuwa ametisha kuliko mtu mwingine mwenye net worth ya TZS 25 billion aliyetoa zawadi ya TZS 2.5 billion (10% ya net worth yake)!
Hao wenye net worth wasikuchanganye achana na hizo fikra za kishamba, una mjua you tuber yule jamaa nani sijui juzi katajwa bilionea ye kadai hana hiyo hela in case of pesa halisi, hizo NAMBA tu mkuu
 
Wivu huo, watajua wenyewe bwana! Pesa zake acha azifanyie kufuru, mara washamba mara sijui nini, wasukuma wasukuma tushawazoea watajiju!😂
Screenshot_20260713-234339.png
comment ya mwisho🔥📌
 
Daah,yaani wanamiliki miguu ya kuku.
Kheee! Sasa utamiliki hizo pesa bila mguu wa kuku mama! Unajiamini nini? Kuna jamaa mmoja anaitwa baraka naye ana mashimo huko katoro, siku moja tumeenda sauna na rafkiangu, tukamuona kaja, anajiandaa kuingia akavua shati, huku nyuma naona bastola niliogopa! Sema huyu huwa ana masifa na ana ego mbaya! Kipindi hicho zimeingia anaconda mil 70 kainunua mapema sana, akiingia club ni yeye tu huko kwenye mic, dorimeee duh! aisee nyie hizi pesa acheni tu!
 
Back
Top Bottom