Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Mambo yamebadilika ndani ya CCM. Dosari kubwa ni jinsi mchakato wa kupata wagombea unavyoendeshwa ambapo hakuna tena muda wa mwanachama anayegombea kujieleza kwa undani na kumwaga sera na mipango yake ya maendeleo.
HAKUNA mgombea yoyote katika jimbo lolote aliyepata kura tano na kuendelea ambaye hajatoa rushwa kwa wajumbe wanaopiga kura, HAKUNA. Mambo ya umaarufu na sifa zingine yanafuata baadae. Na hii si siri hata wakuu wa chama wanajua.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya huko nyuma kwamba sasa kwenye CCM pesa imekua ndio qualification ya mtu kuchaguliwa kwenye uongozi wakati hapo awali pesa ilikua ni disqualification.
Hatari yake ni kwamba inajenga utamaduni wa watu kununua kura na kununua chaguzi na hata wale malaya wa kisiasa wanatengenezwa na tabia hii ambayo imeachiwa iote mizizi kitu ambacho sio afya kwa mustakabali wa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.