Pesa ilikuwa ndiyo sifa ya kwanza kwenye kura za maoni CCM

Pesa ilikuwa ndiyo sifa ya kwanza kwenye kura za maoni CCM

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Mambo yamebadilika ndani ya CCM. Dosari kubwa ni jinsi mchakato wa kupata wagombea unavyoendeshwa ambapo hakuna tena muda wa mwanachama anayegombea kujieleza kwa undani na kumwaga sera na mipango yake ya maendeleo.

HAKUNA mgombea yoyote katika jimbo lolote aliyepata kura tano na kuendelea ambaye hajatoa rushwa kwa wajumbe wanaopiga kura, HAKUNA. Mambo ya umaarufu na sifa zingine yanafuata baadae. Na hii si siri hata wakuu wa chama wanajua.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya huko nyuma kwamba sasa kwenye CCM pesa imekua ndio qualification ya mtu kuchaguliwa kwenye uongozi wakati hapo awali pesa ilikua ni disqualification.

Hatari yake ni kwamba inajenga utamaduni wa watu kununua kura na kununua chaguzi na hata wale malaya wa kisiasa wanatengenezwa na tabia hii ambayo imeachiwa iote mizizi kitu ambacho sio afya kwa mustakabali wa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.
 
Ukiwa huna hela hata utoe sera nzuri kiasi gani huchaguliwi..wajumbe wanaona kama unawapotezea muda kujinadi,wanakusubiri umalize uondoke[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkono mtupu wajumbe hawaulambi.
Tena kama hujatoa pesa na ukijifanya kujieleza kwa sera na mipango wanakuzomea uondoke usiendelee kuongea!
 
Mtu ambaye hana pesa atakuwa na Sera gan , hao ukiwapa uongozi wanaenda kukomboa ukoo wao wa kimaskin badala ya wananchi , kigezo cha Kwanza cha mgombea anatakiwa awe na pesa chafu , istoshe maendeleo ya jimbo yanategemea mikakati ya serikali kuu, ubunge ni bortion tu.
 
Mwaka huu wajumbe wamevuna hela za kutosha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hii ni changamoto kubwa sana kwa CCM.

Hili jambo likiachwa liwe ndio utamaduni wa Chama hicho basi mapambano ya kujenga jamii yenye haki na usawa itakua ni ngonjera za kwenye makaratasi tu.

Mtu akiwa Mbunge au diwani ni kwasababu mfuko wake wake umekua mnene kuweza kuwanunua wajumbe wenye njaa.
 
Nadhani kuna haja ya kubadili huu utaratibu wa wajumbe wa chache kupiga kura za maoni, waruhusu kila mwanachama mwenye kadi apige kura hapa rushwa itapungua maana itakua ni ngumu kuhonga wanachama wote kwenye jimbo au kata
 
Nadhani kuna haja ya kubadili huu utaratibu wa wajumbe wa chache kupiga kura za maoni, waruhusu kila mwanachama mwenye kadi apige kura hapa rushwa itapungua maana itakua ni ngumu kuhonga wanachama wote kwenye jimbo au kata
Naunga mkono hoja yako mkuu. Halafu vyombo vilivyopewa jukumu la kupambana na rushwa havikufanya kazi yake ipasavyo
 
Sasa ndio wakati wa vikao vya juu kuchunguza wagombea wote walio toa au kujihusisha na rushwa hata kama walipata Kura 100% waondolewe na lipitishwe jina ambalo halina makandokando.
 
Tulipokosea ni pale tulipoamua kuipa siasa thamani kubwa isiyistahili kuliko taaluma na ujuzi mwingine..
Kweli kabisa Mkuu. Kazi za taaluma siku hizi zinapigwa kikumbo na Maprofesa na Ma Dr wetu wote wakitaka kua wanasiasa!!! Ukweli ni kwamba mbali ya mshahara mnono na marupurupu kibao, kua mwanasiasa hasa Ubunge imekua ni njia ya kupata ukwasi wa mali kwa kutumia advantage ya uheshimiwa na urahisi wa kupenya kila mahali
 
sasa ndio wakati wa vikao vya juu kuchunguza wagombea wote walio toa au kujihusisha na rushwa hata kama walipata Kura 100% waondolewe na lipitishwe jina ambalo halina makandokando.
Mkuu nakubaliana na wewe mia kwa mia. CCM ngazi ya juu inapaswa waonyeshe mfano kwa wote waliotumia rushwa. Ikibidi wapitishe majina ya wagombea wasafi hata kama italazimika kumchukua mtu aliyepata sifuri lakini hakutumia rushwa kwenye uchaguzi.

Hilo litakua fundisho na salamu mahsusi kwa wajumbe wapiga kura na naamini kabisa wananchi wataunga mkono na kukipa chama kura
 
sasa ndio wakati wa vikao vya juu kuchunguza wagombea wote walio toa au kujihusisha na rushwa hata kama walipata Kura 100% waondolewe na lipitishwe jina ambalo halina makandokando.
Naunga mkono hoja imagine wabunge wote waliopata kiinua mgongo wamehonga na wameshinda kura za maoni, vile magufuli ameonyesha udhubutu tunaomba na hii rushwa kwa wagombea aitendee haki
 
Back
Top Bottom