Pesa mtaani zimepotelea wapi? Je, biashara yako inaendaje?

Pesa mtaani zimepotelea wapi? Je, biashara yako inaendaje?

My turnover dropped by 60% comparing to Magufuli era.........dont know what gonna happen,future looks bleak!
So hizo kodi wanazodai kukusanya maradufu wanakusanya kwa akina nani kama wafanyabiashara turnover zao zinashuka maradufu hivyo? Wanapika data? Mitaji inakwenda sana nje ama shida ni nini?

Hata malipo ya serikali kwa kipindi cha karibuni yanasua sua sana. Inawezekana kuna jambo tunafichwa!!

CC: econonist JokaKuu Nguruvi3
 
Wakuu habari zenu,

Wakati wa utawala wa Mkapa kuna hali ya ukata wa pesa ulijitokeza tukauita UKAPA.

Wakati wa JK kiasi flani mambo yakalainika japo ufisadi ulikuwa juu sana na mfumuko wa bei. Kila mtu aligeuka dalali. Pale Mnazi Mmoja wakazaliwa madali wenye vitambi na kiburi, huwezi uza gari kupitia wao.

Wakati wa JPM likajitokeza neno VYUMA vimekaza. Mwanzoni mwa utawala wa JPM miradi binafsi na iashara zilidoda, hili hata mimi lilinikumba lakini kuna wakati mambo yalininyookea hatari.

Awamu hii ya mama, tulitegemea mambo yanyooke zaidi kwani kwa kauli kuwa anaifungua nchi tulitegemea neema zaidi.

Mambo yamekuwa kinyume sana. Biashara nyingi zimeyumba, mfano kariakoo hali sio nzuri kabisa.

Makampuni mengi binafsi yako hoi.

Shule binafsi wanalia.

Wananchi huku chini uraiani hali ni tete kuliko maelezo.

Je huko uliko hali ikoje?
Tunakusanya pesa ya kufanikisha ushindi kwenye uchaguzi
 
Inaweza ikawa hana washauri wazuri, kakosa maono labda, au kipaumbele chake ni kingine, labda ni siasa za maji taka za kuwaza wakati ujao na namna ya kurudi madarakani, sijui.
Lakini itakua poa tu mwisho wa siku.
1. Ugumu wa maisha unagusa vyama vyote hii inaweza kumpa taabu 2025.

2. Hawa waimbaji kuwa anaupiga mwingi huenda ndio wanashiba na kumpumbaza
 
kama watu wameenda likizo ya kufikiri wanaamini kila kitu kafanya samia unategemea nini? majitu hata mvua ikinyesha baada ya kumshukuru Mungu wanamshukuru hangaya, akili hamna kabisa sikuhizi ndiomaana naungana kabisaaa na Trump kwamba miafrika inabidi tutawaliwe tena ndio akili zitaturudia vinginevyo hamna kitu kabisaaaaa.
 
Mkapa alijenga nchi vizuri ikawa kwenye direction sahihi, akaja Kikwete na kuivuruga vuruga, kiasi kuwa Magufuli alipojaribu kuinyoosha tena ikawa tatizo kubwa, na mama huyu ndiye imekuwa taabu kabisa. Uongozi wa nchi huhitaji uthabiti na maono imara, siyo blah blah za kujaza pesa kwenye mzunguko ili kufurahisha watu.
Kikwete na wanamtandao wenzao walishikwa mfukoni uchumi ukahamia mifukoni mwa matapeli! Ilifia hatua serikali ilikopa hela kwa watu binafsi kulipa mishahara!
Magufuli ndo aliididimiza zaidi nchi kwa kutumia theories zilizoshindwa kwa wengine!

Swali ni jee, hizi data tunazopewa na TRA na BoT zinapikwa? Hakuna reflection katika real life juu ya kinachohubiriwa na hao watu.
 
kama watu wameenda likizo ya kufikiri wanaamini kila kitu kafanya samia unategemea nini? majitu hata mvua ikinyesha baada ya kumshukuru Mungu wanamshukuru hangaya, akili hamna kabisa sikuhizi ndiomaana naungana kabisaaa na Trump kwamba miafrika inabidi tutawaliwe tena ndio akili zitaturudia vinginevyo hamna kitu kabisaaaaa.
Inasikitisha waimba mapambio ni watu wazito.

Nasema Samia ni anguko la nchi
 
Kikwete na wanamtandao wenzao walishikwa mfukoni uchumi ukahamia mifukoni mwa matapeli! Ilifia hatua serikali ilikopa hela kwa watu binafsi kulipa mishahara!
Magufuli ndo aliididimiza zaidi nchi kwa kutumia theories zilizoshindwa kwa wengine!

Swali ni jee, hizi data tunazopewa na TRA na BoT zinapikwa? Hakuna reflection katika real life juu ya kinachohubiriwa na hao watu.
Waziri wa fedha ni Mwigulu bwana propaganda unategemea nini TRA?
 
1. Ugumu wa maisha unagusa vyama vyote hii inaweza kumpa taabu 2025.

2. Hawa waimbaji kuwa anaupiga mwingi huenda ndio wanashiba na kumpumbaza
Natapata ukakasi sana na kuchelea kuamini itampa tabu, unajua mkuu uchumi unaposhuka ni unatugusa sisi ambao tupo kati na chini, na sisi sio sehemu ya watu wa maamuzi ya nchi hii.
 
Natapata ukakasi sana na kuchelea kuamini itampa tabu, unajua mkuu uchumi unaposhuka ni unatugusa sisi ambao tupo kati na chini, na sisi sio sehemu ya watu wa maamuzi ya nchi hii.
Mkuu unakumbuka 2015?
Kilichompa Magufuli urais ni kelele za wanyonge zilizidi ikawa hakuna namna Membe mtoto mpendwa akatiswa?
 
Back
Top Bottom