Pesa ni Shetani; Mchezaji aliyekataa kuvaa jezi ya kuunga ushoga alazimishwa kuchagua kati ya mshahara wa milioni 200 kila wiki ama kurudi Afrika

Pesa ni Shetani; Mchezaji aliyekataa kuvaa jezi ya kuunga ushoga alazimishwa kuchagua kati ya mshahara wa milioni 200 kila wiki ama kurudi Afrika

Kabis mkuu.

Ingelikuwa ni jezi nyuma inapicha ya wanaume wan@fir@..n..a ningeona ina make sense kukataa.

Ila hizo just ni rangi tu ambazo hazina maana yoyote ile kiimani.

Ni sawa na mimi leo nikatae kuvaa shati yenye nyota na mwezi ama shati yenye picha ya ng'ombe eti kwa sababu tu huyo ng'ombe kuna watu wanamuabudu na dini hairuhusu kuabudu ng'ombe so nikatae kuvaa jeI yenye picha ya ng'ombe eti kisa nikivaa nitakuwa nasapoti,hii ni kutokuwa na mawazo yaliyotulia tu.

Sioni kama sahihi kukataa kuvaa hizo jezi kwa sababu ya hizo rangi,kwanza kukataa kwake ndio kunazidi kuipaisha hiyo lebo ya ushoga kuliko angekubali.

So kama lengo asisapoti ushoga anajikuta anausapoti zaidi kwa kuupinga kwake kwa sababu dunia yote iko macho na yeye.

Yeye angeliivaa tu na mambo yangeisha kimya kimya tu.

Kuna mambo ukiyakataa ndio unazidi kuyaa nguvu,na ukiyakubali ndio unazidi kuyanyima ngumu.

Ni suala la kufikiri vizuri tu.
We ndio unampoteza kijana.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Morcos Alonso hapigi goti kupinga ubaguzi wa rangi lakini hawajamfanya chochote kwasababu ana uhuru wa maoni. Ila gueye sasa...
Kupinga ubaguzi ni fair play, kwa hiyo ni jambo la hiyari, sio la lazima au la kisheria. Mikataba ya kuidhamini biashara kupitia jezi sio jambo la hiyari, ni la kisheria hivyo ni la lazima. Kwa hiyo tofautisha kutopinga ubaguzi na kutovaa jezi
 
Kutokuamini au kuunga mkono ushoga ni haki yake ya msingi, kwa hiyo kumshurutisha kwa namna yoyote kuwaunga mkono mashoga ni kukiuka haki yake ya msingi ya kiimani.
Hapo kuna mkataba ambao unamlazimisha avae jezi. Kama anaona hapendezwi kuivaa, avunje tu mkataba na timu ili kuilinda haki yake ya msingi

Unawaona hawa jamaa wa timu ya taifa ya Cameroon! Walilazimika kuvaa vizibao kwa sababu ni mkataba wa kibiashara uliwalazimisha, mchezaji ambaye hataki aondoke tu asicheze World Cup

1653431838822.png
 
Mhhh , hapo kwenye payroll pagumu sana, najua Magufuli alikuwa na mapungufu mengi kwenye uongozi wake ila huenda ulikuwa ni mpango wa Mungu kutpa rais ambae angekuwa na msimami mkali kuhusu janga la covid, ingekuwa ni rais mwengine tungepigwa lock down
Hakuna Rais yoyote Tanzania angeweza kutoa amri ya lockdown wakati wa COVID. Hakuna mtu asiyefahamu kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni LAZIMA tutoke ili kutafuta pesa mkono uende kinywani.
 
Kwa wenzetu huko ukiwa mtu maarufu na ukathibitika huungi mkono ushoga hilo ni tatizo kubwna sana, sitashangaa wakimbambikia kesi kama za r kelly kwamba alibaka binti wa miaka 15.
R. Kelly hajabambikwa kesi.
 
Mpuuzi ni ww unayekurupuka kuandika bila kufikiria kwa kina, jiulize kwann watu maarafu kama wachezaji,wanamiziki, waigizaji ndo wanapewa madeal yakupiga promo ushoga? Kapuku kama ww ukipiga promo ushoga nani atakuelewa?

Fikiria kwamba huyo dogo ana watu wangapi hapo nyuma wanamkubali, na ni role model wa watu wangapi?

Fikiria ni watu wangapi watadumbukia kwenye maswala ya ushoga baada ya yeye kuvaa hiyo jezi?
Hivi mtu unaweza tu kudumbukia kwenye masuala ya ushoga eti tu kwa sababu mchezaji, actor au mwanamuziki unayemshabikia kavaa jezi yenye rangi zinazoshabikia ushoga!!!! Utakuwa na matatizo ya akili au labda tayari ulikuwa unashabikia mambo hayo kabla.
 
Halafu wakiambiwa hizi tumeletewa tunashupaza shingo,cheki wamiliki wa hio team wamepiga kimya,kuna haja waafrica tujifikirie upya kuhusiana na hizi dini
Hata huu mchezo wa mpira unaotufanya tushabikie simba na yanga nao tumeletewa mkuu, kwahiyo tulivyo letewa ni vingi.
 
Hapo kuna mkataba ambao unamlazimisha avae jezi. Kama anaona hapendezwi kuivaa, avunje tu mkataba na timu ili kuilinda haki yake ya msingi

Unawaona hawa jamaa wa timu ya taifa ya Cameroon! Walilazimika kuvaa vizibao kwa sababu ni mkataba wa kibiashara uliwalazimisha, mchezaji ambaye hataki aondoke tu asicheze World Cup

View attachment 2237550
Hana mkataba wa ku support ushoga bali kutumikia club kwenye kucheza mpira, kwenye mkataba wake hakuna kipengele kwamba ataunga mkono mashoga ndo maana amekataa kuvaa jezi yenye nembo hiyo......anaweza kupewa jezi ambayo haijawekewa hiyo nembo ya mashoga na labda akawekewa nembo nyingine ambayo haikwazi imani yake. Huwezi kumlazimisha kula kitimoto kisa wewe mwenye club unaamini katika kula kitimoto, watu wana haki ya kuamua kuhusu mambo yao ya kiimani ndo maana kuna imani mbalimbali za kidini, uislamu, ukristo nk. na kila mmoja ana haki na uhuru wa kuamini kadri ya imani yake, nafikiri utakuwa umenielewa barabara........
 
Hana mkataba wa ku support ushoga bali kutumikia club kwenye kucheza mpira, kwenye mkataba wake hakuna kipengele kwamba ataunga mkono mashoga ndo maana amekataa kuvaa jezi yenye nembo hiyo......
lakini kuna mkataba wa kufanya kazi ya kucheza mpira iliyomfanya aajiriwe, ikiwa ni pamoja na kuvaa jezi za mazoezi, away na home games. Au ulitaka acheze uwanjani na jezi yenye rangi tofauti na waliyovaa wenzake? 😁
 
Basi avunje tu mkataba, ailipe PSG hela zake za kuvunja mkataba, arudi Senegal akacheze Horoya ya Makambo au Teungueth ya Sakho
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi mtu unaweza tu kudumbukia kwenye masuala ya ushoga eti tu kwa sababu mchezaji, actor au mwanamuziki unayemshabikia kavaa jezi yenye rangi zinazoshabikia ushoga!!!! Utakuwa na matatizo ya akili au labda tayari ulikuwa unashabikia mambo hayo kabla.
Bora useme wee. Hawa watu sijui wanawaza nn
 
Kwa jinsi jambo hili lilivyokwenda viral nilitegemea mabilionea wakiarabu wangempa support dogo kwa kumuambia shikilia msimamo wako usihofie kuhusu kupoteza kazi, sisi tutaku fadhili mamilioni ya pesa kwa kulinda misingi ya dini
Aliyekuaminisha kuwa mabilionea wa kiarabu ni wafia dini nani?hao ndio wanaongoza kupiga hizo taka taka kwenye private party zao kwenye mahekalu na ma yatch!
 
Ni uongo.

Gueye hii ni mara yake ya pili kukataa kuvaa jezi ya hivyo na hakukatwa mshahara, iweje leo?

Na hata hivyo uhuru inamaanisha siyo lazima kukubaliana nao. So kama haukubaliani nao mtazamo wao ila ukawaheshimu kama binadamu then haina tatizo.
Mimi ndio siwaelewagi hapo mashoga
1.wanataka kugongana jinsia moja ,fine
2.wanataka kubadili jinsia ,fine
Wafanye upuuzi wao na jamii Yao kwa Nini wa force hii kitu iwe observed na kila mtu?
Sisi ni straight hatupendi ushoga
Waheshimu Hilo basi hatutawaingilia nao wasituingilie wasilete agenda zao kwenye mambo ya general public.
Hawa mapunga wana nguvu angalia tv na redio zetu hapa zimejaa mapunga tu na hata wale wanaojiita machawa au wambea wana vielement vyote vya kipunga na wanapewa attention hata na swrikali katika event za kijamii
Mijitu kama J.lukule ,Dr Kimbika ,Mwajaku na sijui Ari SI toto mapunga tu yalee!
 
Wafanye upuuzi wao na jamii Yao kwa Nini wa force hii kitu iwe observed na kila mtu?
na wao watakuuliza kwa nini ulipofunga ndoa kanisani au msikitini, bado ulitaka uwe observed ukumbini kwa kufanya sherehe ya harusi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] sasa wakisoma hapa wabongo, utaona mapovu yao juu yako.
Watakuwa wajinga. Leo hii idadi ya watu wanaokimbilia kuishi US na Ulaya ni mamilioni. Wanaoshabikia macelebrity wa huko ni mamilioni. Wanaotegemea misaada na mikopo nafuu toka huko ni mabilioni.

US na nchi za EU ndizo nguzo kuu ya LBTQ. Kama kweli umeamua kupambana na ushoga 💯 basi acha kabisa ushirikiano nazo. Kata hata mawasiliano nao. Wala usiende huko au kuruhusu mwakilishi wa nchi hizo kukanyaga nchini kwako. Be extreme ndio tujue kweli umeamua kupambana na ushoga bila tashwishwi wala kupepesa macho.

JK na Uhuru Kenyatta wametupa busara ya bure sisi Waafrika. Ni kupotezea tu as long as hakuna anayetulazimisha na sisi tuwe hivyo.
 
Mimi ndio siwaelewagi hapo mashoga
1.wanataka kugongana jinsia moja ,fine
2.wanataka kubadili jinsia ,fine
Wafanye upuuzi wao na jamii Yao kwa Nini wa force hii kitu iwe observed na kila mtu?
Sisi ni straight hatupendi ushoga
Waheshimu Hilo basi hatutawaingilia nao wasituingilie wasilete agenda zao kwenye mambo ya general public.
Hawa mapunga wana nguvu angalia tv na redio zetu hapa zimejaa mapunga tu na hata wale wanaojiita machawa au wambea wana vielement vyote vya kipunga na wanapewa attention hata na swrikali katika event za kijamii
Mijitu kama J.lukule ,Dr Kimbika ,Mwajaku na sijui Ari SI toto mapunga tu yalee!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3] utapasuka bureee,
 
Watakuwa wajinga. Leo hii idadi ya watu wanaokimbilia kuishi US na Ulaya ni mamilioni. Wanaoshabikia macelebrity wa huko ni mamilioni. Wanaotegemea misaada na mikopo nafuu toka huko ni mabilioni.

US na nchi za EU ndizo nguzo kuu ya LBTQ. Kama kweli umeamua kupambana na ushoga [emoji817] basi acha kabisa ushirikiano nazo. Kata hata mawasiliano nao. Wala usiende huko au kuruhusu mwakilishi wa nchi hizo kukanyaga nchini kwako. Be extreme ndio tujue kweli umeamua kupambana na ushoga bila tashwishwi wala kupepesa macho.

JK na Uhuru Kenyatta wametupa busara ya bure sisi Waafrika. Ni kupotezea tu as long as hakuna anayetulazimisha na sisi tuwe hivyo.
Umemalizaaaaa.
 
Mi wangekuta tu nimeshawaachia mshahara wao nipo zangu Africa. Utu wangu ni wa thamani kuliko fedha. Pesa ipo kwa ajili ya kunitumikia mimi na utu wangu na siyo kinyume chake. Halafu ningemsubiri wa kuleta fyoko fyoko. Angepata cha kusimulia vizazi vyake!

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
Mkuu wewe pambana na kura
 
Back
Top Bottom