youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,319
- 3,097
Pesa nyingi ninazopata kwenye Freelancing zianaishia kuwalipa vijana wanaonisaidia kufanya kazi. Hii level inaitwa dropservicing
Nitakuelekeza mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kufanya dropservicing... Pia ukitaka kufanya freelancing zingatia haya
Kwanza kabisa lazima uanze kama freelancer wa kawaida. Ili ujifunze utaratibu wa Freelancing ulivyo kuanzia kwenye kutafuta clients, kufanya kazi, kupokea malipo.
Unaweza ukaanza na freelancing platforms kwa ajili ya kupata experience. Experience + portfolio
Kwanza kabisa, kufanikiwa kwenye Freelancing ili ufanye dropservicing
Jifunze kutafuta clients wengi na kazi nyingi
Kuna njia nyingi sana za kutafuta clients, (tumia zote) Ni rahisi sana kutafuta clients. Kwasababu kuna soko kubwa sana na watu ni wengi sana wa kufanyia kazi
Njia nyingine lazima ujue kutengeneza offer zenye rate kubwa. Ili kufanya dropservicing lazima ujue kuchaji pesa kubwa ili uwapatie wengine wazifanye.
Offer zinatengenezwa kwa kutuma proposal na kutengeneza project gigs. Jifunze offer creation Kitabu kinaitwa mafia offer
Ukichaji bei kidogo, utapata clients madalali wanakupa kazi nyingi ila malipo kidogo sana na mara nyingi hawapo serious
Ukichaji bei kubwa unapata clients wachache wenye bei nzuri pia wanakuwa serious na kazi zao. Ni rahisi ku outsource kazi zao ukabaki na pesa
Fanya kazi na team bora, ukimpatia kazi kijana wa chuo anakwambia umpe pesa ya bundle, atakwambia umeme umekata, atakwambia ana tes, au atakaa kimya deadline ikifika anakwa sory nilikuwa bize😅 Tafuta watu professional
Njia nyingine rahisi ni unatafuta clients wako wanaolipa vizuri. Unaingia Fiverr, unachukua freelancer wahindi, na wafilipino wa bei ndogo wanakufanyia kitu kizuri sana.
Tafuta kazi kulingana na niche yako, usikimbilie kila kazi. Mfano mimi nimewafundisha vijana wangu niche ya blockchain. Kwahiyo focus yetu ni kazi za blockchain peke yake.
Hii inatusaidia kupata kazi za pesa nzuri na kujitofautisha na wengine wanaofata mkumbo.
Degree, certificate, website, utaalamu wako hautakuletea wateja / clients hautakusaidia
Focus na marketing, sales, kutafuta wateja. Matokeo yatajionesha
Skills za muhimu ni marketing, sales, offer creation, clients retention, project management
Freelancing ni rahisi sana ukiweza hizo skills