Pesa ya Tanzania inatengenezwa na kampuni gani?

Wakuu naomba mwenye uelewa anieleweshe kuhusu pesa ya Tanzania ya note na coin. Vinatengenezewa wapi. Si mtalaam wa haya mambo.
 
Sijui ila nna uhakika, Inachapishwa na mabeberu, huko kwa mabeberu.

Sijui kwanini hatufungui kiwanda cha noti zetu hapa nchini, tukaajiri watu wetu! Fedha tunazo!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sijui ila nna uhakika, Inachapishwa na mabeberu, huko kwa mabeberu.

Sijui kwanini hatufungui kiwanda cha noti zetu hapa nchini, tukaajiri watu wetu! Fedha tunazo!

Everyday is Saturday............................... 😎
Zimbabwe walitaka kufanya hivyo, kiwanda kikamilika, walivyoomba matilio ya kutengenezea Dolali zao wakanyimwa.
 
Huwa nasikia story za vijiweni kuwa pesa zetu zinatengenezwa benki ya dunia USWISI..Naomba mniweke sawa wakuu.
 
Mkuu, hili la kununua malaya umebonyeza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui ila nna uhakika, Inachapishwa na mabeberu, huko kwa mabeberu.

Sijui kwanini hatufungui kiwanda cha noti zetu hapa nchini, tukaajiri watu wetu! Fedha tunazo!

Everyday is Saturday............................... 😎

Nilisikia zinachapishwa Uswisi
 
Kutengenezwa ni popote pale kwenye kamputi itakayo shinda tenda
Exactly ndiyo ninachojua mimi, inawezekana zinatengenezwa na kampuni mbili au hata 3.. Saa zingine siyo lazima noti zote au fedha zote zitengenezwe na kampuni moja.
Nimeona Waingereza wana branch Kenya.

Utakuta zinachapwa hapo kwa jirani.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Mkuu unauliza maswali yenye akili lakini watu hawajuelewi wanazunguka mbuyu tu
 
Yani ww ni kama unatafuta source ya the last man anayetengeneza pesa. Lakini mtu hashtuki. Ni kama kukuta msitu unaungua unatafuta aliechoma msitu. Mtu anakwambia msitu umeongua kwa sababu majani yalikua makavu. Wewe unamwambia ndio msitu kuungua lazima majani yawe makavu lakini nani aliyechoma msitu. Mtu anakwambia kuchoma msitu mpaka uwe na kiberiti bila kiberiti huwezi choma, si unaona msitu wa zimbabwe chini ya mugabe ulivoungua sababu ya kiberiti na njiti.
Kiufupi unajaribu ku reason na watu ambao hawajui kinachoendelea kwenye uchumi
Sisi kama Tanzania tukiprint pesa zetu na kuita watu kutoka nje kutufanyia kazi na kuwalipa izo pesa kuna tatizo lolote au kuna taasis utatufunga,,,,,, aiseeeee
 

Kenya kuna kiwanda cha kutengeneza pesa zao kipo Nairobi Kampuni inaitwa De La Rue​

28 Nov 2018 — De La Rue, which has operated in Kenya for more than 25 years, says it is investing more in its factory in Ruaraka, Nairobi as part of a long- ...


 
Noti ukiprint nyingi kuliko kiwango sahihi zinashuka thamani, maana zinasambaa sana kwa hiyo bei za vitu zinapanda maana watu wengi wanakuwa na pesa.

Si uliona Zimbabwe kilichotokea?

Tarehe 12/4/2009 Zimbabwe ilisitisha matumizi ya sarafu yake ya Dola ya Zimbabwe (ZWD) na kuruhusu sarafu za kigeni zitumike nchini humo.

Sababu ya kusitisha ni kwamba sarafu hiyo ilishuka thamani kwa kiwango cha kutisha kutokana na Benki Kuu ya Zimbabwe kuchapisha sarafu nyingi sana.

Iliporomoka mpaka kufikia kiwango cha Shilingi moja ya Tanzania kuwa sawa na Dola TRILIONI 26.5 za Zimbabwe.

Kwa hiyo ilikuwa ukitaka kununua mkate wa Tshs. 1,000/- kwa Zimbawe ilibidi uwe na dola TRILIONI 26,500 za Zimbabwe. Ndo kipindi hicho waZimbabwe wanabeba noti kwenye toroli au mkokoteni kwenda kununua mkate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…