Peter Msigwa awaasa watanzania kuenzi mazuri ya Hayati John Pombe Magufuli

Peter Msigwa awaasa watanzania kuenzi mazuri ya Hayati John Pombe Magufuli

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
"Pamoja na mapungufu ya Hayati Magufuli lakini kuna mazuri pia tulipaswa kuyaendeleza mfano nidhamu kazini, uoga kwa mali ya umma na kuheshimu wananchi"

B2689647-1877-452D-9875-1940D965852D.jpeg

Mchungaji Peter Msigwa
Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa

Chanzo: Jambo TV
 
Mama Samia, Rais wetu, nakuomba, viongozi uliowachagua serikalini, ukisikia wanafanya upuuzi au kula rushwa au kunyanyasa wananchi au wana dharau serikali yako, haraka kabisa usiwacheleweshe tumbua haraka sana, wala usisubiri sijui aje ajieleze.. Piga chini haraka sana, maana LABDA AU HUENDA kuna viongozi kibao umewachagua na chini kwa chini wanakusema vibaya sana na wengine wanaisema vibaya kabisa serikali yako.

Mh. Rais wetu, ukisikia tu, sijui Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, RC, RAS, DCs, DAS, DEDs, wakurugenzi wakuu wa taasisi mbalimbali au viongozi wengine uliowachagua ukipata taarifa wanakusema hovyo au wanaisema serikali vibaya chini chini, na ww Mh. Rais wetu wapige chini, kimya kimya, yaani mtu akiamka asubuhi anaona katenguliwa tu, sbb wakati wa unamteua hauja discuss nae, pia wakati wa kumtengua wala usi discuss nae..

I know, binadamu watu wa ajabu sana, kapewa hadi cheo, ila bado atakusema tu, hawaridhiki, wako viongozi wengi huenda/labda wanaisema vibaya au wanadharau serikali kichini chini.. Mh. Rais wetu, ukisikia tu, piga chini haraka paaaap, alafu tunasonga mbele na kazi iendelee
 
Mchungaji Umeongea ukweli kabisa. Magufuli kulikua na nidhamu sana SERikalini.

Mama Anafanya vizuri ila kama hakutakuwa na nidhamu ndani ya SERIKALI Yake Basi kila kitakachokua kinapatikana kutaishia mifukoni mwa wajanja.

Miradi mingi ya Serika sasa inalega lega sio kwa kukosa fedha Bali kukosa usimamizi mzuri wa wasaidizi wa MH Rais.

Mradi wetu mkubwa wa Julius Nyerere ungekua umeshakamilika tangu mwaka Jana sawa sawa na makubaliano na SERIKALI ya Awamu ya 5 ila kwa kukosa usimamizi mzuri wa viongozi mradi haujakamilika.

Niwito Wangu kwa MH Rais kweli Unajitahidi kufanya Vizuri. Lakini kuwa Mkali kwa wasaidizi wako. Nchi zote zilizoendelea hazikuwa na utani na wazembe Katika SERIKALI.
 
Huna akili
 
Back
Top Bottom