Peter Msigwa awaasa watanzania kuenzi mazuri ya Hayati John Pombe Magufuli

Peter Msigwa awaasa watanzania kuenzi mazuri ya Hayati John Pombe Magufuli

Mchungaji Umeongea ukweli kabisa. Magufuli kulikua na nidhamu sana SERikalini.

Mama Anafanya vizuri ila kama hakutakuwa na nidhamu ndani ya SERIKALI Yake Basi kila kitakachokua kinapatikana kutaishia mifukoni mwa wajanja.

Miradi mingi ya Serika sasa inalega lega sio kwa kukosa fedha Bali kukosa usimamizi mzuri wa wasaidizi wa MH Rais.

Mradi wetu mkubwa wa Julius Nyerere ungekua umeshakamilika tangu mwaka Jana sawa sawa na makubaliano na SERIKALI ya Awamu ya 5 ila kwa kukosa usimamizi mzuri wa viongozi mradi haujakamilika.

Niwito Wangu kwa MH Rais kweli Unajitahidi kufanya Vizuri. Lakini kuwa Mkali kwa wasaidizi wako. Nchi zote zilizoendelea hazikuwa na utani na wazembe Katika SERIKALI.
Kweli mkuu .

FB_IMG_1665831491154.jpg
 
Huyo mchungaji wa mchongo hana akili. Huyo mtu hawezi kua mfano kwenye jambo lolote, ni aibu kwa taifa.

Nidhamu ipi, kwenda kukaa Chato miezi sita na kutumia resources za taifa kulipa wasaidizi wake na kufanyia shughuli za serikali kibarazani kwake?

Kununua ndege kama mashati bila kufuata sheria za manunjzi?

Kula hela za plea bargain

Kupoteza 1.5 Trillion

Aache utani, au kwasababu ni baba yake mkwe?
 
Ndani ya mioyo yao wanammisi jamaa. Ila kwakua shetani ameshaingia kwenye vichwa vyao lazima wakane hadharani.

Ni jambo la muda tu sote tutakubaliana kuwa tumepoteza kiongozi mweledi na mzalendo.
 
Mama Samia, Rais wetu, nakuomba, viongozi uliowachagua serikalini, ukisikia wanafanya upuuzi au kula rushwa au kunyanyasa wananchi au wana dharau serikali yako, haraka kabisa usiwacheleweshe tumbua haraka sana, wala usisubiri sijui aje ajieleze.. Piga chini haraka sana, maana LABDA AU HUENDA kuna viongozi kibao umewachagua na chini kwa chini wanakusema vibaya sana na wengine wanaisema vibaya kabisa serikali yako.

Mh. Rais wetu, ukisikia tu, sijui Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, RC, RAS, DCs, DAS, DEDs, wakurugenzi wakuu wa taasisi mbalimbali au viongozi wengine uliowachagua ukipata taarifa wanakusema hovyo au wanaisema serikali vibaya chini chini, na ww Mh. Rais wetu wapige chini, kimya kimya, yaani mtu akiamka asubuhi anaona katenguliwa tu, sbb wakati wa unamteua hauja discuss nae, pia wakati wa kumtengua wala usi discuss nae..

I know, binadamu watu wa ajabu sana, kapewa hadi cheo, ila bado atakusema tu, hawaridhiki, wako viongozi wengi huenda/labda wanaisema vibaya au wanadharau serikali kichini chini.. Mh. Rais wetu, ukisikia tu, piga chini haraka paaaap, alafu tunasonga mbele na kazi iendelee
Uongozi hauendi hivyo hizo sifa anazotaka appointees wake wawe nazo inabidi awe nazo kwanza. Ataishia kuwafukuza hadi achoke. Maafisa chini ya RC, RAS,DED, DAS wanajua hilo.
 
"Pamoja na mapungufu ya Hayati Magufuli lakini kuna mazuri pia tulipaswa kuyaendeleza mfano nidhamu kazini, uoga kwa mali ya umma na kuheshimu wananchi"

View attachment 2549519

Mchungaji Peter Msigwa
Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa

Chanzo: Jambo TV
Taratibu mnakubali, mwisho wa siku tukishafika kwenye kilele cha shimo la sewa mtaenda Burigi kuomba afufuke.
 
Ni sawa, Msigwa yupo sahihi.

Uzembe kwenye taasisi za serikali umerudi tena, wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi, wameshajua mama yao anaongea sana, vitendo vichache.
upuuzi umerudi kwa kasi kila kona.yajayo yanasikitisha.
 
Mama Samia, Rais wetu, nakuomba, viongozi uliowachagua serikalini, ukisikia wanafanya upuuzi au kula rushwa au kunyanyasa wananchi au wana dharau serikali yako, haraka kabisa usiwacheleweshe tumbua haraka sana, wala usisubiri sijui aje ajieleze.. Piga chini haraka sana, maana LABDA AU HUENDA kuna viongozi kibao umewachagua na chini kwa chini wanakusema vibaya sana na wengine wanaisema vibaya kabisa serikali yako.

Mh. Rais wetu, ukisikia tu, sijui Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, RC, RAS, DCs, DAS, DEDs, wakurugenzi wakuu wa taasisi mbalimbali au viongozi wengine uliowachagua ukipata taarifa wanakusema hovyo au wanaisema serikali vibaya chini chini, na ww Mh. Rais wetu wapige chini, kimya kimya, yaani mtu akiamka asubuhi anaona katenguliwa tu, sbb wakati wa unamteua hauja discuss nae, pia wakati wa kumtengua wala usi discuss nae..

I know, binadamu watu wa ajabu sana, kapewa hadi cheo, ila bado atakusema tu, hawaridhiki, wako viongozi wengi huenda/labda wanaisema vibaya au wanadharau serikali kichini chini.. Mh. Rais wetu, ukisikia tu, piga chini haraka paaaap, alafu tunasonga mbele na kazi iendeleeguts
hizo guts atazitoa wapi?nchi sasa ni holela kila mtu anaenda ajuavyo,rubani katanglia.
 
Back
Top Bottom