Peter Msigwa: Baada ya mauaji ya Oktoba 29 na ukiukwaji wa haki unaoendelea, siwezi tena kubaki CCM, nimeamua kurejea CHADEMA

Ni afadhali umwamini shetani kuliko mwanasiasa...
 
Kumrudisha mtu kama huyu ambae kamwaga upupu mwingi sana alipoondoka Chadema. Maana anaweza kurudi kama mamluki, akawa anatoa siri za Chama kwa watekaji. Tunavunjana moyo, Chama kiwe na msimamo na kisonge mbele cause kimepitia magumu hakuwepo na kinaendelea kupambana bila yeye. Aende Chauma bhana.
 
Siasa za chama ni Idadi ya watu na ubora. Hawa watarudi wengi chadema imerudi kwenye chati mno mwanasiasa huangalia wapi ambako hatapoteza umaarufu wake. CCM siyo jahazi zuri kwao kisiasa, chadema itabeba wengi sana.
 
Karibu tena mheshimiwa Msigwa. Ni kweli binadamu tunakosea. Ni jambo la kiungwana sana kukubali makosa na kujirudi.
Watu ambao hatutawasamehe ni viongozi wa CCM, baadhi ya majaji, watu wa tume fake ya uchaguzi, baadhi ya mapolisi, baadhi ya maafisa wa usalama wa taifa, etc. Hao ndo mastermind wa vurugu na mateso mengi sana ambayo CHADEMA tunapitia.
 
Amerudi na mikakati mipya na nguvu mpya rafiki zake akina Lema Heche watakuwa wamefurahi. wanaorudi ni vile Mbowe hayupo kwenye uongozi. wote hawa walipishana na Mbowe
 
Kijiweka kundi moja na wauwaji yataka moyo katili na wa chuma.
Ni kweli kabisa. Huwa nashangaa sana sana eti baadhi ya viongozi wa dini wako kundi moja na wauaji. Yaani sijui kwenye nyumba zao za ibada wanahubiri nini!
 
Wamemrudisha Selasini na leo Msigwa. Tukiwaambia demokrasia ni upotezaji wa muda hamuelewi.
 

Na Chadema mnamuamini huyo kinyonga wa CCM?
 
Ni kweli kabisa. Huwa nashangaa sana sana eti baadhi ya viongozi wa dini wako kundi moja na wauaji. Yaani sijui kwenye nyumba zao za ibada wanahubiri nini!
ndugu yangu viongozi wa misikiti na makanisa wanafanya ubakaji ndani ya nyumba za ibada, sembuse la kuwa wanafiki? Lishike analokufundisha madhabahuni kama ni jema, usiangalie matendo yake.
 
Mauaji Oktoba 29, 2025. Machungu na kuhama chama May 23, 2026.

Mchungaji ni mvumilivu sana wallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…