Watu wametafuta namna ya kujipa comfort
Wametengeneza uzembe tegemezi kwa kuendekeza mawazo waliyo jitengenezea kichwani wakiamini huko angani kuna jamaa mwenye midevu na nguo nyeupe
Jamaa ambaye muda wote hana kazi ya kufanya zaidi ya kuangalia nani kafanya dhambi nani hajafanya dhambi
Watu wamejikuta wakiwa watumwa kwa mawazo yao na kudhani jamaa huyo ili kumridhisha inabidi ukae na njaa (wanaita mfungo) utoe pesa (wanaita sadaka)
Halafu ikitokea kitu unacho wish hakijaenda ulivyotaka, hapo itahesabika kama jamaa anajibu maombi kwa wakati wake kwa hiyo uwe mpole
Ikitokea umefanya juhudi zako jambo likafanikiwa basi hapo itahesabika jamaa kajibu maombi yako
Ukiumwa, ni mpinzani wa huyo jamaa ambaye ana sifa ya mapembe na kila kitu kibaya kuwa anakujaribu
Unatakiwa umuombe jamaa mwenye uchebe aliyevalua nguo nyeupe ili akuepushe na mchizi mwenye pembe
Ikitokea umeomba na ukafa, basi huku tutasema jamaa mwenye uchebe na mavazi meupe alikupenda zaidi japokuwa mwanzo tulikuwa tunsmpa lawama mpinzani wake