Kwa hiyo kwako hoja yenye nguvu haiwi challenged?
Ikiwa nanguvu kwako, basi inapaswa kuchukuliwa hivyo hivyo na kwa mwingine bila kuhojiwa kujua uhalali wake?
Hujui pia kuna kanuni za ku verify majibu, na hizo kanuni haziwezi kuja kwa namna nyingine ikiwa ni pamoja na kuhoji?
Ebu fikiria kama ndo mkristo anataka akupe hoja yenye ushawishi ya kukufanya wewe muislamu uamini Yesu alibatizwa na pia ni njia ya kweli ya uzima, ambayo ina lengo la kukufanya uokoke
Akakupa hoja ya maandiko ya biblia yanayozungumza ubatizo wa yesu uliofanywa na yohana mbatizaji ikiwa hiyo ndio hoja kuu anayoamini kua ina nguvu, utakubali aina hiyo ya uthibitisho?
Utaokoka?
Bila shaka utahitaji maelezo zaidi ya hicho alichokiandika japokuwa alisema ni hoja yenye nguvu, kumbe "hoja yenye nguvu" ni another fallacy yenye kulazimisha mtu akubali hoja fulani bila kohoji
Kwa hiyo jambo la busara ni wewe kuweka hiyo hoja kisha tutaichambua kuona authentic yake na hapo ndipo tutaweza kuhitimisha kua hoja hiyo ni bora