Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu

Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu

Kama nimekuzushia naomba twende taratibu wala tusibishane kitoto

Umependekeza hoja ya kutumia aya za kitabu

Hizo aya ndio kwanza naziona hapa

Ili kujihakikishia naomba unithibitishie ukweli wake ili niwe na uhakika kwamba na dili na source ya namna gani
Hizo aya zipo katika sura ya 52 katika Qur'aan. Inaonekana hata Qur'aan hujui kuisoma, jf kuna vituko sana.

Sasa unaomba uthibitishiwe ukweli kwamba ni Qur'aan au ukweli vipi ?

Hivi unajua kuisoma hiyo Qur'aan au tafuta tarjama yoyote ambayo ipo karibu yako, tafuta sura namba 52 katika aya kuanzia 34 mpaka 36.
 
Personal attacks za nini
Hakuna personal attack hapo sababu sijatoka nje ya mada.
hoja 2&3 haina maelezo extra kama ambavyo wewe unadai, ili hoja iwe hivyo kama unavyosema ilipaswa iwe na lead na sio conclusion
Hii siyo kweli tofauti na nyinyi katika elimu ya logic mna tatizo kubwa sana la namna ya ufikiaji wa hitimisho.

Namba mbili na tatu si kweli kama unavyo dai sababu watu tunajifunza imani, tunahoji, tunafikiri na tunafanya utafiti. Wewe umerukia hitimisho kabla ya kuangalia imekuwaje tumefikia huko, huu ni udhaifu wenu na si wewe wa kwanza bali walio kutangulia wamekufikisheni huko.
Sasa hoja ina conclusion, na wewe ulichokielezea ni lead mpaka hapo unakuwa unaelezea kitu kingine tofauti na nilicho kizungumzia mimi
Wewe si ulitaka hoja ikufikishe kwenye hitimisho ukadai ya kuwa namba 2 na 3 zimehitimisha, sasa ni uongo wako ulio kufanya usiulize maswali ya msingi sababu majibu yake yako wazi. Kijana unatakiwa usome tena usome hasa ukienda kwa mtindo huu hutaweza kujenga hoja yenye mashiko hata jwa bahati mbaya sababu laiti kama ungesoma usingepoteza muda kuandika mada nyepesi kama hii, sababu katika kusoma kwako ungekutana na majibu humo humo,ndiyo maana mimi nakushangaa yaani unayo yaandika ni tofauti na tuliyo nayo sisi.
 
Usiseme Qur'aan nyingine sema ikusanywe sehemu moja na iwe kitabu pweke sababu mpaka Mtume anafariki ilikuwa imeshakamilika. Rejea kitabu "Al-Itiqaan fi Ulumil al Qur'aan" cha Imam Suyuti.

Swahaba alihofia akaamuru hilo, ikusanywe na iwekwe kwenye kitabu. Siyo "Yomama" sahihi ni "Yamamah"
Ilikuwa imekamilika ikiwa na jumla ya chapter nagapi?

Kama ilikuwa imekamilika kwanini tena Zayd ibn Thabit alipewa kibarua cha kutafuta collection ya maneno yaliyo miss?

Baada ya vita ya Yamama Quran ilikuwa katika hali gani?

Hicho kitabu ulichoni recommend kimeeleza hayo page number ngapi?
 
Huu uandishi wako una mapengo sana inaonekana ulienda kugoogle hivi punde, yaani hapo kabla hukusoma kabisa ndiyo maana unakosea sana. Kwanza walikuwepo wengi walio hifadhi Qur'aan nzima, iliandikwa kwenye makaratasi. Huko maporini ni mapori gani hayo aliyo enda Swahaba wakati ardhi ya huko ni Jangwa ?
Walio hifadhi kuran nzima wote walikuwa wamekufa kwenye vita ya yamama na ndio sababu Umar kupatwa na hofu kua kuna hatari kubwa inayoweza kutokea kwamba sehemu kubwa ya Quran isipatikane

Watu waliokuwepo katika hicho kipindi walikuwa na nukuu chache sana walizo hifadhi kichwani ambazo hazikuweza kutosha kuifanya ikamilike na ndio maana ikambidi Zayd kutafuta sehemu nyingine nje na hapo
 
Si kweli, inaonekana hujasoma mpaka mwisho huko ulipo soma. Nakuuliza wewe swali, swahaba Abuu Bakr alikamilisha hilo zoezi lini na alilianza lini ? Usiseme miaka mingi kupita.
Kwa hiyo unataka kusema sio kweli kwamba hii Quran ya sasa haikuwa compiled?

Abu Bakri alitoa delegation kwa watu 12 wakamilishe huo mchakato wa kuokoteza okoteza aya zilizo andikwa sehemu tofauti tofauti ambapo pamoja na hayo yote kufanyika bado wanazuoni wa kale walisema Quran hiyo ni incomplete kuna gape kubwa la chapters hazijawekwa ikifananishwa na mwanzo

Lakini pia wapo walio argue kuwa kulikuwa na contents zilizoongezwa ambazo hazikuwepo kwenye Quran ya mwanzo

Kuhusu mwaka gani sijajua
 
Ilikuwa imekamilika ikiwa na jumla ya chapter nagapi?

Kama ilikuwa imekamilika kwanini tena Zayd ibn Thabit alipewa kibarua cha kutafuta collection ya maneno yaliyo miss?

Baada ya vita ya Yamama Quran ilikuwa katika hali gani?

Hicho kitabu ulichoni recommend kimeeleza hayo page number ngapi?
Kwanza jifunze kujibu swali unalo ulizwa kwanza kabla ya wewe kuuliza maswali yako.

1. Qur'aan ina sura 114 tangu ilipokamilika mpaka sasa.

2. Zayd Ibn Thabit alipewa kazi ya kuikusanya pamoja iwe kwenye nakala moja. Kwahiyo kukamilika ilikuwa imakamilika maswahaba walikuwa wameihifadhi vifuani, wamiandika kwenye sehemu kadha wa kadha.

3. Qur'aan ilikuwepo, kilicho hofiwa na Swahaba mtukufu Abu Bakr ni kile kitendo cha kuuliwa kwa wale Mahufadhi (Walio hifadhi) kingekuja kuleta mtihani baadae, likatoka wazo la kukusanywa. Baada ya kukamilika hiyo nakala akawa nayo Swahaba Abuu Bakr, kisha akampa swahaba Umari ile nakala, swahaba Umar kabla hajafa alimkabidhi nakala ile mwanae aliye itwa Hafswa, kisha likaja wazo toma kwa swahaba Hudhaifa al Yamani, ya kwamba iandikwe Qur'aan kudhibiti lahaja zote saba zilizo tumika kuteremka kwayo Qur'aan, kisha zikaandikwa bakala tano zikasambazwa katika miji mitano ya Waislamu nayo ni Makka, Madina, Sham, Kufa na Basra.

4. Rejea tu katika yaliyomo kwenye kwenye kipengele kinacholelezea historia ya ukasanywaji wa Qur'aan.
 
Walio hifadhi kuran nzima wote walikuwa wamekufa kwenye vita ya yamama na ndio sababu Umar kupatwa na hofu kua kuna hatari kubwa inayoweza kutokea kwamba sehemu kubwa ya Quran isipatikane
Hawakufa wote kijana kasome tena historia. Hakuwa Umar ni swahaba Abu Bakr.

Nakuja kuendelea hapa nilipo ishia.
 
Hili hakuna msomi wa dini anae pinga, swali la uongo ni hayo madai yako unayoyaleta kwamba sehemu kubwa haikupatikana, naomba ututhibitishie hili sababu kila kitu kimehifadhiwa. Yaani unavyo andika unaonekana huijui Historia ya ukisanywaji wa Qur'aan. Hapa itabidi ujibu maswali nayo kuuliza.

Hapo mwanzo nilikutahadharisha kwamba ukianzisha mada hakikisha unaiweza mada husika.

Yaani sisi mpaka kesho haya tunafundishwa na tunayajua ila hili la wewe kudai kwamba kuna sehemu kubwa haijapatikana ndiyo unatakiwa kuthibitisha.
Nimekutajia hapo jina la huyo mwanazuoni wa As-Suyuti kale na Quote yake pia nimekuwekea, una bisha nini sasa?

Ni kwamba sio kweli kua hajawahi kutoa maneno kama hayo?
 
Kuna hoja ya kuthibitisha uwepo wa Mungu, hoja ambayo imeegemea zaidi katika kutumia vitabu vya dini kama uthibitisho

Ni hoja ambayo ime base kwenye imani ya kusema Mungu amejidhihirisha uwepo wake kwa binadamu kupitia uumbaji au maandiko matakatifu.

Watu wamekua waki experience hayo maandishi kua yametoka moja kwa moja kwa mungu na kupitia experience hiyo wengi wanaamini kuwa wanawasiliana na Mungu directly.

Hiyo ni hoja ya kutoka kwenye ufunuo (argument from revelation) ambayo huusisha maandiko matakatifu (sacred text)

Kwamba
  • Imekuwa inspired na Mungu
  • Imeamuriwa na Mungu
  • Imeandikwa na kuongozwa na Mungu

Msingi wa hoja hii

  1. . Maandiko yanasema Mungu yupo (Quran)
  2. . Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au watu walio ongozwa
  3. . Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu ndio alifanya hiyo kazi)
  4. . Mungu ndio chanzo na dhamana ya ukweli

HITIMISHO: Mungu yupo

**************
Hoja au uthibitisho wa namna hiyo haukubaliki na rational thinkers kwasababu una makando kando mengi (flaws) kuna matobo kibao kwenye hii raft ambayo umeitumia kujenga hoja yako

Tatizo la kwanza la hoja hii ni

LOGICAL PROBLEM OF FALLACY CIRCULAR ARGUMENT
Hii ni hoja ambayo inatumia assumption kwa kile inachotaka kuthibitisha na hii huchukuliwa kama moja ya hoja za kijinga na zenye udhaifu sana miongoni mwa hoja zinazojaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu

Ukiangalia hiyo misingi ya hoja hizi niliyoiweka hapo juu, namba 2 na namba 3 utaona zime contain hitimisho ndani yake

Hoja ilipaswa ikuongoze mpaka ikufikishe kwenye hitimisho na sio ku assume hitimisho ndani ya msingi wa hoja hiyo hiyo.

Kwasababu lazima ukubali kuwa kitabu hicho kimetoka kwa Mungu ili ukikubali kuwa ni cha kweli na sahihi kisha ukisha kikubali kuwa ni cha kweli na sahihi ukasoma ndani yake kuwa kuna Mungu na hivyo kuhitimisha kuwa kuna Mungu na huyo ndiye. Hicho ndicho ulichohitaji kufikiria ili kukubali kitabu hicho kuwa cha kweli na sahihi hapo awali.

Hii Circular Reasoning ya namna hii haiwezi kumshawishi rational ambaye yeye sio muumini wa Miungu/Mungu

ambulika kua ni maandiko ya kweli zaidi?
However, there are times when we should follow the path in order for God to manifest in our life.

dis.jpeg
 
Kwa hiyo unataka kusema sio kweli kwamba hii Quran ya sasa haikuwa compiled?

Abu Bakri alitoa delegation kwa watu 12 wakamilishe huo mchakato wa kuokoteza okoteza aya zilizo andikwa sehemu tofauti tofauti ambapo pamoja na hayo yote kufanyika bado wanazuoni wa kale walisema Quran hiyo ni incomplete kuna gape kubwa la chapters hazijawekwa ikifananishwa na mwanzo

Lakini pia wapo walio argue kuwa kulikuwa na contents zilizoongezwa ambazo hazikuwepo kwenye Quran ya mwanzo

Kuhusu mwaka gani sijajua
Wakina nani hao wataje walio argue.

Kuhusu mwaka unatakiwa ufatilie.
 
Nimekutajia hapo jina la huyo mwanazuoni wa As-Suyuti kale na Quote yake pia nimekuwekea, una bisha nini sasa?

Ni kwamba sio kweli kua hajawahi kutoa maneno kama hayo?
Unatakiwa useme hiyo Quote inapatikana katika kitabu, usilete kona kona.

Usiniulize swali hilo, mimi nataka unipeleke huko tanako patikana hayo maneno.
 
Imamu Suyuti ni wanazuoni mkubwa sana na tunamkubali na kumuheshimu sana, haya maneno tunayapata wapi yaani kayasema wapi ?

Haya maneno umeyatoa wapi mbona unaandika kama habari za vijiweni ? Tuwekee matrejeo.
Al-Suyuty, Al-Azhareyyah Press, Cairo, Egypt, 1318 AH, Page 59

1646419552949.png
 
Hizo aya zipo katika sura ya 52 katika Qur'aan. Inaonekana hata Qur'aan hujui kuisoma, jf kuna vituko sana.

Sasa unaomba uthibitishiwe ukweli kwamba ni Qur'aan au ukweli vipi ?

Hivi unajua kuisoma hiyo Qur'aan au tafuta tarjama yoyote ambayo ipo karibu yako, tafuta sura namba 52 katika aya kuanzia 34 mpaka 36.
Quran version gani?

Ya 1924 ya kimisri iliyokuwa edited na Iman Hafs?

Au ya Imam Warsh's ambayo inatumika sana north africa?
 
Hakuna personal attack hapo sababu sijatoka nje ya mada.

Hii siyo kweli tofauti na nyinyi katika elimu ya logic mna tatizo kubwa sana la namna ya ufikiaji wa hitimisho.

Namba mbili na tatu si kweli kama unavyo dai sababu watu tunajifunza imani, tunahoji, tunafikiri na tunafanya utafiti. Wewe umerukia hitimisho kabla ya kuangalia imekuwaje tumefikia huko, huu ni udhaifu wenu na si wewe wa kwanza bali walio kutangulia wamekufikisheni huko.

Wewe si ulitaka hoja ikufikishe kwenye hitimisho ukadai ya kuwa namba 2 na 3 zimehitimisha, sasa ni uongo wako ulio kufanya usiulize maswali ya msingi sababu majibu yake yako wazi. Kijana unatakiwa usome tena usome hasa ukienda kwa mtindo huu hutaweza kujenga hoja yenye mashiko hata jwa bahati mbaya sababu laiti kama ungesoma usingepoteza muda kuandika mada nyepesi kama hii, sababu katika kusoma kwako ungekutana na majibu humo humo,ndiyo maana mimi nakushangaa yaani unayo yaandika ni tofauti na tuliyo nayo sisi.
Mkristo anaweza aka formulate hoja kwa mtindo huo huo

Akaweka assertion hapo kwenye Mungu akamuweka Yesu na akasema tayari kasha thibitisha Yesu alibatizwa na ndio njia ya kweli ya uzima, huwezi kuiona pepo bila kupitia yeye

Akaweka msingi wake wa hoja, kama ule ule uliotumika kwenye Mungu
  1. Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au watu walio ongozwa
  2. . Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu ndio alifanya hiyo kazi)
Halafu aka conclude kua kwa vigezo hivyo basi ni kweli Yesu ndio njia ya kweli na uzima

Utakubali?

Utapinga richa ya kwamba katumia principle ile ile uliyoikubali kwenye hoja nyingine kwasababu hoja ya mara ya pili inaenda kinyume na mafundisho yako?
 
Kwanza jifunze kujibu swali unalo ulizwa kwanza kabla ya wewe kuuliza maswali yako.

1. Qur'aan ina sura 114 tangu ilipokamilika mpaka sasa.
Ilipokamilika tangu muda gani?
 
2. Zayd Ibn Thabit alipewa kazi ya kuikusanya pamoja iwe kwenye nakala moja. Kwahiyo kukamilika ilikuwa imakamilika maswahaba walikuwa wameihifadhi vifuani, wamiandika kwenye sehemu kadha wa kadha.
Alikuwa akiikusanya kutoka wapi?

Sio kweli kua watu waliifadhi kifuani, bali waliokuwepo currently walikuwa wameifadhi aya chache kifuani ambazo hazikuweza kutosha kukamilika

Waliodaiwa kuifadhi Quran kifuani walikuwa wamekwisha uliwa kwenye vita ya Yamama
 
3. Qur'aan ilikuwepo, kilicho hofiwa na Swahaba mtukufu Abu Bakr ni kile kitendo cha kuuliwa kwa wale Mahufadhi (Walio hifadhi) kingekuja kuleta mtihani baadae, likatoka wazo la kukusanywa. Baada ya kukamilika hiyo nakala akawa nayo Swahaba Abuu Bakr, kisha akampa swahaba Umari ile nakala, swahaba Umar kabla hajafa alimkabidhi nakala ile mwanae aliye itwa Hafswa, kisha likaja wazo toma kwa swahaba Hudhaifa al Yamani, ya kwamba iandikwe Qur'aan kudhibiti lahaja zote saba zilizo tumika kuteremka kwayo Qur'aan, kisha zikaandikwa bakala tano zikasambazwa katika miji mitano ya Waislamu nayo ni Makka, Madina, Sham, Kufa na Basra.

4. Rejea tu katika yaliyomo kwenye kwenye kipengele kinacholelezea historia ya ukasanywaji wa Qur'aan.
Quran ilikuwepo wapi?

Kwanini likatoka wazo la kukusanya wakati ilikuwepo?
 
Back
Top Bottom