mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,734
- 1,616
Na hilo jumba refu linalojengwa (hii picha ya muda kidogo, sasa hivi limekwisha jengwa) ndiyo kwetu nilipozaliwa.
Mimi na TANU tuna historia ndefu sana, si wengi wanaoweza kutamba kuzaliwa hapo jirani na palipozaliwa TANU. Nyerere binafsi yake akija kununuwa sigara "karata" dukani kwetu halafu baadae akabadili akija mtu kumnunulia sigara SENATE.
Jembepori,mzee ndiyo maana nime appreciate hii ya leo....
big up
Mpitanjia,Kwani yeye ndio cameraman? Acheni wivu wa kipumbavu.
Mohammed Said,
Historia ya Tanu inafanana kabisa ya historia ya chama ya CNDD FDD.
Chama ya CNDD kilikuwa kunabebwa na waislam(waswalihi) wakiongozwa na Hussein Radjabu, Mohammed Rukara alikuwa mwakilishi wa Muslim CongressTanzania , Karenga Ramadhani (BBC) na wengine wengi.
Propaganda na michango mingi ilikuwa inafanyiwa na inatoka misikitini katika miji ya Bujumbura, Gitega, Muyinga na Ngozi.
Same thing kilichotokea kwa wazee wetu wa Dar. Ndiocho kilichotokea kwa waswahili wa Burundi.
Baada ya kuapishwa Bwana Nkurinzinza akawaondoa wote na wengine akawapa kesi.
----------
Wito wangu ni uendelee na jitihada za kuelimisha jamii kuhusu mchango wa waislam katika ukombozi wa taifa hili.
Jembepori,
Ngoja nikufungulie mikoba.
Hii historia ya TANU ilianza kuandikwa mara tu baada ya uhuru na
wazo hilo lilikuwa la Dossa, Nyerere na Abdul.
Jukumu hilo alipewa Abdul kwa kuwa yeye ndiye anajua mengi katika
yale yaliyopitikana katika African Association khasa kwa kuwa baba yake
alikuwa mmoja wa waasisi.
Dr. Wilbard Klerruu akapewa kazi ya kumsaidia Abdul kukamilisha
kazi hiyo.
Kazi hii haikukamilika kwa kuwa inaelekea Abdul na Nyerere bahati
mbaya hawakukubaliana katika baadhi ya mambo.
Abdul akajitoa katika kazi ile lakini Klerruu aliikamilisha mswada lakini
haukuchapwa.
Sasa historia ya TANU ilipokuja kuandikwa na Chuo Cha Kivukoni majina
ya Abdul na Ally yakaondolewa pamoja na ya wazalendo wengine.
Historia ya TANU ikaanza na Nyerere na kumalizikia na Nyerere.
Jembepori,
Sasa labda na mimi nikuulize.
Kufutwa kwa historia hii ya TANU ya akina Abdul Sykes na Baraza la
Wazee wa TANU la akina Sheikh Suleiman Takadir na Mzee Idd
Tulio ndiyo kuepuka udini?
Ikiwa tutawafuta Waislam kama Ali Msham katika historia ya uhuru
ndiyo tutaepukana na udini?
Jembepori,
Hayo maswali umeyaelekeza sipo. Yanafaa uwaulize wahusika. Mimi imenitosha kuwa nimeandika historia ya wazee wangu na ndiyo hizi darsa ninazosomesha hapa Majlis. Historia ya Magogoni ipo ila kitabu hakijachapwa kwa miaka mingi. Maktaba ya CCM Dodoma wanayo nakala. Waislam wazee wetu hawakuwa wanyonge ila ni wastaarabu. Ukitaka kujua ushujaa wao soma hii historia niliyoandika na soma pia vipi walivyomkabili Mjerumani katika Vita Vya Majimaji.
Sasa mkuu Mohammed umeenda mbali na hili swala la vita vya majimaji nlishalijibu kwqni ulishawahi kulileta nalo................
ninachotaka kusemq ni kwamba wazee wa kiislam hawakuwa wanyonge kama mnavyojitahid kuonyesha na hakuna msitaarabu atakayeendekeza maswala ya kibaguzi hata ukiwa wa kidini..........
hapo tunakubaliana sawa kwani naamini wakati wakipigana na wajerumani pia wlishirikuana na makafiri wasio na dini kama akina kinjekitile ngwale...........
sidhan kama hata walikuwa wanawaza uislqm wakati wanapambana ndani ya mapigano ya majimaji.........
mkuu nachotaka tukubaliane ni kwamba hii ni nchi yetu sote na kama kuna watu waliwahi kukaa dar enzi za ukoloni kama wazazi wenu kama mnavyodai ila pia walihamia kutoka mahala kama kilwa, zanzibar,morogoro na kwingineko, kifupi wote ni wa kuja na hata kama ni mzawa original basi ilikuwa ni bahati tuu......
hiyo haimpi mtu kuwa daraja lq kwanza ndaji ya tanzania maana mnavyosimulia ni kama vile wakristu hawafai kuwepo dar yan hata hili jina lipo kwenye quran (nilisoma nukuu za faizafoxy)...........
hii si sawa hata kidogo na mimi naamini ndiyo maana hata Mungu kuamua kumsaidia mtu kutoka interior aje navkufanikisha uhuru wa mtanganyika kwani kwa story hizi sipati picha kama nyinyi na wazazi wenu ndo mgepata uhuru wa tanganyika na hizi roho za kibaguzi ijui ingekuwaje............
mi nitaendelea kujibu hoja kwa kadri ya ufaham na maarifa niliyonayo kila itakapoibuka ili kuweka sawa kwani wa kale wakipata kusema hata uongo ukisemwa saaana mwisjowe huwa ukweli..........
wasalaam.
Jembepori,
Kitabu changu kizima kimejaa ushujaa.
Sijui hii lugha ya unyonge umetoa wapi.
Soma kitabu cha Abdul Sykes usijadili rsomo hulijui.
Ndiyo haya matatizo.
Huna uwezo wa kutoa majibu kwa historia hii ninayosomesha hapa.
Wenzako wamejaribu wameshindwa sihitaji hapa kukueleza mengine.
TUKIFUTA HII HISTORIA YA WAZEE WANGU TUKABAKISHA YA KIVUKONI
NDIYO HISTORIA YA UHURU ITAKUWA HAINA UDINI?
By Mohamed Said
Jembepori,
Ngoja nikufungulie mikoba.
Hii historia ya TANU ilianza kuandikwa mara tu baada ya uhuru na
wazo hilo lilikuwa la Dossa, Nyerere, Abdul na Mwalimu Kihere.
Habari hizi alinieleza Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi.
Jukumu hilo alipewa Abdul kwa kuwa yeye ndiye anajua mengi katika
yale yaliyopitikana katika African Association khasa kwa kuwa baba yake
alikuwa mmoja wa waasisi.
Dr. Wilbard Klerruu akapewa kazi ya kumsaidia Abdul kukamilisha
kazi hiyo.
Kazi hii haikukamilika kwa kuwa inaelekea Abdul na Nyerere bahati
mbaya hawakukubaliana katika baadhi ya mambo.
Abdul akajitoa katika kazi ile lakini Klerruu aliikamilisha mswada lakini
haukuchapwa.
Sasa historia ya TANU ilipokuja kuandikwa na Chuo Cha Kivukoni majina
ya Abdul na Ally yakaondolewa pamoja na ya wazalendo wengine.
Historia ya TANU ikaanza na Nyerere na kumalizikia na Nyerere.
Jembepori,
Sasa labda na mimi nikuulize.
Kufutwa kwa historia hii ya TANU ya akina Abdul Sykes na Baraza la
Wazee wa TANU la akina Sheikh Suleiman Takadir na Mzee Idd
Tulio ndiyo kuepuka udini?
Ikiwa tutawafuta Waislam kama Ali Msham katika historia ya uhuru
ndiyo tutaepukana na udini?
Naishangaa Serikali kukataza vikundi vya ulinzi vya vyama, kumbr TANU ilikuwa na vijana wa Bantu Group?
kwa hiyo historia ya magogoni yenyewe haina waislam ni wakristo tuu?....
Tena Bantu group wanaonekana walikua wanabeba mashoka eneo la tukio.
Hili swali ni zito sana.
Je walitajwa wakristo na wasio na dini tu katika historia ya kivukoni?
Yeye atakwambia "wazee wake" walisahaulika, na anandika historia ya wazee wake.
Huyu bwana anatumia mlango huu wa kuandika historia ya wazee wake, kutimiza nia yake ya kufarakanisha jamii huku akifikiri anawaunganisha waislam kwa ujumla wao kwa kuwafanya wawe na chuki ya pamoja dhidi ya Nyerere na ukristo. Na ana sababu yake iliyojengeka kwenye kisasi, mdingi wake ambaye alikuwa kwenye AMNUT alishughulikiwa na serikali. Lakini badala ya kuilaumu serikali kwa ujumla, anamlaumu Nyerere na ukristo. Ila hali kama hiyo ikitokea wakati Rais ni muislam, lawama haziendi kwa Rais, bali zinaenda kwa serikali inayoongozwa na anachokiita christian lobby au mfumo kristo. He is a man on a mission...
Nanren,
Unajitisha bure na unataka kuwatisha watu wengine bila sababu.
Sijapata kuona swali gumu hapa Majlis.
Ikiwa swali nalijua nalijibu silijui nasema hilo silijui.
Ikiwa "mdingi" umemkusudia ni babu yangu Salum Abdallah yeye
alikuwa TAA kisha TANU toka mwanzo na mwaka 1955 aliasisi
Tanganyika Railway African Union (TRAU).
Hakupatapo kuwa AMNUT na kweli alishughulikiwa mwaka wa 1964
baada ya maasi ya wanajeshi yeye na viongozi wengine wa vyama
vya wafanyakazi waliwekwa kizuizini.
Ukitaka kujua kisa cha yeye kuwekwa kizuizini nitakueleza.
We sema tu.
Ni historia kama hizi ndizo zinazonifanya kuwa mjuzi wa historia
ya Tanganyika.
Iko siku nitakuwekeeni hapa Majlis yaliyopitikana ndani ya jela ya
Uyui, Tabora alikozuiwa babu yangu kati ya 1964 - 1965.
Bwana Jela alikuwa Mzee Munthali na Mkuu wa Mkoa Tabora
alikuwa Rashid Kheri Baghdelleh.
Hawa wote wakifahamiana vizuri sana na baba yangu.
Kwa ajili hii habari nitakazowawekea hapa ni kutoka "kinywa cha
farasi."
Habari zinatoka kwa Munthali kuja kwa baba yangu.
Habari zinatoka kwa Baghdelleh kuja kwa baba yangu.
Kutoka kwa hao wawili ndipo nilipozipokea mimi.
Unauona huo upokezi?
Sikuishia hapo.
Nimepokea habari nyingine kutoka kwa Bilal Rehani Waikela
aliyekuwa kizuizini na babu yangu.
Waikela na babu yangu wote walikuwa mstari wa mbele kupambana
na ukoloni.
Hayo mengine uliyoandika sioni sababu ya kuyasemea.
Nanren,
Zimenifikia taarifa hivi punde kuwa gazeti la Raia Mwema la leo tarehe
6 May 2015 wamechapa makala ya Mtemvu ambayo iko hapa Majlis.
Wakati wewe unajitisha na historia hii ya TANU leo kuna magazeti
yanaingia katika blog yangu na wakikuta kitu cha manufaa wanakichapa.
sawa mkuu mi nimekupata ila swali langu ni hivi wewe kwenye hiyo historia ya kivukoni hujawahi ona hata jina la muislam mmoja angalau ukamwelezea kwa positive.......
yan ni nyerere tuuuu mwanzo mwisho?.....
Jembepori,
Hivi unatambua kwa nini mimi niliandika kitabu cha historia ya TANU ilhali
historia hiyo ilishaandikwa na Chuo Cha Kivukoni?
Jembepori,
Hebu soma kitabu kwanza.