Picha aliyoposti Makonda siku moja baada ya Mahakama kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani

Picha aliyoposti Makonda siku moja baada ya Mahakama kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije, Makonda amepost picha kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akiwa na darubini.

Katika kesi hiyo, Saed Kubenea anaomba kuweza kumshtaki Paul Makonda, hata hivyo Makonda hajaonekana Mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Machi 2, 2022.

Makonda amepost picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram lakini hajaandika chochote.

Makonda.JPG
 
Siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije, Makonda amepost picha kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akiwa na darubini...
Kama kuna kamhimili ka kichina vile
 
Siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije, Makonda amepost picha kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akiwa na darubini.
...
😂
Kuna mtu anam-zoom tu..
Kifuatacho ni kutekwa !
 
Ni siku kadhaa sasa imeripotiwa kua aliekua RC wa Dar,ndugu Makonda anatafutwa,jambo ambalo wengi wanaona ni maigizo,itiliwe maanani yule bwana haishi kupost kwenye mtandao.

Mara kadhaa imeripotiwa polisi ana TCRA kuhusika kuwakamata watumiaji wa mitandao ambao waliwahi kutoa maoni tofauti na kupewa makosa ya uchochezi,kwa nini Makonda tunaambiwa hapatikani huku anapost kwenye akaunti yake?!! Je ni kweli dola haijui alipo?!!

Mathalani,picha ambatanishi ameipost muda mchache,wataalamu wa picha wanaweza kutoa neno!!

Screenshot_20220209-120121.png
 
Sidhani kama yupo nchi hii, yupo ........
 
Back
Top Bottom