PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Hivi kweli polisi wataieleza nini dunia Maskini!! Yaani askari wote Hao wanamshambulia Mwanahabari Hadi Kumuua Badala ya kumshikilia kama alikuwa anahatarisha amani!! Sasa Polisi Kumi wanashiriki Kumuua Mwandishi Mmoja? Kweli Huu Unyama Umepindukia!!

Ila aliyotabiri Sumaye 2005 Yametimia! Eeeh Mungu Muweza Tuepushe na yote Haya!!
 
tanzania tanzania!nchi yangu tanzaia ,mama yangu tanzania!nakulilia mama yangu tanzania nakulilia tanzania!wanao hatujui adui yetu ni nani,na rafikia yetu ni nani!anayeahidi kulinda usalama wetu ndiye anayetengua usalamua huo,anayeahidi kututetea ndiye wakili wa aliyetudhulumu,anayelia pamoja nasi ndiye anayecheka na adui yetu,anayekuja kwenye misiba yetu ndiye anayelipia mauaji yetu!mama yangu tanzania uko wapi utunisuru,hataujui mchana wala usiku salama ni wapi!hatujui kichaka wala pepo tutasalimika wapi,hatuijui shibe maana njaa manusura yetu!nalia na mama yangu tanzania ainuke atupe ujasiri wa kusimama!nalia na mama yangu tanzania ikiwezekana atuzae upya maana uhai ulio sawa na kifo ni kheri nikabaki mfu!mama yangu tanzania inuka sasa tujitambue leo!inuka tanzania wanao hatujui tunakwenda wapi,inuka mama yangu tanzania tuonyeshe njia ya kupita maana juu yetu kuna chui,pembeni kuna simba,nyuma yetu moto,mbele yetu bahari chini yetu kuzimu.damu ya wanao tanzania inamwagika na bila shaka umechoka kuifyonza ,itapike sasa mama yangu tanzania itapike sasa na wanao ituloweshe tukijua kama leo sio sisi kesho yetu haipo mbali!walipowaua wenzetu tulinyamaza,watakapotuua sisi hakutakuwa na wa kutututetea.ole wako tanzania mama yangu na katika hili unyamaze!ole wako tanzania?ole wako na damu hii uinywe kimya bila kuicheua adhabu yako sitaki kuikadiria !
 
Huyu uzalendo na ubinadamu ulimzidi.......akipatikana atasema yote ya ukweli

 
Sasa hapa nadhani mmepata picha iliyochezwa kwa kijana aliekua akiuza magazeti na hatimae kuadai khakupigwa risasui bali ni kitu chenye ncha kali.
 
Huyu uzalendo na ubinadamu ulimzidi.......akipatikana atasema yote ya ukweli


hivi huyu askri anajisikiaje hapo,je angekuwa ni ndugu yake ndio katolewa utumbo huku akishuhudia nini angefanya.
waandishi wa habari endeleeni kuwa na uvumilivu,maana hii imepita ubinadamu
 
Kuna kila sababu ya kubadili mitaala ya kufundishwa hawa mapolisi wetu. naoana wanajua kutumia maguvu tu bila akili.
 
Kwa matukio haya Mwema, waziri wa mambo ya ndani wajiuzuru....maaskari waliohusika wafungwe maisha
 
mauaji ya kikatili namna hii kweli inasikitisha Mungu tusaidie....tatizo la uongozi dhaifu hakuna atakayechukuliwa hatua zaidi ya blabla
 
Serikali yetu sasa imeamua kutufanya kafara kwa siasa.

Mimi natamani kutokee siku ambayo CHADEMA itafanya mkutano na polisi wasiingilie ili tuone kama kuna mtu atakufa tena. Maana ni kama polisi hawapo kwa kuzuia ghasia ila kuua watu. Very bad. Machozi ya watanzania kwa hiki kipindi kigumu tunachopitia hakika yamebeba mambo mengi sana. Actually, yasituvunje moyo. Kuenzi na kuheshimu damu za wenzetu hawa ni kuongeza nguvu za mapambano.

Remember: "A GRAIN OF WHEAT AND THE SEEDS OF ITS OWN DESTRUCTION"
 
Rai yangu kwa polisi wote lazima wazingatie utu na kuwa makini kazini sio kama mnafyo fanya sasa kwani mpo kama mnajifunza kutumia risasi za moto kwa raia kama kuua basi ueni viongozi wa chama. nimeumia sana kwa vitendo vyenu pia mfahamu katika picha hizi na zingine tunaziona SURA ZENU ipo siku wewe askari utakutana na hasira ya watu ukiwa peke yk kwani si tumek uona katika picha hivyo lazima uwe makini katika kutekeleza majukumu yako hata kama umetumwa KUMBUKA KAULI YA RAISI YA MBAYUWAYU
 
Mungu amlaze mahala pema ndugu yetu, mpiganaji mwenzetu Daudi Mwangosi.
 
Hao ndo askari wetu ambao hawawezi hata kufikiri japo kwa asilimia ndogo kabisa-walikuwa na bifu naye tu. Mbona majambazi wanatesa wanavyotaka?

Sheria ichukue mkondo wake.
 
Askari wote wako loaded, hakukuwa na sababu, risasi za moto kwenye mkutano wa siasa wapi na wapi, mbona ngao wanazo nyingi tu kwaandamanaji hawaendi na silaha mikutanoni, labda Rage, wengine tuliobaki tunaenda bila silaha.
As of now tunataka tamko la CDM la kumtaka RPC kuresign na kufuatiwa na mashitaka juu yake,mtu hawezi kuuliwa tena zaidi sana kuuliwa hvi,we must act now or never,hivi vitu vinaumiza lazima watu wawjibishwe,i am serious ktk hili lazima watu waresign,say it Dr Slaa,hatuwez kuwa kimya kwa hli............God bless Tanzania
 
Planned Murder by Police!! Picha inaelezea Vizuri!!
 
Mungu amrehemu ndugu yetu, mtanzania mwenzetu!
 

....acheni kuandamana mnasababisha vifo kwa wasiohusika..shame on chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…