PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa



OCD aliyeumia katika tukio na ambaye yuko critical condition hospitalini ni yupi katika kundi hili? Au huyo aliyevaa kiraia? Waliopo Iringa wanaweza kutupasha maana wanawajua watu wao.
 
Very sad.....hakuna jambo lolote ambalo linaweza ku-justify jambo hili!
 
Ushahidi huu apa eti police wanakanusha kweri wana akili angalia jamaa anavyo mlenga ili amuue untaka tume ya nini hapa au unataka ushahidi gani mwingine huyu police niwa wapi na sale alizo vaa nizanani ccm mmekuwa mawakala wa kuua watu kwa kutumia jeshi la police why?
 

Attachments

  • Mwangosi.jpg
    26.6 KB · Views: 2,462
Inasikitisha kusikia watu wanasema atiwanaunda tume ya kuchunguza mauaji haya ya kikatili .................. mambo mengine ni ya kutibuana nyongo!!
 

Hata mimi nashangaa sana tume na ushahidi wa nini wakati vipi wazi? Kipoteza hela za walipa kodi tu.
 
Huwezi amini kama mambo haya yanatokea katika nchi ambayo viongozi wake wanakesha wakiisifu kua nia ya amani na utulivu!! Wapi dhaifu, aliyekua akinadiwa na walamba miguu wake kua ni kipenzi cha wanahabari?
 
kwa tukio hili linaniondoa katika ubinafsi wangu wa kumuomba MUNGU anitete na kuanzia sasa nitasali pia kwa nchi yangu na nimeamini kuwa utawala tulio nao ni mgumu mno kuzidi kipindi chochote kile.
tumekuwa na viongozi wabinafsi wasio taka mabadiliko wako tayari kuua ili mradi wao watawale haya bwana lakin nawaomba wadanganyika wenzangu tufanye mawili
kwanza tuendelee kupiga kelele kwa pamoja kwa sababu hili linaweza kutusaidia katika kuwaangamiza
cha pili tuungane kwa maombi kuiombea nchi yetu na tusali kwa imani zetu kweli kweli utawala huu sio kabisa
haya si mambo kabisa sijawahi kuona katika management yoyote rpc anashiriki moja kwa moja katika oparation ya mauaji na yeye akiwa mstali wa mbele! hii ni aibu sasa wanaunda timu ya nini kama si kula kodi yetu kiduchu waliokusanya kutoka kwa wadanganyika.
police wanausishwa na mauaji mengi ya raia wasio na hatia na mengine yanafichwa lakni MUNGU hawezi kukubali
basi wale wenye upako tupeni mistali ikiwezekana kila siku tuitumie kukomboa nchi yetu katika utawala huu wa shetani anayewalazimisha watoe makafara kwa kuua
 
Ogopa mtu mwenye division 4/o then anafanyakazi ambayo inafanyika kwa AMRI pekee.
 
Walipoua Arusha, wakatelekeza majeneza nini kilifanyika zaidi ya kuchunguza halafu yameishia hapo. Baada ya kugundua hakuna linaloweza kutokea wanaendelea na hawata acha kuua mpaka watakapotakiwa kufanya vinginevyo na wenye mamlaka ya kuwapa amri ya kusitisha mauaji. Naamin Jeshi la polisi linamfumo wa utawala na wanaotoa amri ya kuua raia wapo kwenye ngazi mojawapo ndani ya Jeshi na wengine nje ya jeshi...
Kwa nini polisi wanatumia nguvu nyingi kiasi tunachokiona kama si wamepata baraka kutoka kwa watawala wa nchi!? Kama sivyo sivyo IGP alitoa tamko gani kwa mauaji ya Arusha na hatua gani zilichukuliwa?

Mwanzo mzuri wakuwafanya waTz wawe sugu na wakatili. Tutafika huko wanapotupeleka na haitakua kheri sana. IGP unanafasi kubwa kuwatumikia raia nje ya siasa. Ukiendelea kuangalia haya mambo yaendelee hivi ataandika historia mbaya kwa taifa lako.
 

Nadhani nipo sahihi kabisa katika kuisoma picture ,nasikia Chanell 10 kuna mtu anasema kuwa marehemu alikuwa akiozozana na afisa wa polisi.Nadhani walianza tembeza virungu na kumsukuma,sasa huyu jamaa alikuwa hana balance na hivyo kujizua aianguke akatafuta support.Sasa kama ameshika kamera basi option ilikuwa kushika kiuno.Sasa hapo ndipo mambo yakaanza enda fasta hadi yakatokea haya.Hapa hata polisi nadhani walijikuta ghafla hapo, tafsiri zilizopita ghafla katik vichwa vyao(reflex actions) .

Kosa la kwanza nadhani ni kujaribu mweka chini ya ulinzi kwa style ya nguvu, ndio iliyopolekea kushikana na pengine haya.Huyu polisi anaweza kuwa alikuwa na papara,huku akiwa na silaha ya moto.Sidhani kama alijiandaa kuua.Kama ndivyo angetumia risasi kwani bomu limedhuru wengi, na lingeweza ua hata bosi wake.

Napata picture huyu askari alidhani akimpiga nalo jamaa pengine angepaliwa na gas ya machozi,bila kujua lilipaswa lipukia kwingine halafu moshi umwendee.Polisi hawakufundishwa vyema kuhusu matumizi n aimpact ya silaha+ pia hawa polisi si maalumu kwa riots.

Bado kwa style aliyokuwa amemshika huyo askari kiunoni huyo askari angeweza lalanae chini ghafla na kumbana wakati wengine wakizuia bastola kama walihisi kuwa anataka chukua silaha.wangeweza m sandwich kiasi cha kunyima nafasi ya kutumia silaha ya kamanda kabla ya kumuweka under control. Pia walikuwa na bulet proof karibu wote.Inaelekea kuna mambo mengi yanatokea kwa kutoelewa ,zaidi ya haya ya kisiasa na kujipendekeza.Sura za wale polisi wawili zinaonyesha hisia,ghafla wamekuwa km raia na kubaki speechless.Yanapita mengi sana vichwani.Mwangalie aliyeshika shield na anayetoa mask.wengine nadhani walichelewa ona hiyo kwa makini.

Itakuwa Kesi ngumu kwani matukio yalivyofikisha hapo ni questionable, na polisi tayari wamekuwa na picture mbaya.sidhani kama wataachiwa pumzi.Na upande wa marehemu nao watakuwa na stake kubwa waki compromise.Mbaya report lazima itoke hadharani na ikitoka kwa majibu yoyote yale ni damaging sana.Nadhani hiyo tume inahitaji kuwa makini sana.

Bado nasoma psychology ya polisi katika tukio.
 
Pole sikuwa namaanisha bangi ila moshi wa mabomu. Hiyo picha yako itakuwa ni diffence ya polisi, marehemu anaonekana kakamata silaha ya askari.

nope!! ile aliyokamata marehemu ni video camera ,
 

Remember ours are not riot police, they are Field Force Unit, they are not trained to negotiate they are trained to attack when confronted, when they ask you to disperse, you simply disperse, you never ever confront them or seek refuge to them. Do not think they are called Field Force Unit for nothing, they are brutal than police dogs.

All their life they are isolated, they do not have pity or regret, they do not know what is mercy. And when you confront their master (commanding officer), no matter, to seek refuge or to surrender, they simply do not know that. Those are trained to use maximum force with a simple order of "disperse". There is no word "attack" in their training, they do not even know what it is. What they know is only one thing, to disperse you with maximum force, if you confront them they still disperse you with what ever means, and that is exactly what happened, they dispersed him indeed.
 
Leo nikiwa naelekea nyumbani nimemsikia mtu anayeitwa makene akiojiwa (KISS FM) kama mwandishi wa habari
alitoa maelezo akisema RPC alikuwa kwenye gari na alienda kugongewa na mwandishi mwingine akamuokoe David Mwangosi RPC alifungua kioo na kufunga kioo hii nimeiona tena ITV





Je RPC kwenye PICHA katoka wapi? kwenye hii picha? Je n00b na Tumaini Makene wametoa wapi hii picha?

 
Picha haijachakachulia ni sawa na ile ya mwanzo. Alichofanya ni kuweka mishale na maelezo kwenye picha.
 
tell it to the birds!!! acha ukada wa kipumbavu wewe.. kuna maisha ya baba wa mtu/mume wa mtu yashapotea hapa

Usilete upumbavu wakati watu tuna hasira ya kumpoteza ndugu yetu
 
hapo hamna cha fotoshop, inaonyesha wazi kabisa marehemu amemshikilia RPC hapo...na polisi anamuelekezea bunduki ya bom la machozi marehemu aliyelala chini, sasa mtuambie, huyu aliyezungusha mikono kwa RPC si marehemu? na aliyezungushiwa mikono si sura ya RPC kwa wale wanaomfahamu?..je kama ilishafika kipindi marehemu akazungusha mikono kwa rpc live hivyo, ni vipi kama utasema bom lililipuliwa baada ya rpc kuondoka yeye hakutoa maelekezo ya kumwacha marehemu asipigwe au aliona kuna habari ya utata itatokea ambayo marehemu anayo akaagiza afyatuliwe? tujue nini hapa sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…