PICHA: Hii biashara ya usafirishaji wahamiaji inafanywa na matajiri wakubwa wenye connection na vigogo

Wana miili ya afya hao kilo hazizidi 55
 
Mikataba ya nchi na nchi, Kenya wanaingia bila Visa hapa kwetu lazima wawe na Visa na SA wanatakiwa wawe na Visa. Sisi tunaisaidia Ethiopia kuwadhibiti na tunaisaidia SA pia
 
Mkuu inaonekana uko Pre-occupied na ubaguzi na udini.

Kwenye comment yangu nimetaja wapi Ubaguzi au Uislam?
 
Mikataba ya nchi na nchi, Kenya wanaingia bila Visa hapa kwetu lazima wawe na Visa na SA wanatakiwa wawe na Visa. Sisi tunaisaidia Ethiopia kuwadhibiti na tunaisaidia SA pia
Mkuu...! Kwa Mwafrica ukiwa na Passport na unasafiri toka Nchi Yako na unapita Nchi kama 3 mpaka kufika unapokwenda, huitaji kuomba Visa Kwa kila Nchi unayopita, wewe unajurikana kama ni TRANSIT, ukifika Boda unaulizwa unakokwenda, kama unapita tu kwenye Hiyo Nchi, unawaambia wewe ni TRANSIT.

Watakupa siku hazizidi 7, kwamba Kwa vile wewe ni TRANSIT na unapita tu kwenye Nchi Yao, ndani ya siku hizo uwe umevuka tayari, otherwise wakikukuta ume overstay ni Jela.

Lakini sio Kwa Hawa Wasomali, Hawa wapo Transit tu...!

Labda kama Kuna Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia kuwakamata kila Waethiopia wanaopita hapa.
 
Utakuwa hujawahi kusafiri? Hebu tuambie wewe ukikata Visa ya Misri utapita Kenya bila mahitaji ya visa je Ethiopia na Sudan utapita bila Visa?
 
Kwanini wasipitie Uganda Kisha Kongo
Kongo kwa barabara hamna kitu kutoka dar mfano kwa barabara kama unataka kwenda Kinshasa utatumia miezi mitatu

Tanzania haikwepeki kwenye safari yao ya kwenda South Africa sababu wakitaka kupitia kongo lazima wapitie Kenya Uganda halafu waingie Eastern kongo kwenye waasi kama wote wataporwa kila walichonacho wakiweza ndio wasafiri hadi lubumbashi
Wasomali wanakuwa na passport waethiopia hamna

Tanzania pia ni wahanga hili swala watanzania kibao wanakamatwa Afrika kusini hawana passport sababu ya ugumu kupata wanarudishwa nchini asante kwa mahakama huwapiga faini ndogo elfu 50 na kuwaachia faini ambayo ni ndogo kuliko bei ya passport kama serikali ingewapa bila longolongo asante mhimili wa mahakama kujitambua na kutambua changamoto ya waomba passport wanapata na kuwapa hukumu ya huruma

Mahakama mbariiiwe
 
Pia kuna boda au route ya kupitia Mozambique huwa wanatumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…