Copied from somewhere, may help some...
UKIWA NA GARI BARABARANI ONGEA VIZURI NA RAIA WA KUDUMU WA BARABARANI NA HESHIMU BARABARA
Kuna taarifa za Ajali na Vifo nimezisikia na zinahusu Watumishi wa Serikali... Nimeona nije na ushauri maridhawa kwa watu wanaotumia hasa barabara kila siku na ni Watumishi wa Serikali...
Siku moja nilikuwa Arusha maeneo ya Njiro ile Moshi Road tukiwa na gari STL Pick Up Nyeupe... Mie nikiwa Boss na hapa makutano ya barabara (TRIPPLE A) kuna Mataa... Dereva hakuzingatia maelekezo ya taa bali alipita kwa kuangalia hali halisi... Mbali kule kulikuwa na Askari wa Usalama barabarani na aliuona ule UTOPOLO ambao tulifanya...
Tulipofika kwake akatusimamisha na swali la kwanza akamuuliza Dereva... Umefanya nini?? Jamaa akaanza kujitetea sijui namuwahisha boss... Katika mazungumzo Askari akasema... Unapokuwa barabarani ongea na Raia wa Kudumu wa Barabarani.... Dereva akajibu Ndiyo Mkuu... Kisha Askari akamuuliza.. Unawajua Raia wa kudumu wa Barabarani?? Ikawa mtihani... Nami nakuambia leo... Barabarani ongea vizuri na Raia wa kudumu wa barabarani na heshimu barabara....
Hizi barabara na magari hawajui cheo cha mtu... Wao wana Sheria zao na miongozo Katiba na Kanuni zao.... Ukizingatia basi wewe na gari wote mtakuwa salama...
Hebu fikiria wewe ni Mkurugenzi wa Taasisi iwe kubwa au ndogo au nyeti au kivipi... Juzi juzi Tumenpoteza DAP wa Msajili wa Hazina na sasa tushamsahau, tunapoteza viongozi wengi na tunawashau na ofisi zinawasahau... Halafu Serikali inanunua magari mengine...
Sasa ukiwa Kiongozi ama dereva wa Serikali mkiwa barabarani kumbukeni mambo yafuatayo
1. Barabara na gari mlilolopo na magari mengine hawajui vyeo vyenu na hamuwezi kuwatisha...
2. Ukipata Ajali utakufa hata usipokufa utapata mateso sana na hapo barabara yenyewe itaendelea tu kuwepo...
3. Ukifa katika Ajali Familia yako utaiacha na itapata mateso na tabu nyingi duniani...
4. Ukifa katika Ajali familia yaani mwenza na watoto wako na wategemezi wako wataondolewa katika nyumba ya Serikali, wataondolewa nafuu za maisha ulizokuwa nazo kama Umeme, maji, Internet na hata school bus...
5. Familia yako itaanza kupata taabu ya kufuatilia mirathi na kwa ofisi ambayo leo wewe ni Boss watapretend hawawakumbuki na watawapa usumbufu mkubwa...
6. Huku nyuma Utaacha mtafaruku mkubwa miongoni mwa familia yako na ndugu zako maana cha muhimu ndugu watakimbilia mirathi na hata kajumba ulikojenga Ilazo watafikiria namna ya kukauza ili kumaliza fitna...
7. Mweza wako (Mke au Mme) atapata mtu mwingine ambaye atarithi starehe yako tu watoto wako watapambana na hali yao...
8. Serikali itaweka mtu mwingine mahali pako maana wako wengi tu nje..
9. Mwisho.... Kule kazini kwako utasahaulika na utabaki tu kwenye orodha ya waliowahi kuwa wakubwa hapo ila hao watumishi waliopo leo watahamishia mahaba yote kwa kwa atakayerithi mahali pako..
Ni maumivu Taifa kupoteza Mtu kwa ajali... Tuzingatie Usalam barabarani.... Maisha hayana second option..